Mke arejesha heshima kwa Kasi ya 5G

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,468
8,289
Ni kisa Cha ukweli kilicho mkuta jamaa yangu.

Yalikua ni malalamiko tu kila siku akisema mkewe hana heshima yaani hamuheshimu kabisa.

Pamoja na kuto kuwa na heshima alikua na kauli chafu Sana yule mwanamke kumuambia jamaa kuwa alimuonea huruma tu akamuoa ni neno la kawaida Sana na hili neno jamaa alikua analalamika Sana na kusema ndio linalo muuma ila hajui afanye Nini.

Basi Mimi Kama mshauri wa karibu wa jamaa sikuwahi kumshauri kitu zaidi tu ni kumpa nafasi jamaa amwage sumu zote na kumuambia ndoa ndivyo zilivyo inahitaji uvumilivu huku moyoni nikisema sijui hata kwa Nini umekua rafiki yangu kwa uzaifu huu.

Basi siku na masiku yakapita Mambo yakiwa ni hayo hayo.

Kiufupi huyu jamaa alikua ni wale wanaume wa baby baby nyingii Sana akiwa na huyo mwanamke wake wanae Hadi hapo wanakatoto kamoja ,kifu ni Kama wale wakina junior Hadi hapo mtakua mmepata picha ya hiyo familia.

Basi siku zinavyo zidi kwenda mwanamke matusi ,kejeli na dharau ndio vimepamba Moto siku nikaalikwa diner kwao kwa picha tu nilio iona yaani jamaa anajitahidi kujichekesha lkn kwa upande wa mkewe hamna kitu zaidi ya kusubiri tu mgeni apanguse bambataa zake asepe

Basi bana nami mgeni nikaona isiwe tabu ngoja nisepe kesho yake nilipo kutana na jamaa akasema nilivyo ondoka tu mwanamke alikiwasha hatari ..! Eti ndio naleta marafiki usiku ili iwaje ....? Nilicheka Sana huku jamaa akinisisitiza kuwa hayo Mambo sio ya kucheka .

Nikamwambia tu mwanangu hiyo ndio Mara ya kwanza na mwisho kuja Tena kwako , jamaa akanisihi nisifanye hivyo Mimi ndio rafiki yake nahitajika kumshauri na ili aweze kuitweka ndoa yake sawa itengamae . Nikamuelewa pale Basi story mbili tatu tukawa tumetawanyika.

Nikaanza kumkochi mwamba huyu jamaa alikua ni mtu wa kililia Sana mapenzi nikamwambia Kama upo tayari hiyo tabia ife onesha kuwa unaweza ishi bila uwepo wa mbususu yake.

Nikamwambia ukitaka kufanya kitu ndani ya nyumba fanya bila kushauriana nae haijalishi atanuna au atafurahi. Jamaa akanza kwa kutoa tv inch 48 na kuweka inch 32 bila taarifa kwa mkewe mkewe akajiongelesha na kuanza kusema jamaa amehonga Malaya zake jamaa hakuomba msamaha Kama ilivyo zoeleka na kujikausha tu asubuhi akanipigia simu nikampa pongezi Kama kweli amefanya hivyo.zikapita siku akarudisha kimya kimya vilevile

Basi siku mwanamke akakiwasha Tena na kumwambia jamaa unazani upo pekeyako Kama umenichoka sema wanaume wengi wananitaka huku akizunguka kumuonesha mwili wake ofcose mwanamke ni mzuri Nahisi uzuri wake ndio unao mpa ujeuri , nikamuuliza jamaa kamjibu Nini akasema hajajibu nikamwambia umefanya vizuri ila unatakiwa umjibu kwa vitendo upo tayari ...? Akajibu nakusikiliza kocha wangu

Basi nikamuuliza hivi birthday ya mwanao tarehe ngapi nikajibiwa mwezi nikasema yes hapo hapo ndio siku ya kujenga heshima kwa mkeo Cha kufanya andaa fungu la kutosha na umshirikishe mkeo kuwa unataka umfanyie mtoto birthday moja mashinee hadi watu washangaee lkn ndio itakua siku ya kumfunza mkeo adabu ....akacheka na kuniuliza Sasa birthday itamfundishaje mtu adabu..? Nikamjibu msikioize kocha anasema Nini

Basi mwezi wa kwanza ukapita wa pili ukapita wa tatu Sasa tarehe kumi ndio siku ya tukio Basi Kuna Dada mmja hivi friend of mine yaani huyu Dada ni wale madada wa mjini Basi Nika mpanga na kumueela ishu nzima na kumuambia anitafutie midada mizuri ilio jaa vya kutosha iwe Kama 10 au na zaidi na uwapange kabisa kuwa mnataka kwenda kwenye birthday ya mtoto wa rafiki yako hata wakitaka usafiri upo wasijari na wanaenda Kama marafiki wa baba mtoto Basi bana ikawa hivyo.

Siku ya tukio vikandaliwa vitu vizuri na watu wengine walio alikwa pia wakaja siku hiyo shemeji alikua mchangamfu utafikiri sio yeye nikapewa na u mc ...Basi ile timu ya Dada ikiwa njiani huku nikiwaelekeza sehem ya tukio hao wakafika wadada wapatao 13 wenye miili utafikiri wamejiumba wao huku wametupia hatari na Mimi Kama mc nikiwakaribisha na kuwapa pole na Safari huku nikiibia ibia kumcheki shemeji anavyo angalia na kukitana na sura ilio na maswali mengi yasio na majibu Basi ilipo fika zawadi nikawasimamisha wazazi na kuwatambukisha marafiki wa jamaa yangu wale wadada na kusisitiza kuwa jmn Hawa ni marafiki tu msiogope ile kiutanitani lkn ndio meseji zinaenda hivyo watu wakiwa wanacheka cheka nikaongezea Tena hivi jamaa yangu uliwezaje kuoa ukiwa na marafiki wazuri hivi ....hautamani kuwa bachelor Tena ....? Jamaa akatabasamu Basi nika changanya maneno pale zawadi zikatolewa sherehe ikaisha tukawasindikiza marafiki waalikwa Hadi kwenye gari nikarudi ndani na kuagana na shemu na kupeana pongezi na kusepa zangu.

Huku nikiwa ninahamu ya kusikia mrejesho wa kile tulicho kifanya.

Ikapita Kama wiki tatu hivi jamaa anasema shemeji kapoa Sana ni Kama amefiwa hivi na ka usikivu kapo , Hana mabishano Kama awali Yale maneno ya kuambiwa ameonewa huruma hayapo Tena , na Yale majigambo ya kujiona mzuri hayapo yaani kiufupi shemu kapoa.

Nikamwambia tu Mimi Kama kocha wako nakuambia hivi hapo mkeo kwa Sasa anakuona Kama bado hajakujua vizuri yaani ni Kama umemtomgoza juzi hivyo Basi ni jukumu lako kumshep upya utakavyo . Kama ulimdekeza ukayaona Yale Basi usimdekeze tena uwe mwanaume mwenye sauti na komand ndani ya nyumba yako , Mambo ya baby baby yafe , uwe usie tabirika ndani ya nyumba siku nyingine Rudi nyumbani saa 12 jioni ,au 2 usiku ,au usiku mkubwa Sana bila sababu ya msingi ukiulizwa jibu liwe nilikua kutafuta hela and no more explanation bila kusahau kuwatoa out Mara moja moja .

Nb
Siku mshauri kuachana kwa sababu ya mtoto wao ....sipendi kuona watoto wanateseka ndio maana tukaingia ngharama ya kuealeta watu ili kufanya ndoa itulie na imetulia
 
Basi ile timu ya Dada ikiwa njiani huku nikiwaelekeza sehem ya tukio hao wakafika wadada wapatao 13 wenye miili utafikiri wamejiumba wao huku
Da unahatari sana.
wakiwa wanacheka cheka nikaongezea Tena hivi jamaa yangu uliwezaje kuoa ukiwa na marafiki wazuri hivi ....hautamani kuwa bachelor Tena ....?
 
Ni kisa Cha ukweli kilicho mkuta jamaa yangu.

Yalikua ni malalamiko tu kila siku akisema mkewe hana heshima yaani hamuheshimu kabisa.

Pamoja na kuto kuwa na heshima alikua na kauli chafu Sana yule mwanamke kumuambia jamaa kuwa alimuonea huruma tu akamuoa ni neno la kawaida Sana na hili neno jamaa alikua analalamika Sana na kusema ndio linalo muuma ila hajui afanye Nini.
Nimekupenda bureee👋👋👋
 
Ko
Ni kisa Cha ukweli kilicho mkuta jamaa yangu.

Yalikua ni malalamiko tu kila siku akisema mkewe hana heshima yaani hamuheshimu kabisa.

Pamoja na kuto kuwa na heshima alikua na kauli chafu Sana yule mwanamke kumuambia jamaa kuwa alimuonea
Kocha teh teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom