Ni sahihi wabunge knunuliwa mashangingi na si landcruzer hard board kama lengo ni kupunguza gharama?

Dr-of-three-Phd

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
202
30
Ni sahihi wabunge knunuliwa mashangingi na si landcruzer hard board kama lengo ni kupunguza gharama?
 
Si sahihi hata kidogo wangepewa defender au prado zile za toleo la kwanza.
 
Si sahihi hata kidogo wangepewa defender au prado zile za toleo la kwanza.

kaka, bei ya defender ni m120. Kwa maoni yangu ni kwamba, wote wasikopeshwe wala kununuliwa. System ya zamani irudi. Magari yanunuliwe na serikali na yawe ya serikali. Mbunge akistaafu liwe la atakayemrithi. Kama ni kuwakopesha, wakopeshe hata walimu na waratibu elimu japo pikipiki. Kuna shule umasaini ni km 28 toka nyumba ya mungu na ni polini. Halmashauri wamewapa pikipiki japo ni mbovu na sijui kama ipo tena. Shule inahudumia boma kama 4 tu. Hakuna maji wala nini. Kuna walimu wanatembea kwa miguu zaidi ya masaa 7 toka shuleni hadi kijiji fulani ili wapande gari kufuata mshahara na mahitaji yao. Kuna waratibu elimu wanatembelea shule kwa umbali mrefu wa zaidi ya km 20 na wakati mwingine hawaendi na hivyo kufanya kazi yao kuwa ngumu na maendeleo ya elimu kudolola. Kwa nini wasipewe usafiri kama wabunge? Na tena siyo pikipiki. Wapewe magari yenye consumption ndogo wafanye kazi yao. Serikali yenyewe ipo busy kufungua mashule kisiasa bila kuangalia miundombinu na hivyo kuwatesa walimu. Wabunge wawe treated kama walimu au walimu na wafanyakazi wengine wa serikali wawe treated kama wabunge.
 
kwa mtizamo wangu sio sahihi. kitendo cha wabunge kununuliwa mashangingi na kilipwa hela kubwa wanaonyesha dhahiri ni jinsi gani walivyo after money. hata wale wapinzani tunaowaamini na wenyewe wapo kimaslai yao zaid coz kama waliweza kutoka nje kutokusikiliza hotuba ya rais kwa nn wasingeshinikiza kupunguzwa kwa fedha anazolipwa mbunge(allowance) na wakikataliwa watoke nje ili angalau watanzania tujue wamejitahid ila imeshindikana kama walivyofanya kwa rais
 
Back
Top Bottom