Ni ukweli mtupu Mshahara wa kima cha chini TUCTA wanaoutaka hautekelezeki

...Mkuu MkamaP, heshima yako. hawa wawakilishi wetu wanaopokea milioni 9 kwa mwezi na bado wanajenga hoja ya kutaka kuongezewa nyingine wanachapa ama wamechapa kazi gani ya kuimarisha uchumi kuhalalisha malipo wanayojilipa? mawaziri je?

Mkuu Baba
Sasa kama wawakilishi wanaopanga hiyo bei ndo wanajiripa hivyo ,sasa ni nani kati yako ama Kikwete anayetakiwa kuwawajibisha wawakilishi ili wajiripe kidogo. ?
Mkuu. Nafikiri track letu limekatika somewhere wananchi ndo wamelikata hasa hawa wafanyakazi. Kama wanajua kikwete ndiye tatizo wangeligoma na uhakika Kikwete angejiuzulu ndani ya week.
Yani kila sehemu wagome hospitali, umeme,tanesco,shule,vyuo nk wewe unadhani kikwete angetoka kwa gear ipi? zaidi kama gear ya Mbeki. ? Ile biti ya Kikwete kwamba wapo wengi wanaotafuta kazi si kweli , wakigoma hakutaendeka kitu.

Lakini kwa kuwa tucta wanajua hiyo kitu haiwezekani wanazuga zuga tu kwa mitaji yao. Rais kisha sema kura wasimpe hiyo mshahara haiwezekani .
 
Yale makontena yapo pale kwa sababu ya hawa wanasiasa ambao wanalipwa pesa nyingi katika pato la taifa na hapo hapo wanapewa asilimia 10 kwa hao wanaoitwa wawekezajiwezi wetu. Period.

Yawezekana ni kweli ama si kweli
Wale wafanyakazi nina uhakika wanalipwa zaidi ya kiwango ya tucta ya chini wanayo propose.
Sasa wewe tuma pale gari uweke na radio mle ndani. Ndio utajua sio wasana siasa tu
 
mkuu, nakubaliana na wewe kuwa tanzania ni nchi masikini. Kama hatuwezi kupanga kcc kuwa hiyo laki tatu, mbona wanajipangia mshahara wa mbunge kima cha chini ni milioni 7? Wakiwa kwenye kikao laki na 30. Huko pesa zinatoka wapi?

Swali langu kwako na wenzio ni lile lile kama kweli mnafahamu hesabu kama mnavyotamba kumsahihisha bakari :

1 + 1 = ___?

1 + 1 = 3 (synergy)
 
Wakuu zangu nadhani ipo haja ya kuzungumza mambo yanayojenga badala ya kubishana hapa kipi kingefanyika..Hili neno KINGE - fanyika imeisha pitwa na wakati, la muhimu ni kuutazama vizuri Utawala wa JK na CCM kuorodhesha makosa ya makusudi ambayo ndio sababu kubwa tumefikia hapa.

Hali ya msiha Tanzania ipo juu sana kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya tena basi zile zilizoendelea. Maisha Tanzania yapo juu kuliko Marekani na Canada kwa uhakika kabisa na sababu kubwa ni kwamba nchi yetu ipo ktk VITA Kiuchumi. Sasa mimi sielewi kama vita hii inatokana na Umaskini au Uzalishaji mdogo wa ndani lakini lililo wazi ni kwamba Tanzania sawa na nchi zilizo vitani kama Kongo, maisha yetu yamepanda sana kuliko hali halisi.

Mfumko wa bei uliopo Tanzania hauna kipimo cha kiuchumi zaidi ya kufikiria kwamba tumetoka ktk mfumo wa Uzalishaji kukidhi Mahitaji (Demand and Supply) na tumejenga mfumo wa SHIDA na KUJIKIMU kiuchumi kutokana na uwezo mdogo wa kuzalisha ndani kukidhi mahitaji yetu. Tatizo kubwa ni uthaminisho wa fedha yetu toka mali inayoingia nchini kujikimu hali tupo ktk vita ya Umaskini. Ni sawa na Kongo ambako kutokana na vita ya wenyewe wananchi wameshindwa kuzalisha ndani wakiwa vitani hivyo wanategemea walanguzi kutoka nchi za jirani kuleta mali (supply) kwa mahitaji yao.

Sasa kibaya zaidi ni kwamba mahitaji yao yamekwisha ondoka ktk demand ila ni SHIDA hivyo ushindani unakuwa sii kwa wazalishaji (supplier) ila ushindani upo kwa Wanunuzi. Na hali kama hii husukuma juu bei ya vitu (inflation) isiyokubalika kiuchumi. Na Hata mzunguko mkubwa wa biashara unaoonekana huko Kongo huwa hauna maana yoyote kiuchumi kwa nchi hiyo isipokuwa kuididimiza zaidi ktk lindi la Umaskini. Mfumko wa bei kama hauwezi kufanyiwa utafiti wa hali ya juu kutambua kwanza sababu yake ni kazi bure kabisa kuchukua hatua ambazo hazilengi kuondoa sababu zilizo sababisha SHIDA hizo.

Tanzania tuna shida kubwa ya Uzalishaji.. SHIDA kubwa sana kiasi kwamba nyumba hazitoshelezi ni shida, usafiri hautoshi, shida tupu. Vyakula havitoshi mahitaji yetu, maji hayatoshi, Umeme hautoshi, huduma za Afya hazitoshi, Shule, walimu na vifaa havitoshii..Yaani kila usambazaji wa mali na huduma utakayofikiria ni SHIDA tupu. Hivyo bei za huduma zote hizi ni bei za kuchonga, yaani hazina Uhalali wowote kwa asilimia ya faida au karibu na ukweli wa bei inayotakiwa. Na fedha ambazo znatengwa kuimarisha miundombinu ya vitu hivi haifiki kunakotakiwa. Nusu kama sii robo tatu ya fedha hizi hubakia mifukoni mwa watu na kufanya mzunguko unaopandisha mfumko wa bei ktk uchumi wa kujihami..

Hakuna sababu kabisa ya nyumba ya Kupanga Kinondoni ipangishwe kwa dollar 200 kwa mwezi kisha mpangaji anatakiwa kulipa kodi ya mwaka mzima! hakuna sababu zaidi ya uchahce wa nyumba za kuishi na fedha kuwa mifukoni mwa baadhi ya watu wachache wanaoendesha soko hili. Hakuna sababu Kilo moja ya Nyama kuuzwa Tsh 3,500 hali mwenye Butcher hawezi kumaliza kuuza ng'ombe mmoja kwa siku. Huyu muuzaji hana haraka, kapanga sehemu ndogo tu akilipa 500,000 kwa mwezi, ng'ombe bei juu machinjioni na kwa asili mchungaji Mmasai hachungi ng'ombe wake kwa ajili ya kuuza nyama isipokuwa mnyama huyo ni Pet wake...Hivyo kiuchumi hakuna mfumo wa Ufugaji wa ng'ombe kwa ajili ya nyama. Haya tazama Uvuvi, tuliambiwa na Wataalam athari za uvuvi wa Sangara, tukawabishia Wataalam kwa sababu ya tamaa ya utajiri wa haraka..matokeo yake leo hii samaki wanakwisha ziwa Nyanza (Victoria), hata hao sangara wenyeweni adimu kutokana na upungufu wa hewa safi (oxygen). Leo hii Wananchi wa kanda ya ziwa wanalia njaa, samaki hawashikiki bei kwa sababu upatikanaji wa samaki ni SHIDA kubwa nje ya kuwa mahitaji ya kawaida. Na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhakikisha hali hii inakabiriwa kabla haijawa too late.

Hivyo hivyo ukitazama sekta nyinginezo utagundua kwamba Tanzania tupo ktk Uchumi wa KUJIKIMU tukiagiza mali toka nje kuondoa shida zilizopo, ili hali uzalishaji wa ndani haupo kabisa na kama upo basi hauna malengo ya kuondoa SHIDA zilizopo ndani. Hivyo basi hatuwezi kufanikiwa kwa kujikimu wala hatuwezi kufanikiwa kwa kutoagiza mali toka nje kwa sababu hatuna uzalishaji wa ndani.
Na hatuwezi chukua mfumo wowote wa kiuchumi kujikwamua ktk adha hii pasipo kuondoa kwanza dosari kubwa za kiutawala. Kubwa kuliko yote ni Utawala wa CCM ambao umejenga mahekalu ya Rushwa. Rushwa ni adui mkubwa sana wa uchumi wa KUJIKIMU ambao mara zote huwa ni dharura. Rushwa inapoingia ktk uchumi wa kujikimu basi huzidisha Umaskini na hata Inflation hupanda kinyume cha mapigo ya kawaida.

Pili, mfumo wa ukusanyaji kodi na matumizi ya serikali ni mbovu sana. Sielewi hadi leo kwa nini Mkapa alisifika kwa mfumo mbovu wa ukusanyaji kodi. Mfumo ambao unazingatia zaidi kukusanya chochote kinachowezekana pasipo kujali taratibu za kiuchumi. Unakuta mtu anatozwa kodi kabla kajauza mali yake wala kutazama ugharama wa mali hiyo kwa walaji. wapo watu wanaofanya biashara ya mabillioni hulipa kodi chini ama sawa na mfanyakazi. Kodi za kukadiliwa ni moja ya sababu kubwa zinazodhoofisha wajasiliamali na kuwatajirisha wachache hasa wale wenye kuendesha uchumi wa kujikimu. Bei zinapangwa kulingana na mlanguzi anavyojisikia na nguvu ya monopoly inawezeshwa kutokana na wahusika wenyewe kuwa ndio viongozi wa serikali na wenye mamlaka ya vibali vya uagizaji mali.

Wakuu zangu nisiwachoshe, Ile mada yangu ya HII NI NCHI ya WAJINGA inabeba mzigo mkubwa wa matatizo haya tulokuwa nayo. Mfumo wa Utawala uliopo ni mbovu sana kiuchumi. Matatizo ya Wafanyakazi sii matatizo ya Kikwete, wala hayatokani na kivuri cha Kikwete isipokuwa hata yeye mwenyewe kamezwa na mfumo hasi wa kiuchumi na utawala. Hakuna mtu wala kiongozi yeyote anayeweza kuleta mabadiliko nchini pasipo kuondosha kwanza mfumo mbaya wa kiutawala. Mfumo ambao unayatazama mahitaji yetu kama ni SHIDA iliyoletwa na Mungu, hivyo hakuna sababu ya ubunifu wowote isipokuwa kuishi kama tulivyopangiwa. Na hakika ukiniuliza mimi leo hii nitakwambia kwamba hizo Tsh 315,000 zinaonekana nyingi kwa sababu Tsh yetu inathaminishwa kinyume cha hali halisi..Kama ingethamanishwa Tsh 2600 sawa na dollar 1 (moja) basi tusingeitazama hiyo mishahara kwa kina hiki cha kushtua. Hizo Tsh laki 315 zingekuwa chini ya Usd 120 kwa mwezi na hata hizo bado ni juu ktk thaminisho kwani majority ya wananchinchini wanaishi kwa pato la dollar 1 kwa siku.
 
Mkandara
hizo Tsh 315,000 zinaonekana nyingi kwa sababu Tsh yetu inathaminishwa kinyume cha hali halisi..Kama ingethamanishwa Tsh 2600 sawa na dollar 1 (moja) basi tusingeitazama hiyo mishahara kwa kina hiki cha kushtua. Hizo Tsh laki 315 zingekuwa chini ya Usd 120 kwa mwezi na hata hizo bado ni juu ktk thaminisho kwani majority ya wananchinchini wanaishi kwa pato la dollar 1 kwa siku.
Tatizo wazalisha Takwimu pale BOT wanazo Data kamili za hali halisi ya uchumi wetu kwa kuangalia mfumuko wabei, na mambo mengine katika uchumi.
tatizo , wanahold kwa faida ya wanasiasa, hali halisi ndio hiyo. kabla hawajatoa kuna watu wanazipika hizo Takwimu, nakumbuka wakati fulani Lipumba(Prof) aliwahi kukosoa hali hiyo.
 
Wakuu zangu nadhani ipo haja ya kuzungumza mambo yanayojenga badala ya kubishana hapa kipi kingefanyika..Hili neno KINGE - fanyika imeisha pitwa na wakati, la muhimu ni kuutazama vizuri Utawala wa JK na CCM kuorodhesha makosa ya makusudi ambayo ndio sababu kubwa tumefikia hapa.

Hali ya msiha Tanzania ipo juu sana kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya tena basi zile zilizoendelea. Maisha Tanzania yapo juu kuliko Marekani na Canada kwa uhakika kabisa na sababu kubwa ni kwamba nchi yetu ipo ktk VITA Kiuchumi. Sasa mimi sielewi kama vita hii inatokana na Umaskini au Uzalishaji mdogo wa ndani lakini lililo wazi ni kwamba Tanzania sawa na nchi zilizo vitani kama Kongo, maisha yetu yamepanda sana kuliko hali halisi.

Mfumko wa bei uliopo Tanzania hauna kipimo cha kiuchumi zaidi ya kufikiria kwamba tumetoka ktk mfumo wa Uzalishaji kukidhi Mahitaji (Demand and Supply) na tumejenga mfumo wa SHIDA na KUJIKIMU kiuchumi kutokana na uwezo mdogo wa kuzalisha ndani kukidhi mahitaji yetu. Tatizo kubwa ni uthaminisho wa fedha yetu toka mali inayoingia nchini kujikimu hali tupo ktk vita ya Umaskini. Ni sawa na Kongo ambako kutokana na vita ya wenyewe wananchi wameshindwa kuzalisha ndani wakiwa vitani hivyo wanategemea walanguzi kutoka nchi za jirani kuleta mali (supply) kwa mahitaji yao.

Sasa kibaya zaidi ni kwamba mahitaji yao yamekwisha ondoka ktk demand ila ni SHIDA hivyo ushindani unakuwa sii kwa wazalishaji (supplier) ila ushindani upo kwa Wanunuzi. Na hali kama hii husukuma juu bei ya vitu (inflation) isiyokubalika kiuchumi. Na Hata mzunguko mkubwa wa biashara unaoonekana huko Kongo huwa hauna maana yoyote kiuchumi kwa nchi hiyo isipokuwa kuididimiza zaidi ktk lindi la Umaskini. Mfumko wa bei kama hauwezi kufanyiwa utafiti wa hali ya juu kutambua kwanza sababu yake ni kazi bure kabisa kuchukua hatua ambazo hazilengi kuondoa sababu zilizo sababisha SHIDA hizo.

Tanzania tuna shida kubwa ya Uzalishaji.. SHIDA kubwa sana kiasi kwamba nyumba hazitoshelezi ni shida, usafiri hautoshi, shida tupu. Vyakula havitoshi mahitaji yetu, maji hayatoshi, Umeme hautoshi, huduma za Afya hazitoshi, Shule, walimu na vifaa havitoshii..Yaani kila usambazaji wa mali na huduma utakayofikiria ni SHIDA tupu. Hivyo bei za huduma zote hizi ni bei za kuchonga, yaani hazina Uhalali wowote kwa asilimia ya faida au karibu na ukweli wa bei inayotakiwa. Na fedha ambazo znatengwa kuimarisha miundombinu ya vitu hivi haifiki kunakotakiwa. Nusu kama sii robo tatu ya fedha hizi hubakia mifukoni mwa watu na kufanya mzunguko unaopandisha mfumko wa bei ktk uchumi wa kujihami..

Hakuna sababu kabisa ya nyumba ya Kupanga Kinondoni ipangishwe kwa dollar 200 kwa mwezi kisha mpangaji anatakiwa kulipa kodi ya mwaka mzima! hakuna sababu zaidi ya uchahce wa nyumba za kuishi na fedha kuwa mifukoni mwa baadhi ya watu wachache wanaoendesha soko hili. Hakuna sababu Kilo moja ya Nyama kuuzwa Tsh 3,500 hali mwenye Butcher hawezi kumaliza kuuza ng'ombe mmoja kwa siku. Huyu muuzaji hana haraka, kapanga sehemu ndogo tu akilipa 500,000 kwa mwezi, ng'ombe bei juu machinjioni na kwa asili mchungaji Mmasai hachungi ng'ombe wake kwa ajili ya kuuza nyama isipokuwa mnyama huyo ni Pet wake...Hivyo kiuchumi hakuna mfumo wa Ufugaji wa ng'ombe kwa ajili ya nyama. Haya tazama Uvuvi, tuliambiwa na Wataalam athari za uvuvi wa Sangara, tukawabishia Wataalam kwa sababu ya tamaa ya utajiri wa haraka..matokeo yake leo hii samaki wanakwisha ziwa Nyanza (Victoria), hata hao sangara wenyeweni adimu kutokana na upungufu wa hewa safi (oxygen). Leo hii Wananchi wa kanda ya ziwa wanalia njaa, samaki hawashikiki bei kwa sababu upatikanaji wa samaki ni SHIDA kubwa nje ya kuwa mahitaji ya kawaida. Na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhakikisha hali hii inakabiriwa kabla haijawa too late.

Hivyo hivyo ukitazama sekta nyinginezo utagundua kwamba Tanzania tupo ktk Uchumi wa KUJIKIMU tukiagiza mali toka nje kuondoa shida zilizopo, ili hali uzalishaji wa ndani haupo kabisa na kama upo basi hauna malengo ya kuondoa SHIDA zilizopo ndani. Hivyo basi hatuwezi kufanikiwa kwa kujikimu wala hatuwezi kufanikiwa kwa kutoagiza mali toka nje kwa sababu hatuna uzalishaji wa ndani.
Na hatuwezi chukua mfumo wowote wa kiuchumi kujikwamua ktk adha hii pasipo kuondoa kwanza dosari kubwa za kiutawala. Kubwa kuliko yote ni Utawala wa CCM ambao umejenga mahekalu ya Rushwa. Rushwa ni adui mkubwa sana wa uchumi wa KUJIKIMU ambao mara zote huwa ni dharura. Rushwa inapoingia ktk uchumi wa kujikimu basi huzidisha Umaskini na hata Inflation hupanda kinyume cha mapigo ya kawaida.

Pili, mfumo wa ukusanyaji kodi na matumizi ya serikali ni mbovu sana. Sielewi hadi leo kwa nini Mkapa alisifika kwa mfumo mbovu wa ukusanyaji kodi. Mfumo ambao unazingatia zaidi kukusanya chochote kinachowezekana pasipo kujali taratibu za kiuchumi. Unakuta mtu anatozwa kodi kabla kajauza mali yake wala kutazama ugharama wa mali hiyo kwa walaji. wapo watu wanaofanya biashara ya mabillioni hulipa kodi chini ama sawa na mfanyakazi. Kodi za kukadiliwa ni moja ya sababu kubwa zinazodhoofisha wajasiliamali na kuwatajirisha wachache hasa wale wenye kuendesha uchumi wa kujikimu. Bei zinapangwa kulingana na mlanguzi anavyojisikia na nguvu ya monopoly inawezeshwa kutokana na wahusika wenyewe kuwa ndio viongozi wa serikali na wenye mamlaka ya vibali vya uagizaji mali.

Wakuu zangu nisiwachoshe, Ile mada yangu ya HII NI NCHI ya WAJINGA inabeba mzigo mkubwa wa matatizo haya tulokuwa nayo. Mfumo wa Utawala uliopo ni mbovu sana kiuchumi. Matatizo ya Wafanyakazi sii matatizo ya Kikwete, wala hayatokani na kivuri cha Kikwete isipokuwa hata yeye mwenyewe kamezwa na mfumo hasi wa kiuchumi na utawala. Hakuna mtu wala kiongozi yeyote anayeweza kuleta mabadiliko nchini pasipo kuondosha kwanza mfumo mbaya wa kiutawala. Mfumo ambao unayatazama mahitaji yetu kama ni SHIDA iliyoletwa na Mungu, hivyo hakuna sababu ya ubunifu wowote isipokuwa kuishi kama tulivyopangiwa. Na hakika ukiniuliza mimi leo hii nitakwambia kwamba hizo Tsh 315,000 zinaonekana nyingi kwa sababu Tsh yetu inathaminishwa kinyume cha hali halisi..Kama ingethamanishwa Tsh 2600 sawa na dollar 1 (moja) basi tusingeitazama hiyo mishahara kwa kina hiki cha kushtua. Hizo Tsh laki 315 zingekuwa chini ya Usd 120 kwa mwezi na hata hizo bado ni juu ktk thaminisho kwani majority ya wananchinchini wanaishi kwa pato la dollar 1 kwa siku.
Sasa Mkandara kuanzia hapa nakubaliana na wewe. Ukweli ishu si 315,000 au 104000. Na ni kweli kabisa bei ya bidhaa kwa Tz ni kubwa hata kuliko nchi zilizoendelea. Mf vyakula nk. Hata mie silitazami tatizo hili kwa kumnyooshea vidole Kikwete. Ingawa ukweli haya yoote ni matokeo ya stimulus mbalimbali kwenye sekta zinahusika. Mfano; Licha ya kuwa nafasi katika elimu ya juu hazitoshi idadi ya wanafunzi lakini nchi siku zote ilikuwa ikifocus kwenye elimu ya msingi na sekondari na kusahau hatma ya wahitimu hao mbeleni. Binafsi naona mafanikio katika kupunguza haya matatizo ni kuwa na ushirikiano chanya na sekta binafsi. Tanzania sekta binfsi wanaonekana wabadhirifu, wala rushwa, watu wabaya nk. Lakini ukweli unabaki kuwa hali tete tulizokuwa nazo kuanzia kwenye elimu, uzalishaji kwenye kilimo na viwandani unahitaji ushirikishwaji kikamilifu wa sekta binafsi. Tukubali kuwa falsafa ya socialism hatuiwezi. Tuandae wataalam wakueleweka wanaoweza kunegotiate contract kwa maslahi ya nchi na tuzialike sekta binafsi. Mahitaji ya nchi ni makubwa saana na si mshahara peke yake.
 
Kwanza ingekuwa vizuri wakaomba marupu rupu wanayolipwa yaingizwe kwenye mshahara. Nadhani sasa hivi wastani wa wafanyakzi wengi wanapata zaidi ya kile kiwango kinachoombwa. huo ndio ukweli.

Pili wafanyakazi wengi tunaodai nyongeza ya mshahara hatuko kwenye sekta za moja kwa moja za uzalishaji kama kilimo, ufugaji madini na viwanda. Tuko kwenye sekta za kutoa huduma ( Tunatumia kalamu)na tunatumia kodi inayozalishwa na wazalishaji halisi.

Sipingi Nyongeza lakini inabidi tujue ukweli je take home halisi ya mfanyakazi wa serikali halisi ni ipi. am sure every one can be suprised .

Tujiulize Je tucta wako tayari kuspport reform ya kupunguza wafanyakazi ili kuwe na effectiveness na efficinecy si tu kwenye utoaji wa huduma bali ili wale wachache watakaobaki wapate mshahara mnono.

Vile Vile baadhi ya sekta zina wafanyakazi wengi kuliko mahitaji wakati service delivery yao haiendani na idaidi

Kwa hiyo Jibu langu sio kuwa mshahara wanaodai TUCTA hautekelezeki bali haungalii hali halisi.
 
Tatizo nafikiri unatafuta majibu rahisi ya kuwezesha kutoka kisiasa. No siwezi pendekeza kima cha chini ni ngapi kwa sababu hilo suala si lakisasa kuwekana ktk kona.
Swala mhimu ni kutambua makadirio ya fedha zote tutakazopata 2010/2011 na toa huduma zote gawanya kwa idadi ya wafanyakazi hiyo ndo kima ya chini.
Hata ikija elfu hamsini hiyo ndo kima ya chini itakayotakiwa.

Tucta binafsi ningewaelewa wangekuja na sehebu hiyo kamili, kwamba serikali ikabana hapa na pale ina uwezo wa kukusanya pesa kiasi fulani kwa mwaka 2010/2011. Harafu huduma zingine na ujenzi mwingine utakuwa jumla ya pesa ni hizi. zinazobaki ni hizi hapa tukigawanya kwa idadi kima cha chini kinaonekana hiki hapa ambacho ni 315000.

Madai mengine ya mimi siongelei.Lakini kwa halihalisi ya tanzania huo mshahara hautekelezeki.

Alright. Na kima cha juu cha mshahara unapendekeza kiwe kiasi gani? Nitashukuru kupata formula yake.
 
Yawezekana ni kweli ama si kweli
Wale wafanyakazi nina uhakika wanalipwa zaidi ya kiwango ya tucta ya chini wanayo propose.
Sasa wewe tuma pale gari uweke na radio mle ndani. Ndio utajua sio wasana siasa tu
Kwa hili hata wabunge wetu wamepiga kelele sana na serikali inassema haiwezi kuvunja mkataba na hao wawekezajiwezi kwa kuwa watajikuta wakiwalipa pesa nyingi sana. Iko wazi kabisa kwamba pamoja na yote mhusika mkuu katika kuharibu ufanisi bandarini ni serikali yenyewe. Kesi inarudi kule kule.
 
Mkamap unasema kanuni yako ya kutafuta kima cha chini ni:

Swala mhimu ni kutambua makadirio ya fedha zote tutakazopata 2010/2011 na toa huduma zote gawanya kwa idadi ya wafanyakazi hiyo ndo kima ya chini.

MAKADIRIO YA MAPATO YOTE - GHARAMA ZA HUDUMA ZOTE / IDADI YA WAFANYAKAZI = KIMA CHA CHINI!

Kwa maneno mengine, tutakachopata ndicho kitawezekana?
 
Mkamap unasema kanuni yako ya kutafuta kima cha chini ni:

MAKADIRIO YA MAPATO YOTE - GHARAMA ZA HUDUMA ZOTE / IDADI YA WAFANYAKAZI = KIMA CHA CHINI!

Kwa maneno mengine, tutakachopata ndicho kitawezekana?
Mwanakijiji equation yako haipo sawa. Ukisema hiyo ndiyo kima cha chini unamaanisha wafanyakazi wote wanalipwa sawa. Kwenye thread moja niliambatanisha bajeti speech na hapa ninaiweka tena. Ukinzia page ya 14 utaona kuwa serikali ililipa mishahara ya kiasi cha trilion 1.2 kwa miezi 9 kwa hiyo kwa ratio hiyo inamaana mishahara ni zaidi ya 1.6 trilion kwa kwa mujbu wa bajeti ya 2009/10. Lakini pia tukumbuke kuwa serikali imekuwa ikifinya bajeti ya kila kitu kwa sababu mapato hayatoshelezi matumizi. Kwahiyo ukisema Mapato-Matumizi unless uchague matumizi vinginevyo wafanyakazi watakosa mishahara. Kimsingi nchi yetu ni maskini tufocus kwenye macro economics variables.
 
Attachments

  • Bajeti Speech.pdf
    743.3 KB · Views: 28
Serikali yetu ina matumizi makubwa sana yaani ukitoa mishahara....Gharama za IKULU peke yake acha mawaziri ingetosha kulipa wafanyakazi wengi tu kwa miaka kadhaa.
 
inawezekana
katika wafanyakazi 350,000 wa serikali only 50,000 ndio wanapata above 1m.

kwa hiyo wafanyakazi 300,000 waliobakiwa ambao wanapata chini ya 1m wakipewa ongezeko la 200,000 kwa mwezi inakuwa
300,000 x 200,000 x 12 = inakuja 720 000 000 000 or 720bil
kwa hiyo hili ni ongezeko la 720 bil kwa bajeti ya taifa

hizi hela zinaweza kupatika kama serikali itajenga gold refinery yenye capacity kubwa mwanza ambayo ita cost a mere $10m.
badala ya dhahabu kupelekwa south africa kuwa refined mambo yote yatafanyika mwanza na kuzui upotevu wa pesa. this is more than enough
uganda wamejenga refinery ndogo ambayo ina process 60kg a day at cost of $1.5m.

au wakitoa exemption wanazopewa makampuni makubwa basi ni more than enough ( na ichi ni moja kitu TUCTA wanachokipigania na kusema kwa nini maskini wanalipa kodi more than reach people)
 
Ongezeko la mshahara huwa halifanyiki hivyo yaani the same throughout, pia kuna watu wanapanda vyeo pia. Kwa kuwa hatuna data basis etu inaweza kuwa bajeti ya Fedha ya mwaka 2009/10. Inaonyesha wazi kabisa mishahara inagharimu Taifa kiasi gani. Wakati fulani tofauti ya mishahara lazima iwepo ili kuvutia wataalam katika sekta.
 
Mwanakijiji equation yako haipo sawa. Ukisema hiyo ndiyo kima cha chini unamaanisha wafanyakazi wote wanalipwa sawa. Kwenye thread moja niliambatanisha bajeti speech na hapa ninaiweka tena. Ukinzia page ya 14 utaona kuwa serikali ililipa mishahara ya kiasi cha trilion 1.2 kwa miezi 9 kwa hiyo kwa ratio hiyo inamaana mishahara ni zaidi ya 1.6 trilion kwa kwa mujbu wa bajeti ya 2009/10. Lakini pia tukumbuke kuwa serikali imekuwa ikifinya bajeti ya kila kitu kwa sababu mapato hayatoshelezi matumizi. Kwahiyo ukisema Mapato-Matumizi unless uchague matumizi vinginevyo wafanyakazi watakosa mishahara. Kimsingi nchi yetu ni maskini tufocus kwenye macro economics variables.

hiyo siyo equation yangu; ni equation ya Mkamap..

Ni kweli mapato hayatoshelezi matumizi? au Matumizi yamezidi mapato?
 
Ongezeko la mshahara huwa halifanyiki hivyo yaani the same throughout, pia kuna watu wanapanda vyeo pia. Kwa kuwa hatuna data basis etu inaweza kuwa bajeti ya Fedha ya mwaka 2009/10. Inaonyesha wazi kabisa mishahara inagharimu Taifa kiasi gani. Wakati fulani tofauti ya mishahara lazima iwepo ili kuvutia wataalam katika sekta.

hiyo ni estimate ili kuonyesha kuwa inawezekana
mara nyingi mishahara inaongezwa kwa pasenti kutokana na inflation. hapa focus yetu ni kima cha chini.

ni kama vile manesi/wauguzi wakiwa wanataka nyongeza ya mishahara sio lazima ma dr waongezewe
au hata junior dr wakiwa wanataka nyongeza sio lazima seniour dr waongezewe

nimesema ongezeko ilo through out kwa ajili mishahara ya kuanzia 100,000 mpaka 1m iko karibu mno kiasi cha kwamba ongezeko la daraja la chini linafikia daraja lingine na kusababisha pia daraja lingine liongezewe.

serikali ingekuwa wazi na statistics zote tungeweza kujua kujua cost ni kiasi gani
 
hiyo siyo equation yangu; ni equation ya Mkamap..

Ni kweli mapato hayatoshelezi matumizi? au Matumizi yamezidi mapato?

Taifa halizalishi hakuna kinachozalishwa na wa nanchi zaidi ya huruma ya Mungu Dhahabu, samaki,gas.
Kwa hiyo kwa mshahara huo kwa hali ya sasa hautekelezeki.
 
hiyo ni estimate ili kuonyesha kuwa inawezekana
mara nyingi mishahara inaongezwa kwa pasenti kutokana na inflation. hapa focus yetu ni kima cha chini.

ni kama vile manesi/wauguzi wakiwa wanataka nyongeza ya mishahara sio lazima ma dr waongezewe
au hata junior dr wakiwa wanataka nyongeza sio lazima seniour dr waongezewe

nimesema ongezeko ilo through out kwa ajili mishahara ya kuanzia 100,000 mpaka 1m iko karibu mno kiasi cha kwamba ongezeko la daraja la chini linafikia daraja lingine na kusababisha pia daraja lingine liongezewe.

serikali ingekuwa wazi na statistics zote tungeweza kujua kujua cost ni kiasi gani

Asilimia 40% ya bajeti wanakopa. Na ili upate mkopo anayekupa mkopo anakupa masharti namna itakayotumika. Na hata kama ukikusanya hiyo pesa si kwamba yote utaielekezea kwa watumishi ili maisha yawe bora bali utaongeza pia tija ktk nyanja zingine za huduma.
 
Back
Top Bottom