Ni ukweli mtupu Mshahara wa kima cha chini TUCTA wanaoutaka hautekelezeki

huwezi kumpangia mtu mmoja mmoja kima cha mshahara specific kwake tu! Marekani kuna minimum wage kwa wafanyakazi wote na muda wa kufanya kazi na overtime n.k na vinaongozwa na sheria.. kutokea hapo unawez akupanga chochote na hakipangwi kwa kuangalia uzalishaji wa mtu mmoja mmoja. Tunaangalia gharama ya maisha n.k. Kwa maoni yako kwa Tanzania mfanyakazi wa kawaida anahitaji kama kiasi gani kwa mwezi kuweza kumudu maisha? Sidhani kama ni swali gumu sana.

Mwanakijiji
mimi nafikiri mnataka kupotosha, nafikiri hakuna mahala binadamu kuna mshahara unaomtoshesheleza. Hawa watu wa europe sijui huko marekani, kama mishahara inawatosha mbona maisha yao ni ya madeni?? kukopa kila kitu. Wanaishi kwa benki.

Imefika mahala hata simu ya mkononi hawawezi toa keshi, simu wanakopa. tusidanganyane hapa ni ukweli wanakopa kwa sababu keshi inapiga chega, hakuna anayependa kukopa kama keshi ipo.
Hakuna kima cha chini ambacho utaweka eti useme hiki kitawatosheleza watu wangu. Kima cha chini kinatakiwa kuwa kile ambacho serikali inaweza kua affford yenyewe kuwalipa na kutoa huduma mhimu. Concrete namba huwezi toa kirahisi kama mnavyotaka kuwa.
 
Housegirls/boys, wafanyakazi wa mahotelini na mashambani nadhani wanacho chama chao pia, chaitwa CHODAWU. Hicho chama pia ni miongoni mwa hivyo vyama 14 vinavyokuja pamoja kuunda shirikisho la vyama vya wafanyakazi yaani TUCTA. Tena kwa ziada hao CHODAWU ndio waliohost shughuli ya Mei Mosi kitaifa mwaka huu wa 2010. Ni active members wa TUCTA.

Hii nimeipenda
Asante sana
 
Mwanakijiji
mimi nafikiri mnataka kupotosha, nafikiri hakuna mahala binadamu kuna mshahara unaomtoshesheleza. Hawa watu wa europe sijui huko marekani, kama mishahara inawatosha mbona maisha yao ni ya madeni?? kukopa kila kitu. Wanaishi kwa benki.

Imefika mahala hata simu ya mkononi hawawezi toa keshi, simu wanakopa. tusidanganyane hapa ni ukweli wanakopa kwa sababu keshi inapiga chega, hakuna anayependa kukopa kama keshi ipo.
Hakuna kima cha chini ambacho utaweka eti useme hiki kitawatosheleza watu wangu. Kima cha chini kinatakiwa kuwa kile ambacho serikali inaweza kua affford yenyewe kuwalipa na kutoa huduma mhimu. Concrete namba huwezi toa kirahisi kama mnavyotaka kuwa.
kwahiyo wewe ukmekaa hapo ofisi ya Chama , kazi yako kujenga hoja kuwa 100,000 inaweza kufanya Mtanzania aishi..
 
Guys...Hata kama serikali haiwezi kulipa kima cha chini kinachotakiwa..they need to bridge the gap kati ya kima cha chini na cha juu..Hilot u linaotosha kupunguza grievancies..Because..wananchi wanaona namna viongozi wa juu wanavyokamua maisha...! Isitoshe,kuna opportunity ya kuongeza mapato ya serikali ili kuweza kumudu kulipa vizuri wafanyakazi wake...! TRA kuna Rushwa nzito inayoikosesha mapato..Viongozi wetu wanafanya decisions kwa maslahi yao..na hivyo kulikosesha Taifa Mapato...! It is time for change..TUCTA wachague viongozi watakaowalinda..
 
uNADHANI HAWAKUWA NA UTHIBITISHO WA VIPI SERIKALI INAWEZA KULIPA MISHAHARA WATUMISHI WAKE.
Upo mchanganuo, Kikwete na Kapuya wake, hawana nia njema na Watumishi wa nnchi hii, wamejaa urafi,tamaa na kila madudu.
wanadhani wao tu ndio wanahaki ya kula keki ya taifa bila Tija.

wafanyakzi ndo hawana nia njema. wangekuwa na nia njema wangegoma Kikwete angelijiuzulu hata kabla ya uchaguzi. Maana kila sehemu pangefungwa, mahospitali, maji,umeme,shule nk.
 
Mkapa aliweza kudhibiti "inflation" ama kwa kiswahili mfumuko wa bei huyo jamaa hajafanya lolote zaidi ya kucheka cheka tu na kuuza sura yake. Inaudhi sana. "Wao wameshiba sisi tuna njaa, mwenye njaa lazima atakuwa na hasira (THEM BELLY FULL)"....BOB MARLEY. Aliyeshiba hamjui mwenye njaa tuachane na propaganda za kumpamba mwenye kaya wakati tukijua mifukoni mwetu kuna nini. Tuwe wakweli angalau tuwe huru .
 
kwahiyo wewe ukmekaa hapo ofisi ya Chama , kazi yako kujenga hoja kuwa 100,000 inaweza kufanya Mtanzania aishi..

Teh teh teh
Namba sio tija, hilo tena tunashindwa kuliona namba inaweza kuwa kubwa ikashindwa na namba ndogo. Cha msingi hapa ni kuchapa kazi kuimarisha uchumi
 
Sidhani kama ni wavivu bali kwa vile mishahara haikidhi mahitaji, wanaingia maofisini, mawazo kibao wanawaza magenge yao yanaendeleaje ili mkono uende kinywani! Wakilipwa vizuri nina hakika watakuwa productive!

Hata hao wakulima, wanalima mazao yao yanaozea shambani, barabara mbovu, garama za kuyasafirisha ziko juu, hakuna wanunuzi, wakitokea walanguzi wanawalalia bei, wakitaka peleka yauza mahali ambapo watapa bei nzuri serikali inawakatazana kuwakamata kam vile wameiba mazao hayo ili hali ni ya kwao, unategemea ataendelea kuwa na moyo wa kulima tena?

Serikali iwalipe vizuri, watu watulize akili afanye kazi, wakulima nao wawekewe miundo mbinu na wasiaidiwe kupata masoko ya mazao yao, Hili linawezeakana kinacho takiwa ni serikali makini bac, si ya wachumia matumbo yao!
 
Teh teh teh
Namba sio tija, hilo tena tunashindwa kuliona namba inaweza kuwa kubwa ikashindwa na namba ndogo. Cha msingi hapa ni kuchapa kazi kuimarisha uchumi

nawewe nawe, unadhani mtumishi atatoa wapi tija kwa kamshahara hako, mazingira ya kazi duni, kodi juu, dharau za Rais wao, matusi ya Rais dhidi yao, nakuhakikishia, watumishi wa Umma wako mbiombio, kukimbiza shilingi, watoe wapi tija, wakae kazini wakati rais anasema anaweza kuwafukuza kazi woote na akaajili wengine.
Wamezalisha sana, kiasi ya kuiwezesha BOT kuwa na pesa nyingi ambazi CCM wakaiba pale BOT, WAMEZALISHA SANA . SASA NI VITA VYA ULAJI
 
Na kubaliana na wewe
Sasa naomba nikuulize maswali? Bandarini na uhakika fulani wanapata pesa juu ya hiyo kiwango ya tucta mbona pale kazi haiendi? wale jamaa wanadiriki hata wakati mwingine kuiba radio tu ndani ya gari ambalo unakuwa umelisafisha.

Makontena pale yamejaa longolongo nyingiiiiiiiii .?hakuna lolote
 
unajua upuuzi wa Watu wetu wengi hapa Tanzania ndio unaoinufaishaga CCM na Rais Kikwete.
Kikwete alikua anaparamia hoja hovyohovyo bila mtiririko wa kisomi na wala uchambuzi makini.
TUCTA ni shirikisho huru la vyama vya wafanyakazi hapa Tanzania, linaunganisha vyama kama CHAMA CHA WALIMU , RAAWU,TUGHE, TALGWU ,TUICO nk.
kwahiyo katika mtiririko wa vyama hivyo hakuna vyama vya mahausigeli na mashamba boy, TUCTA wanasimamia hoja ya kutetea wafanyakazi hasa katika sekta rasmi za UMMA na ZISIZO ZA UMMA.
Alikua anaunganisha mishahara ya wauza duka katika swala hili ili apate compromise ya UMMA....., alipotoka ,alijipotosha ama alipotoshwa.
TUCTA wanamadai mengi sana, kama Rais wa Jamuhuri alipaswa kujikita katika hoja moja baada ya nyingine, badala ya kujikita katika hoja moja, nakuimba taarabu na kuchombeza na vimipasho.
mshahara wa 315,000 Unawezekana katika sekta rasmi zooote hapa nyumbani, waache kuchezea hela katika mambo yasiyo na maana, waache kulipana posho za safari za kwenda kubembea Jamaica, apunguze makundi ya wapambe akiwa safarini, wadhibiti kodi, wajiepushe na misamaha hewa....vilevile upandaji wa mishahara usizingatie hoja ya asilimia sawa, maana ailimia kumi ya mshahara wa muhudumu ni Tsh 10000 wakati kwa mishahara ya mawaziri, makatibu wakuu ni TSh 300,000.
Tanzania Amka achana na mawazo kuwa Rais adanganyi , Rais huwa anadanganya kama mtu mwingine yoyote.

...Mkuu, Aswante! Hapo umemaliza maneno....!
 
Na kubaliana na wewe
Sasa naomba nikuulize maswali? Bandarini na uhakika fulani wanapata pesa juu ya hiyo kiwango ya tucta mbona pale kazi haiendi? wale jamaa wanadiriki hata wakati mwingine kuiba radio tu ndani ya gari ambalo unakuwa umelisafisha.

Makontena pale yamejaa longolongo nyingiiiiiiiii .?hakuna lolote
mbona unauliza swali ambalo nilikupa jibu lake jana?
 
Wananchi na wana jamii wenzagu

Kiu -halisia mshahara wa kima cha chini cha zaidi ya US dola 300 kwa wafanyakazi wa Tanzania hautekelezeki.
Haiwezekani na haiwezekani, mfanyakazi anayedai huo mshahara itambidi adai zaidi ya hapo mara mbili ili atekeleze. Mfano wewe ni mwalimu wa kike una mtoto na umeajiri dada wa kumlea nyumbani itakubidi umlipe dada huyo zaidi ya us dola 300. Na utaishi je? itabidi udai tena zaidi us dola 300 kutoka serikalini ili upate kuishi.

Ugiriki lwo wamefirisika kwa sababu nao wafanya kazi wali dai ongezeko kama hilo. Ugiriki wanahaha kutafuta sehemu ya kukopa, EURO imeanguka sababu ya ugiriki.

Naungana na JK mshahara huo hautekelezeki
.

Mzee wa propaganda!

“Propaganda is neutrally defined as a systematic form of purposeful persuasion that attempts to influence the emotions, attitudes, opinions, and actions of specified target audiences for ideological, political or commercial purposes through the controlled transmission of one-sided messages (which may or may not be factual) via mass and direct media channels. ”
— Richard Alan Nelson, A Chronology and Glossary of Propaganda in the United States

Wikipedia
 
Mkuu katika hali ya kawaida, mshahara wa shilingi laki 3 au hata 3.5 unawzekana. Kama isingekuwa wizi, ufisadi inawezekana kabisa. Sababu ni kuwa Civil service sio kubwa sana kwa seriklai kushindwa kuafford kuwalipa hivyo, na kama ukiangalia marupurupu yanayotolewa ovyo(pamoja na kusema walifondoa) bado unaona kuna wastage kubwa sana ya hela, kila kukicha ukiangalia unaweza kuona jinsi mgari ambayo hayahitajiki yanavyonunuliwa na matumizi mengine yasiyo ya lazima yanavyofanywa, for usre hata zaidi ya laki nne inawezekana.

HOja hapa nadhani inatakiwa kuwa malipo ya mshahara yaendane na efficiency na sio mahitaji ya maisha. KUna wwatu ni less efficent na pia wezi wanalipwa zaidi kuliko toilers na wale ambao ni efficent. Hii inaweza kuwa hoja ya haki.
 
Mkuu
Na hiyo nyeusi pia ni hoja ya msingi. Pamoja na ufisadi wote mshahara kwa hali iliyopo sasa kwa miono yangu mshahara huo unaotakwa kulipwa haiwezekani, sijui naeleweka?
 
Na kubaliana na wewe
Sasa naomba nikuulize maswali? Bandarini na uhakika fulani wanapata pesa juu ya hiyo kiwango ya tucta mbona pale kazi haiendi? wale jamaa wanadiriki hata wakati mwingine kuiba radio tu ndani ya gari ambalo unakuwa umelisafisha.

Makontena pale yamejaa longolongo nyingiiiiiiiii .?hakuna lolote
KUMBE HUJUI NINANI MWIZI PALE BANDARINI, WEZI WENGI HUSHIRIKIANA NA WALINZI WALE WA MAKAMPUNI NA WALE WA BANDARI,
BANDARINI UFANISI HAUONEKANI NI MATOKEO YA SERIKALI YA KIKWETE KUINGIZA SIASA KATIKA UBINAFSISHAJI WA VITENGO FULANI FULANI PALE BANDARINI, pale longroom wadau wanachapa kazi ile mbali, wanachapa mzigo mpaka basi.
Angalia mkapa alivyowaongeza mishahara pale TRA, then kumbuka tija ilivyoongezeka katika ukusanyaji ...ukusanyaji ambao mpaka leo kikwete anashindwa kupiga hatua moja mbele, huyu Mkwere hana lolote.
 
Teh teh teh
Namba sio tija, hilo tena tunashindwa kuliona namba inaweza kuwa kubwa ikashindwa na namba ndogo. Cha msingi hapa ni kuchapa kazi kuimarisha uchumi

...Mkuu MkamaP, heshima yako. hawa wawakilishi wetu wanaopokea milioni 9 kwa mwezi na bado wanajenga hoja ya kutaka kuongezewa nyingine wanachapa ama wamechapa kazi gani ya kuimarisha uchumi kuhalalisha malipo wanayojilipa? mawaziri je?
 
wafanyakzi ndo hawana nia njema. wangekuwa na nia njema wangegoma Kikwete angelijiuzulu hata kabla ya uchaguzi. Maana kila sehemu pangefungwa, mahospitali, maji,umeme,shule nk.

nnchi hii imebadirika sana, kumbuka miaka ya 1980 huko ungesikia kiongozi waTUCTA Kalala ndani, kuna kauoga kidogo, najuhudi zetu ni kuwafundisha watu wajua kuasi watawala Fisadi kama hawa tulionao si dhambi, lazima watu wajue kugoma ni haki yao ndani ya sheria, wasiogope.
Kuna kausaliti kasababishwacho na Umasikini, na high rate of unemployment, ila watu wetu wanakoelekea watakuja kuasi dhidi ya Mafisadi hawa.
 
Back
Top Bottom