Sera ya maendeleo ya vitu, imesababisha uwepo wa miundo mbinu ya maandamano

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,308
24,200
JAKAYA KIKWETE MUASISI WA JIJI JIPYA LA DAR ES SALAAM LENYE MIUNDO-MBINU YA KISASA

1706209031282.png

Awamu ya nne chini ya rais Jakaya Kikwete kwa nia safi isiyo ya kidikteta iliasisi ujenzi wa barabara pana za kisasa na za njia nne hadi nane ni mradi wa maendeleao ya vitu ambayo sasa inatumika kuibana CCM kukubali mbinyo wa sauti kubwa za wananchi wanaozitumia kufanyia maandamano kudai maisha bora (maendeleo ya watu) , katiba mpya, demokrasia na utawala bora.

1706206854709.png
Picha: Mbezi kituo cha Magufuli Dar es Salaam

Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli kama alivyokuwa bwana jiji la Paris France mjenzi Baron Hausmann 1853 - 1870 alipoongoza kulivunja jiji la Paris la miundombinu ya kizamani ya majengo na barabara nyembamba, Baron Haussmann a.k.a tingatinga wa mtawala Louis-Napoléon Bonaparte alifanya kazi hiyo kwa kujituma sana kujenga barabara pana, majengo ya kisasa.
1706208754363.png

Picha : Vichochoro vya Paris ya kabla ya mwaka 1850​


Mtawala Louis-Napoléon Bonaparte aliogopa Paris ya kizamani yenye barabara za kupindapinda na vichochoro kedekede ambavyo vilitumika na wapinga watawala mabwanyenye kuleta vurugu na kutokomea vichochoroni.


Napoleon alikuwa na visheni ya kuona mbali kuwa licha ya kuigeuza Paris iwe jiji la kisasa lenye barabara pana zilizonyooka lakini miundo mbinu hiyo pia itafaa kupambana na waandamanaji kwani wataonekana kwa mbali na ni rahisi kuwadhibiti kwa vifaa vya kisasa na kuwazingira waandamanaji mithili ya mifugo inayolazimishwa kuingia katika dimbwi la josho la ngombe.

Louis-Napoléon Bonaparte aliona sasa zana za kisasa wakati huo kama askari wakutisha wanaokuja kwa kasi waliopanda farasi wengi, huku wamebeba virungu, ngao na zana zingine watakuwa na urahisi wa kuzima na kudhibiti maandamano.
The radical transformations of Paris – essentially the result of Louis-Napoléon Bonaparte’s desires and Baron Haussmann’s actions – did open the door to modernity, they also created, through their social consequences, the conditions for the revolution of 1871 ...

Ilikuwa kweli kwa kiasi fulani kipindi cha utawala wa Louis-Napoléon Bonaparte lakini baadaye miundombinu hiyo ikaweza pia kutumika kufanya maandamano makubwa yanayohushisha watu wengi wenye kutisha kuliko ilivyokuwa awali kulipokuwa na barabara nyembamba na vichochoro.

Kiongozi mtawala John Magufuli aliona mbele wakati akitumika kama kiongozi mnyampara kama waziri wa ujenzi asiye na masihara, na alipopata urais akaona aende mbali zaidi ya njia za mwendokasi na kujenga njia za juu flyover Mfugale flyover, John Kijazi flyover na kadhalika akiona mbele zitatumika na vikosi vyake kupambana na waandamanaji kama enzi za mtawala Louis-Napoléon Bonaparte.
1706208453070.png
Picha: Flyover mojawapo ya DSM
Infrastructure expenditure during the apartheid years in South Africa was relatively high as a percentage of GDP. The apartheid state made excessive investments in infrastructure that served mainly the white minority and maintained the apartheid state.
Vyombo vya askari ya maji ya washawasha, defenders, gari za deraya, pikipiki n.k yangeweza kutoka mbio toka eneo moja la mji kwenda jingine kupambana na wapinzani waandamanaji. Flyovers zingetumika kama ngome, vilenge na viota vya ulinzi kupunguza kasi ya kwenda mbele wapingaji wa utawala wake.
1706287375722.png

Picha maktaba: vyombo vya dola wakati wa awamu ya 5.


Awamu ya 6 imeona mikakati hiyo ya wahafidhina kama kina John Magufuli waliobaki ndani ya CCM haifai na imepitwa na wakati, kutumia maendeleo ya vitu kama barabara za njia nne, sita hadi nane pamoja na flyovers ili kungangania katiba na sheria mbovu ili kubaki madarakani kwa hila zote ikiwemo kodi iliyotumika kujenga maendeleo ya vitu kuwa kikwazo cha kungolewa madarakani.

Awamu ya sita ya CCM sasa imepatiwa nguvu ya umma kuwadhibiti wahafidhina waliopo ndani ya CCM wasiotaka mabadiliko ya sheria na katiba.

Kwa hali hiyo tutegemee wahafidhina hao wachache ndani ya awamu ya tano ambao wamebaki, wamejaribu kumpa shindikizo kiongozi mkuu wa awamu ya sita wa CCM kubana maandamano, watambue wameshindwa na hivyo tarehe 30 January 2024 serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan imepata nguvu mpya kuondoa sheria mbovu na kukaribisha katiba mpya yenye mabadiliko msingi muhimu (ya minimum reforms) ifanyike.

Hakika chini wa utawala wa Rais Samia Hassan kwa kuangalia vuguvugu la ndani ya nchi na pia dunia hii kijiji - global Village alikuwa anasubiria tukio hili muhimu la maandamano.

Na mheshimiwa Rais amejiandaa kwa kutumia mfano hai wa historia iliyoandikwa tarehe 24 January 2024 kuwaambia wahafidhina ndani ya CCM kuwa zama za tawala gandamizi kwa kutumia chama dola kongwe na vyombo vya usalama kuzuia mabadiliko hazina nafasi tena, hivyo vyombo vya maamuzi lazima viongozwe na wale walioshinda kihalali ngazi ya vijiji, kata, wilaya, majimbo-bunge na Urais

1706209419074.png
Picha : Paris 1870 soma zaidi source :
 
UCHAMBUZI WA KINA MAFANIKIO YA MAANDAMANO NA CHANGAMOTO ZA WATAWALA WAHAFIDHINA CCM KUVURUGA NGUVU YA UMMA

Miundo-mbinu ya CHADEMA msingi yashinda mbinu za mahafidhina wa CCM waliojaribu kukwamisha R4


View: https://m.youtube.com/watch?v=pFsk2vWDsU0

Mwamko wa wananchi nyuma ya maandamano.....

Media house zilizotumika na wahafidhina walio katika chama tawala na serikalini kujaribu kukwamisha maadamano...
 
Wafahamu baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa NEC CCM wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM katika kuaminiwa kuanzisha jambo jipya

1706231789824.png

Ndugu Sophia Mjema nafasi yake uenezi ameteuliwa ndugu Paul Makonda na ya Daniel Chongolo aliyekuwa katibu mkuu nafasi yake Dkt. Emmanuel Nchimbi


Picha Toka Maktaba :


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,kabla ya kuaza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashuari ya CCM Taifa, kilichofanyika katika Mkoa wa Kusini Unguja leo 15-1-2024 na (kulia kwa Rais) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhandisi Nassir na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Kassim Majaliwa.


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo 15-1-2024, katika Mkoa wa Kusini Unguja.


WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakisoma ajenda za Kikao hicho kabla ya kuaza, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika Mkoa wa Kusini Unguja leo 15-1-2024.

(Picha kwa hisani ya Ikulu)
 
Back
Top Bottom