HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
Akizungumza na NIPASHE jana jioni kuhusu madai ya kufungwa kwa mgodi, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema suala hilo ni la kisheria na anachofanya Dk. Kigwangalla(Mbunge wa Nzega-CCM) ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Ngeleja alisema kama kuna madai ya msingi Dk. Kigwangalla angefika ofisini kwake kuyasasilisha ili apate kauli ya serikali.
Mbunge huyu ni miongoni mwa wabunge wanaotunga sheria za nchi na yeye anazijua, lakini nashangaa anapohamasisha wananchi kuzivunja, alisema Ngeleja.
Hata hivyo, Ngeleja alisema wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa Golden Pride wapo kisheria na hawawezi kuondolewa kwa njia ya
maandamano. Alimtaka mbunge huyu kama ana madai ya msingi kuwasiliana angalau na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ili kujua kama mgodi huo una athari zozote za mazingira kulingana na madai yake.
Sigma, KTY Waziri Ngeleja hayuko katika nafasi yoyote ile kupinga Maandamano! Haya locus yoyote ile kwa kweli.
Na kauli yake imenishangaza sana. Hususan anaposema Mbunge na wananchi wanavunja sheria, sheria ipi? Sidhani kama yeye kwa utaalamu wake kisheria au hata uzoefu wake tu anaweza kusema kama alivyosema. Kusema kwamba eti kufanya maandamano ya amani ni kuvunja sheria ni upotofu wa hali ya juu!
Nadhani Mwandishi wa NIPASHE alimnukuu Waziri wetu vibaya au basi Waziri alikuwa amechoka sana na kazi siku hiyo, ukizingatia ilikuwa Ijumaa!