Ni Mkoa gani utazidi Tanga Tanzania!

Nasikia tabora zipo zinazotembelea 2tyres.

Mkuu Tabora ni miongoni mwa Mikoa ambayo nasikia Magari yake uwezi kuyaacha ukitia mkuu kwenye pedal ila sijawai kuyaendesha!

Story za utoto walikuwa wanatutisha juu ya magari ya huku kuwa yanashikilia dereva kiushirikina sijui kama ni kweli au Dereva mwenye analewa akiwa ndani ya gari kwa raha zake then wanasema kakamatwa ndani ya gari kiushirikina!
 
Hahahaha....

Mkuu heshima uliyopewa hapo ni kupasua tope siyo?......

Karibu Pemba, kuna magari yanapita kwenye matope tu....Kwenye lami linapita unapolimiliki kihalali........ siyo kulikodisha,

Yani ukikodi halipiti Lami? Duh basi hayo yanafaa kuja kufanya kazi huku Bara ambako bado hawajui magari yanavyopasua tope.
 
Mbu haya magari umewai kuyaendesha au unasimuliwa tu! maana umenitia hamu Mkuu, kwakweli sijawai kuwapa kuendesha gari kama hilo itabidi nikutafute Mkuu

...Ohooo, hujawahi sikia "msimulia mvua imemnyea?" ...Am joking bana. Mimi ni mlokole,
nimesimuliwa tu visa vya alfu lela u lela!

BTW, jaribu pia landrover short chassis milima ya uluguru, au kwa malori makubwa na trailer zake toka usukumani na hata kwenye viunga vya mbeya bana. Muungano na Udumu.
 
...Ohooo, hujawahi sikia "msimulia mvua imemnyea?" ...Am joking bana. Mimi ni mlokole,
nimesimuliwa tu visa vya alfu lela u lela!

BTW, jaribu pia landrover short chassis milima ya uluguru, au kwa malori makubwa na trailer zake toka usukumani na hata kwenye viunga vya mbeya bana. Muungano na Udumu.

Udumu milele maana Mola kaweka kila aina ya magari katika pande zote za Muungano, Short chasiss naziogopa unaweza kupinduka haraka kwenye kona.
 
Wiki hii nili vinjali Tanga Baada ya Mizunguko ya muda mrefu kutafuta faranga pande zote za Dunia!

Nikiwa Ocean Breeze pale Tower Street, Nilikuwa na hamu kubwa ya kuendesha black mettalic car maana ni siku nyingi sijapata kuendesha black car! Nilifanya makeke na kupata gari jeusi kama nilivyotaka, halina miaka mingi bado jipyaa! ila limetumika kiasi chake.

Nikiwa na furaha na raha tere, baada ya kuingia ndani ya gari nikafunga mkanda wakati bado shangaa dashboard ili kujipa muda kulielewa gari na jinsi ya switch-on, nilishangaa gari lenye linaingiza four-wheel na kuanza kuondoka huku bado nimedua sija-synchlonise mwendo safari ikakolezwa kupasua tope! Nilichanganyikiwa kwa furaha na raha juu ya gari hili.

Baadaye nilipouliza inakuwaje gari lina-engage four wheel haraka hivyo tene lenyewe Niliambiwa "Unabahati sana shukuru Mungu hiyo ni heshima nimekupa wewe peke yako si kila mtu anapata hiyo heshima!"

Kitendo hicho kimenifanya ni-rank Tanga kuwa Na.01 Tanzania nzima. Kama kuna mkoa unazidi Tanga nijuzeni Tafadhali sana.
Dah! Kwanza pole kwa kudanganywa ndugu. Hiyo 4 wheel ilishatumiwa na waliokutangulia maana umesema gari imeshatumika. Halafu unai rank Tanga kuwa # 1 kisa 4 wheel? Tanga inajulikana kwa mvua nyingi na njia zake zina tope sana, so mara nyingi 4 wheel ni muhimu huko
 
Arafat ogopa magari ya Dar ....huwa na mabody mazuri ila Engine ziko used sana unaweza kuona hummer ila mileage ni kubwa mno sababu ya kushushwa Engine na overhaul za mara kwa mara!

Rev unataka kusema gari likifanyiwa overhaul halifai tena!

Duh kuna magari mengine imara sana hata baada ya overhaul bado linadunda mzigo kama kawa!
 
Yani ukikodi halipiti Lami? Duh basi hayo yanafaa kuja kufanya kazi huku Bara ambako bado hawajui magari yanavyopasua tope.

Yeah....ukilikodi halitaki ulipitishe kwenye lami, ili atakayeamua kulimiliki akute tairi hazijawa kipara.....We utapitishwa topeni, tairi zinachafuka lakini hazipati kipara.
 
Magari mengine bwana matairi makuubwa ya trecta kwenye bito ya nini?
 
Yeah....ukilikodi halitaki ulipitishe kwenye lami, ili atakayeamua kulimiliki akute tairi hazijawa kipara.....We utapitishwa topeni, tairi zinachafuka lakini hazipati kipara.

Sasa mbona mnunuzi atakuwa anauziwa mbuzi ndani ya gunia!

Ila pananifaa huko nadhani kuna kila sababu ya kutembelea huko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom