- Thread starter
- #81
huwezi kumpangia mtu mmoja mmoja kima cha mshahara specific kwake tu! Marekani kuna minimum wage kwa wafanyakazi wote na muda wa kufanya kazi na overtime n.k na vinaongozwa na sheria.. kutokea hapo unawez akupanga chochote na hakipangwi kwa kuangalia uzalishaji wa mtu mmoja mmoja. Tunaangalia gharama ya maisha n.k. Kwa maoni yako kwa Tanzania mfanyakazi wa kawaida anahitaji kama kiasi gani kwa mwezi kuweza kumudu maisha? Sidhani kama ni swali gumu sana.
Mwanakijiji
mimi nafikiri mnataka kupotosha, nafikiri hakuna mahala binadamu kuna mshahara unaomtoshesheleza. Hawa watu wa europe sijui huko marekani, kama mishahara inawatosha mbona maisha yao ni ya madeni?? kukopa kila kitu. Wanaishi kwa benki.
Imefika mahala hata simu ya mkononi hawawezi toa keshi, simu wanakopa. tusidanganyane hapa ni ukweli wanakopa kwa sababu keshi inapiga chega, hakuna anayependa kukopa kama keshi ipo.
Hakuna kima cha chini ambacho utaweka eti useme hiki kitawatosheleza watu wangu. Kima cha chini kinatakiwa kuwa kile ambacho serikali inaweza kua affford yenyewe kuwalipa na kutoa huduma mhimu. Concrete namba huwezi toa kirahisi kama mnavyotaka kuwa.