Nia ya Dhati ya Wanaharakati Kumshtaki Livingstone Lusinde kwa Child Abuse

Wadau hebu nipeni mifano ya matusi aliyetukana huyo lusinde kwani huku songea umeme unakatika sana sikuweza kufatilia mikutano yote ya kampeni.
 
Si vizuri kujumlisha kuwa wagogo wote ni wajinga, tujaribu kuchangia si kwa kuwashambulia wana Mtera hata hivyo sio wagogo wote
 
Kwa ujinga wa wagogo watamchagua tena kwa kishindo njaa yao kubwa ni ubwabwa na choya.

:shut-mouth: Una uhakika kuwa Lusinde amechaguliwa na Wagogo wote? Si vizuri kuchangia hoja kwa kushambulia utu wa watu kama anavyofanya Lusinde mwenyewe. Twende kistaarabu
 
Mpaka mtu kama huyo kuja kupata uongozi ujue kuna tatizo kubwa katika jamii nzima, wala si yeye tu.

Ana ubingwa gani wa kuficha kichaa chake ngazi zote hizo aje kukionyesha leo?
 
Hakimu atakae sikiliza kesi amfunge mwaka mmoja jela na viboko sita anapoingia na anapotoka viboko sita tena akawaonyeshe wabunge wenzie wa ccm kuwa kutukana mbele ya hadhara sio vizuri.
 
Mdau na Wana JF,
Kwa kweli Mbunge Lusinde amepitiliza kuteleza, Cha Muhimu ni Kumwombea kwa Mungu na Kumkabidhi kwa Mungu, ukipanda mchicha hutavuna Mchicha, wamevuna walichopanda, Watanzania wa leo sio Watanzania wa miaka ile,
Hivi hizi semina, warsha haziwasaidii kujua wajibu wao kama Mbunge, Kiongozi wa Jamii, Je hawajui Uongozi ni dhamana ??? Na wenye Nchi ni Wananchi waliowachagua ??? Wanafikiri watafanya, kusema na kutisha watu milele ?? Am so speechless kuhusu hili, mimi nimemsamehe BURE.
Mungu ana Mpango madhubuti na watu kama hawa.
Nawakilisha


Wadau naomba tuziweke pembeni siasa katika kujadili mada hii, tuweke michango yetu kwa nia ya kulitimiza hili....maneno aliyoongea Mbunge Lusinde yametugusa sana sisi wanaharakati wa haki za watoto, ukizingatia kwamba kulikua na watoto wadogo pale ambao waliyasikia..technically, he did abuse those children..kwa hilo basi, tuna nia ya kulifikisha shauri hili katika vyombo vya sheria ili wanasiasa au watu wenye tabia ya kuongea offensive and abusive words mbele ya watoto wafahamu kwamba watawajibika kwa matamshi yao kisheria!

1. tunaomba weledi wa sheria za kitaifa na za kimataifa; hasa katika Child Rights' watoe mwongozo katika hili...

2. tunaomba wakazi wa Arumeru, waandishi wa habari, au yeyote aliyehudhuria mkutano ule awe tayari kutoa ushahidi, ikibidi mahakamani...

3. tutashirikishana katika kila hatua itakayoendelea katika hili..

3. ikibidi tuwe tayari kwa michango ya hali na mali ili kufanikisha jamobo hili....

Mwisho; tukumbuke kwamba mtoto wa mwenzio ni wako........nakaribisha michango na ushauri...
 
huyu lusinde anapaswa kufikishwa mahakamani mara moja, hakuna mjadala katika hili. kazi kwenu wataalam wa sheria
 
Hizi ni siasa. Mtu amevunja sheria za nchi, tunaanza kupindisha pindisha, ya nini? Amefanya kosa la jinai. Yeye na wote ambao hawakumchukulia hatua - polisi waliokuwepo na viongozi wengine wa ccm. Wote wakamatwe wajibu mashtaka.
 
Maneno alosema Lusinde yangekuwa yamesemwa na Mbunge wa CDM saa hizi kesi ingekuwa ishafunguliwa na keshahojiwa na pale Clouds FM ingekuwa ndo Topic!Naomba wanaojua sheria watusaidie kufungua kesi juu ya huyo Lusinde plz
 
Back
Top Bottom