Ngeleja Apiga stop Maandamano Nzega ya kupinga uwepo wa Mgodi

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
Akizungumza na NIPASHE jana jioni kuhusu madai ya kufungwa kwa mgodi, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema suala hilo ni la kisheria na anachofanya Dk. Kigwangalla (Mbunge wa Nzega-CCM) ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Ngeleja alisema kama kuna madai ya msingi Dk. Kigwangalla angefika ofisini kwake kuyasasilisha ili apate kauli ya serikali.

Mbunge huyu ni miongoni mwa wabunge wanaotunga sheria za nchi na yeye anazijua, lakini nashangaa anapohamasisha wananchi kuzivunja, alisema Ngeleja.

Hata hivyo, Ngeleja alisema wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa Golden Pride wapo kisheria na hawawezi kuondolewa kwa njia ya maandamano.

Alimtaka mbunge huyu kama ana madai ya msingi kuwasiliana angalau na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ili kujua kama mgodi huo una athari zozote za mazingira kulingana na madai yake.
 
Mechi ya kirafiki haina mvuto wowote.

Kaka mbona unaipa chat kihivyo, Afadhali ingekuwa mechi ya kirafiki(ccm+cuf) tungesema ya kujipima nguvu, lakini hii ni mechi ya timu ya wachezaji wa akiba na kikosi cha kwanza, Aina mvuto
 
Kuvunja kwa makusudi sheria inayoendeleza ufujaji wa rasilimali za taifa, kunamkweza mhusika kwenye kilele cha utiifu wa utawala wa sheria.
 
Kigwangala endelea na uzi huo huo. Wewe ndiye unayejua madhara ya mgodi huo na siyo Ngeleja. Mechi haichagui wachezaji.
 
inafurahisha sana, kigwangala go...go.............go andamaneno tu mpaka kielewe kuwa ndani ya ccm wanyonyaji ni akina nani na wakweli ni akina nani!!!!!!!!!!!!!! hali hii itawachanganua wenyewe na wananchi watajua ukweli wake.
 
Kaka mbona unaipa chat kihivyo, Afadhali ingekuwa mechi ya kirafiki(ccm+cuf) tungesema ya kujipima nguvu, lakini hii ni mechi ya timu ya wachezaji wa akiba na kikosi cha kwanza, Aina mvuto
Sure, timu moja iko mazoezini walichofanya ni kugawana jezi wengine wako vifua wazi.
 
Akizungumza na NIPASHE jana jioni kuhusu madai ya kufungwa kwa mgodi, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema suala hilo ni la kisheria na anachofanya Dk. Kigwangalla(Mbunge wa Nzega-CCM) ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Ngeleja alisema kama kuna madai ya msingi Dk. Kigwangalla angefika ofisini kwake kuyasasilisha ili apate kauli ya serikali.
"Mbunge huyu ni miongoni mwa wabunge wanaotunga sheria za nchi na yeye anazijua, lakini nashangaa anapohamasisha wananchi kuzivunja," alisema Ngeleja.
Hata hivyo, Ngeleja alisema wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa Golden Pride wapo kisheria na hawawezi kuondolewa kwa njia ya maandamano. Alimtaka mbunge huyu kama ana madai ya msingi kuwasiliana angalau na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ili kujua kama mgodi huo una athari zozote za mazingira kulingana na madai yake.

Sheria zipi wewe fisadi. Kuna sheria yeyote unafahamu ya kutetea wananchi na raslimali zake? Hakuna sheria yeyote ile kama ipo mbona hizo taratibu na sheria zingezuia kuwepo kwa hiyo kampuni Nzega? Kama kungekuwa na sheria Tanzania Kikwete asingekuwa Ikulu na Mbunge usingekuwa Mbunge hapo Nzega.

Sababu kama hizi ndizo zinatufanya wananchi tupiganie Katiba kwa manufaa yetu sio ccm. Mtaona kama ccm mtakuwepo mweiz ujao Ikulu[
 
Hivi ngeleja ana uwezo kisheria kuzuia maandamano?

Aache ufisadi wake hapa, washaona hata kama ni mechi ya mazoezi lakini ina athari kwani watu watahoji nani alisaini mkataba wa mgodi huu, na kwa kuwa aliesaini ni bosi wake JK (alipokuwa waziri wa madini - kumbuka list of shame) italeta picha mbaya. Kigwa endelea na mipango yako mpuuze huyu mpuuzi Ngeleja.
 
Kaka mbona unaipa chat kihivyo, Afadhali ingekuwa mechi ya kirafiki(ccm+cuf) tungesema ya kujipima nguvu, lakini hii ni mechi ya timu ya wachezaji wa akiba na kikosi cha kwanza, Aina mvuto

acha kuipa mvuto hii walao si mechi ya first team vs reserve haya ni mazoezi tu ya kikosi B ( yaani wenyewe kwa wenyewe :)
 
Ha ha ha Kigwangala hiyo ndiyo CCM lazima wakukabe koo,uwe ndani ya hicho chama utetee wananchi subiri ni imani yangu wanakuhesabia wakuchakachue. Hicho ni chama cha maslah binafsi

Sina shaka na wewe kwani najua ulivyoongoza mgomo wa madaktari Muhimbili kudai maslahi yao ila wasiwasi wangu ndani ya chama hicho cha ghilba ambacho hakijali tena maslahi ya wengi jitihada yako haita fika mbali.
 
Ha ha ha Kigwangala hiyo ndiyo CCM lazima wakukabe koo,uwe ndani ya hicho chama utetee wananchi? subiri ni imani yangu wanakuhesabia wakuchakachue.Hicho ni chama cha maslah binafsi.

Sina shaka na wewe kwenye kudai haki kwani najua ulivyoongoza mgomo wa madaktari Muhimbili kudai maslahi yao ila wasiwasi wangu ndani ya chama hicho cha ghilba ambacho hakijali tena maslahi ya wengi jitihada zako hazita fika mbali.
 
Kigwangala kweliumedhamiria? hvi unafahamu kuwa serikali ya kijiji kinachozunguka mgodi walisainiana mkataba na mgodi kuhusu kupewa hudumaa za kijamii? je nani anafuatilia utekelezaji huu, mimi ninatarifa za kina kuwa jambo hili siku hizi halitekelezeki, unajiamini na upo pamoja katika mapambano dhidi ya mafisadi hata kwa gharama yoyote, jitokeze unijibu kwani kwa sasa ninatafakari kulifikisha suala hili kwa CHADEMA
 
CCM ina wenyewe nao ni mafisadi, wengine wote ni washika pembe tu! Kama kweli Dr Kigwangala amedhamiria kutetea haki za wananchi wake ajue tu kwamba hiyo ni vita kati yake na mafisadi, lakini akisimama imara atashinda kwasababu wananchi (nguvu ya umma) watamuunga mkono.
 
... hii ni mechi ya timu ya wachezaji wa akiba na kikosi cha kwanza, Aina mvuto
Kigwangala kampiga buti Ngeleja mazoezini, anataka sifa achukue namba, kumbe kocha mwenyewe anataka timu lake lishindwe, namba ya Ngeleja hachukui, na asipoangalia hata benchi watamtoa kama Selelii.
 
Back
Top Bottom