Ni shemeji yangu kabisa..

sarikoki

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
1,194
721
Yaani huyu jamaa kamuoa dada yangu kabisa.. Jana jioni kanipigia simu, bwana shem njoo hapa- (hotel moja maarufu city center) tupunguze foleni. Nilikua na kiu kwelikweli dakika sifuri nikawa nshafika.
Basi mzee nikaanza kukata maji... ya kwanza--ya tatu imefunguliwa, mara anangia demu mmoja mkali balaa... naona anakuja tulipo kaa huku anatabasamu... mimi majicho yamenitoka huku mapigo ya moyo yanaenda kasi.

Hello Darling... shem anasimama anambusu lipsini. Na kumkaribisha aketi.... umependeza mpenzi, Dada akajibu hasante Darl. Wakaangaliana kwa sekunde kadhaa huku wakitabasamiana... alafu kama vile shem anashtuka , bytheway huyu ndio yule shemeji yangu nilikua nakuambiaga.... enheee ndio huyu? nice to meet you. Huku tabasamu likizidishwa.Halafu shem akaniambia, kiongozi usimwambie dada bwana.Wote tukacheka kwa sauti..

Wakuu yote hayo yametokea mbele yangu...nilihisi kama nilipigwa na radi vile, sikuamini kinachotokea. Nikaipiga ile ya tatu fasta nikafake napokea simu , alafu nikaaga.
 
Itabidi uhave a long chat with ur shemeji; ila kwa mtazamo wangu huyo shemeji yako hana adabu wala heshima.
 
Yaani huyu jamaa kamuoa dada yangu kabisa.. Jana jioni kanipigia simu, bwana shem njoo hapa- (hotel moja maarufu city center) tupunguze foleni. Nilikua na kiu kwelikweli dakika sifuri nikawa nshafika.
Basi mzee nikaanza kukata maji... ya kwanza--ya tatu imefunguliwa, mara anangia demu mmoja mkali balaa... naona anakuja tulipo kaa huku anatabasamu... mimi majicho yamenitoka huku mapigo ya moyo yanaenda kasi.

Hello Darling... shem anasimama anambusu lipsini. Na kumkaribisha aketi.... umependeza mpenzi, Dada akajibu hasante Darl. Wakaangaliana kwa sekunde kadhaa huku wakitabasamiana... alafu kama vile shem anashtuka , bytheway huyu ndio yule shemeji yangu nilikua nakuambiaga.... enheee ndio huyu? nice to meet you. Huku tabasamu likizidishwa.Halafu shem akaniambia, kiongozi usimwambie dada bwana.Wote tukacheka kwa sauti..

Wakuu yote hayo yametokea mbele yangu...nilihisi kama nilipigwa na radi vile, sikuamini kinachotokea. Nikaipiga ile ya tatu fasta nikafake napokea simu , alafu nikaaga.

Kilichokuchekesha?
OTIS
 
Itakuwaje dada yako akija pata taarifa toka chanzo chochote kile kuwa wewe nduguye wa damu ni mojawapo kati ya wanaomkuadia mumewe kwa wanawake wengine?

Leo ukipata malalamiko toka kwa dada yako kuwa shemeji haachi fedha ya matumuzi nyumbani na badala yake anatumbua na vimada wake utajisikiaje wakati na wewe beer ulikunywa?

Tahadhari fanya maamuzi chukua hatua stahiki
 
Huyo shemeji yako hana heshima anaona wewe kwa sababu ya pombe basi huwezi sema kumwambia dada ako.

Na labda anaona unamtegemea kwenye mengine, hii ni kama yapo.

Ni dharau sana amekufanyia kukuonyesha hayo hadi kumbusu yaani ni anakuonyesha dada yako hafai. Kama ilivyosemwa hapo juu ongea nae, ila pia mfikirie dada yako maana anaweza kufa kabla ya siku zake na magonjwa haya ni hata bp labda shemeji yako anamtesa kiaina na wewe hujui.

Anaza kuongea kwa ukaribu na dada yako kianina na kwa heshima uone kama utaona hana raha ndoani mwake, imagine pesa za kulea familia atakuwa anatwanga kwa huyo binti, magonjwa pia.

Duh amenitia hasira ingekuwa mimi lazima nimwambie tuheshimiane, ila waambie wazazi or ndugu wengine mujue cha kufanya juu ya hili, ikiwezekana mumtonye sister mtashangaa kukuta nae anahisia au anajua. Msaidieni.
 
hii kali mazee, yaani amesha konkludi kuwa hamna cha kumfanya..hiyo mbaya mkuu
 
Amekuvujia heshima sana. tena usikae nae tena manake ni kama hakujali wewe uliyempa mke.
 
Huyo haitaki tena ndoa na Dada yako, ameamua kukuonyesha waziwazi. Inawezekana ana pesa na mnamtegemea sana ndio maana kadiriki kukufanyia dharau kubwa kiasi hicho. Pia inawezekana anajua madhambi yako mengi unayofanya kwa hiyo anaona hilo analolifanya ni dogo kulinganisha na yakwako.
 
Hapo ndio ninapoona hekima ya kuoa mke zaidi ya mmoja ila sheria inapobana unakuwa huna budi kufanya kama ya shemeji yako.
 
Sina vile naeza sema..
U nid smtyms 2 thnk abt it..
Na kama mamako yuko na anafikika na anaweza kuyachukulia mambo ni vema umshirikishe na yeye au mshenga wake kwa dadako...

Kiukweli hapo Mapenzi kwa dadako hakuna tena wangu ,, hata ingekuwa bia 10 hasingeeza fanya utuntufunyusu kama huo..!!
 
coffee_computer_scientist-trns.png
 
Bila shaka mnamtegemea sana huyo bwana shemeji si ajabu familia yenu hela ya kula inatoka kwa shemeji,sio rahisi shemeji kukuonyesha dharau kiasi hicho bila sababu,kweli kua uyaone duh! Pole sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom