Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
NI WAKATI SAHIHI KWA SERIKALI KUANZISHA SHERIA ZA PRENUP KWA WANAOTAKA KUINGIA KWENYE NDOA KUEPUSHA MATAPELI.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Huwezi ukawa na sheria ya Talaka alafu muda huohuo isiwepo sheria ya PreNup. Huko ni kutengeneza mazingira ya utapeli, dhulma na kuifanya ndoa isiwe ya Haki.
Ni wakati sasa Serikali ipeleke mswada bungeni ili iundwe sheria ya PreNup Yaani makubaliano ya Wenza hasa Wachumba kuhusu mgawanyo wa mali utakavyokuwa kabla hawajaingia ndoani pindi tuu wakapoachana.
Kama kweli Watu wapo Serious na ulimwengu wa sasa na wanataka ndoa ziendelee kuwepo basi sheria ya PreNup haitaepukika. Vinginevyo idadi ya Watu wanaokimbia na kuipinga ndoa itazidi kuongezeka maradufu.
Vijana wengi wa sasa wanajifunza mengi hasa yale mabaya yanayotokana na ndoa. Wanaona wanaume wengi wakipasuka na kuchukuliwa mali zao na wale walioitwa wenza wao.
Vijana hawataki kuoa. Moja ya sababu yao kubwa ni hiyo ya kugawana Mali.
Jasho la mtu haliliwi, lazima mtu aonee uchungu jasho lake. Ingawaje matapeli na wenye dhulma vijana hawa hawana hoja lakini ukifuatilia vijana wanahoja.
Unataka tuingie Ndoani tunasaini makubaliano ya kugawana mali endapo itatokea tutaachana.
Hii itafanya kila mmoja afanye kazi kwa bidii.
Pili hii itadhihirisha mapenzi ya kweli ya wahusika hasa wanawake ambao wengi ni walemavu wa akili na ombaomba ambao hutaka mserereko.
Hii itachochea nguvu kazi yote ya nchi hasa rasilimali Watu kutumika ipasavyo,
Hii itaepusha malalamiko ya wanaume kuwa wanatapeliwa mali na nguvu zao. Lakini pia itachochea wanawake kufanya kazi na kutodhulumiwa haki zao hasa za jasho lako.
Masuala ya Dini hapa hayana nafasi kwa sababu sisi sio dini moja.
Masuala ya utamaduni hapa hayana nafasi kwa sababu sisi sio Kabila wala ukoo mmoja.
Masuala ya kusema dini sijui utamaduni wetu hizo ni kauli za kisiasa ambazo zimekaa kitapeli tapeli. Sisi sio Dini moja, hatuabudu Mungu mmoja, hatutoi kabila moja.
Sheria ndio itakuwa muongozo wetu. Masuala ya kusema utamaduni wa Muafrika ni kauli za kijanja janja. Afrika ina makabila zaidi ya elfu moja yenye tamaduni tofauti. Huo utamaduni ni upi unaoitwa utamaduni wetu.
Kama tumeamua kufanya muingiliano wa Watu iwe kikabila au kidini huwezi leta mambo ya utamaduni wetu wakati sisi ni Watu kutoka maeneo tofautitofauti. Hapo kinachotakiwa ni kuunda sheria mpya za Watu walioamua kuchangamana.
Vinginevyo hili kundi la kataa ndoa na idadi ya single Mothers itaongezeka kila kukicha na itafikia hatua ndio itakuwa maisha ya jamii yetu.
Ndoa itaonekana ni utapeli, dhulma, ujanjaujanja.
Sheria hii itaepusha maisha ya kubet bet. Maisha yasiyo na uhakika.
Yaani ati ndoa au kupata mwenza inachukuliwa kama mchezo wa kubet wakati tunaweza kuweka sheria ili Watu waishi maisha ya uhakika. Huu ni ujinga wa hali ya juu.
Hii itasaidia pia kuondoa tamaa kwa wale wanaotaka kuoa au kuolewa na Watu wasio hadhi sawa ili wapate Mali. Kila mmoja ataoa au kuolewa na mtu wa hadhi yake, wanaofanana kama ilivyo kanuni ya asili kuwa ndege wafananao huruka pamoja.
Wewe kama ni maskini kaoe au kaolewe na maskini mwenzako ili siku mkiachana usijisikie vibaya mnapogawana mali kwa sababu uwiano utakuwa unakaribiana.
Lakini wewe kipato chako ni laki moja, unaolewa na mtu mwenye kipato cha milioni tano alafu siku mkitaka kugawana mali baada ya kutengana mnaanza kukamiana kwa sababu huyu mwenye kipato kikubwa ataona amedhulumiwa alafu na wewe utajifanya unataka nyingi kisa ulichangia vitu vilivyoonekana.
Nimemaliza.
Acha Nipumzike
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam