Mkuu ama kweli nawe mbayuwayu...Hakuna ukweli wowote kisayansi kama hotuba ya JK - Karagabaho!Mkandara
Pia cheki mstari wa pili na mwisho kuto mwisho kabisa
Mkuu ama kweli nawe mbayuwayu...Hakuna ukweli wowote kisayansi kama hotuba ya JK - Karagabaho!
Ni mwaka gani kiwango cha kima cha chini kilikuwa kimoja?..
Nipe mfano ambao ulimtazama housegirl, tingo au mlinzi kuwa sawa na mwajiriwa wa serikali au shirika la Umma..
Wananchi na wana jamii wenzagu
Kiu -halisia mshahara wa kima cha chini cha zaidi ya US dola 300 kwa wafanyakazi wa Tanzania hautekelezeki.
Haiwezekani na haiwezekani, mfanyakazi anayedai huo mshahara itambidi adai zaidi ya hapo mara mbili ili atekeleze. Mfano wewe ni mwalimu wa kike una mtoto na umeajiri dada wa kumlea nyumbani itakubidi umlipe dada huyo zaidi ya us dola 300. Na utaishi je? itabidi udai tena zaidi us dola 300 kutoka serikalini ili upate kuishi.
Ugiriki lwo wamefirisika kwa sababu nao wafanya kazi wali dai ongezeko kama hilo. Ugiriki wanahaha kutafuta sehemu ya kukopa, EURO imeanguka sababu ya ugiriki.
Naungana na JK mshahara huo hautekelezeki.
Kunradhi wana JF na TUCTA kama nitawakwaza kwa kuuliza kuwa hivi mbona sijasikia suala la productivity likizungumziwa ? Jee hili siyo suala la msingi kabla ya yote? Jee haiwezekani wazee hawa wakabulliana kuwa a certain percentage of the budget ya serikali iwe ni mishahara hivyo productivity na efficiency vikiongezeka na wastage ikipungua ni endelevu zaidi [kwani kila serikali itakapokusanya zaidi automatically mishahara itapanda. JUST THINKING OUT ALOUD
Abunuasi,
Mkuu Productivity ktk sekta ya serikali huanza na huduma zenyewe kuwa bora hapa hakuna uzalishaji isipokuwa huduma. Kinachogomba hapa ni mishshara duni kwa wafanayakzi waserikalikiasi kwamba kila mfanyakazi wa serikali ana kijiofisi chake pembeni. Ukitaka Passport unazunguka, Ukitaka huduma ya Hospital au elimu ni lazima upitie ktk ofisi zao kupata huduma safi na bora kuliko ile ya serikali.
Na ukitazama undani wa hali hii umetokana na mishahara midogo sana na jambo moja lililonikera zaidi nilipokuwa tanzania ni kwamba hata wale watoto wanaosoma Private schools ni lazima wapate tuition jioni kwa malipo ya ziada. Kuna rafiki yangu ana mwanaye anasoma Internatioonal school akilipa ada ya dollar 14,000 kwa mwaka, lakini watoto wake bado wanaenda tuition jioni kulingana na mapendekezo ya walimu...Hii kweli ni - HAKI?
Kama nilivyosema mdogowangu alifanyiwa operation ya Apendix, ujumla wa gharama ilifikia Tsh 800 tena Muhimbili. Na wala sii yeye pekee kuna gharama kubwa ktk Elimu na Afya kiasi kwamba unashindwa kuelewa fedha zinapelekwa wapi hasa ikiwa pato la serikali linatokana na kodi zetu.
Mimi naamini kabisa maelezo ya Tucta kwamba ipo kila sababu ya kuongeza mishahara ya chini kulingana na maisha yetu laa sivyo Bank kuu ithaminishe Tsh kulingana na mfumko wa bei ili wananchi wapate uhalali wa mishahara wanayopokea..Kweli haiwezekani kuwapa wananchi mshahara mmoja kima cha chini sekta zote. Haiwezekani kwa sababu ya Mazingira yetu..Watanzania ni watu wavivu sana, wavivu kufikiri na wavivu kufanya kazi. Utamaduni wetu umebeba sana na mila za Kikoloni na utumwa ambazo ndio rolemodel ya mafanikio..Ulaya huwezi kukuta mtu akiwa na mtumishi (housegirl) mfungua gate mkata majani, sijui mlinzi na kadhalika kwa kipato cha kati (middle class) lakini Afrika na hasa Tanzania kila familia ina Kijakazi..
Na kama umesoma hapo juu kuna kiongozi wa vyama hivi vya ushirika amediriki hata kudai kwamba mishahara ya housegirl ni mikubwa pasipo kufikiria kwamba utaratibu wote wa kuwa na Kijakazi ni fikra za Kikoloni na Utumwa. Amediriki hata kutaja salio la kijakazi kuwa ni malipo bora zaidi ya mwajiri ambaye halazimiki kuwa na Kijakazi, ila analazimika kuomba haki yake kwa kusema mshahara anaopata ni mdogo hauwezi kukidhi mahitaji yake. Ni akili ya kitumwa kuangalia mwenzako anapata ngapi ili upime uhalali wa malipo yako hali ni mchakato mzima wa maisha, elimu, uzalishaji na true value ya fedha unayopokea ndiyo thamani halisi ya kazi yako.
Hata hivyo mkuu wangu kinachogomba hapa ni uwezekano wa serikali kulipa mshahara huo. Serikali inaweza kuwalipa wafanyakazi kiwango hicho kama serikali yenyewe itakuwa na uwazi ktk jambo hili. Serikali itakuwa tayari kukubali kutazama njia na mbinu ambazo wachumi na wahadhiri wamependekeza. Inawezekana tu ikiwa kuna transfer na makato ya matumizi ktk sekta nyinginezo kwa sababu kama iitokea vita kesho basi utaona serikali ikikusanya fedha na kuwa na uwezo wa ajabu kijeshi kupambana na uvamizi. Ikitokea njaa na ukame tutasubiri misaada ya ILO na Red cross kutusaidia kwa sababu waathirika sii viongozi wa Ikulu..
Well, a Corrupt Government ndiyo chanzo cha wananchi wake kufuata matendo yao..Ndio maana wahenga husema - Practice what U preach! Hao watumishi wote wala rushwa ni matokeo ya uongozi mbaya na ndio maana wenzetu huziondoa madarakani serikali zilizo corrupt.Hao wote ni bakora tu ndo zinawafaa.
Hizo ndo roho za kifisadi tunazoziongea, kwamba watanzania karibu wote ni mafisadi . Ndio wakipata chansi kama ya RA nao hao watafisadi kwa kasi ile ile.
Lowasa ama RA hawakutengeneza richmondi kwa sababu ya mshahara mdogo, bali ni huruka iliyo damuni tu kama walivyo watanzania wengine kwa nafasi zao.
Na ukitazama undani wa hali hii umetokana na mishahara midogo sana na jambo moja lililonikera zaidi nilipokuwa tanzania ni kwamba hata wale watoto wanaosoma Private schools ni lazima wapate tuition jioni kwa malipo ya ziada. Kuna rafiki yangu ana mwanaye anasoma Internatioonal school akilipa ada ya dollar 14,000 kwa mwaka, lakini watoto wake bado wanaenda tuition jioni kulingana na mapendekezo ya walimu...Hii kweli ni - HAKI?
Kama nilivyosema mdogowangu alifanyiwa operation ya Apendix, ujumla wa gharama ilifikia Tsh 800 tena Muhimbili.