Neno lolote toka kwa mpenzio ambalo liliutikisa moyo wako

Usining'ang'anie maana bado sijaoa nna haki yakuwa na wanawake varieties kwenye mahusiano niweze kuchagua! kwanza sijawahi kufikiria kudate na mtu muislam ama background ya kiislam umenitokea wapi kama shetani wewe mwanamke? wewe sio type yangu
hahahahahahhahahah jf bhanaaaaa khaaaaa pole sana
 
"nina mimba yako na sina mpango wa kutoa",nilikuwa bado kijana sana na nliona kama itanihalibia mipango yangu maana nlikuwa form 5 pale tambaza nliona kama mkosi il leo hii mkosi umekuwa fulaha ya maisha maana kwel hakutoa na akanizalia kidume mpaka leo nikiwa nae watu huhisi mdogo wangu!!!!
je huyo mama mtoto uko naye bado?
 
Yaaan wanaume bhana ni kiboko yaaaan alianza visa tu akawa busy Sana na simu wakati wa usiku nkimpigia nakuta inatumika anakuja nipigia baadae sana namuuliza kulkon mwenzangu busy unaongea na nani akanijibu usitake kujua naongea na nani maana ukijua utajiumiza tu daaaa nkameza mate nkamwambia usiku mwema lakini sikupata usingizi kwelii sasa hapo ndo mwanzo wa visa akaniambia anahitaji break kidogo lakini nkawa nampigia simu mimi namwambia mimi siwezi yaan kukupotezea kukusahau hajibu kitu nilpojua kanichoka akanipgia usiku akasema unataka nikupe nin au nikufanyie kitu gani ili unisahau haya maneno yalikuwa magumu ila yalnipa ujasiri wa kumuacha kabisa sikumtafuta tena baada ya miezi miwili akaanza kunitafuta kwa namba mpya akajitambulisha shida yako eti nisamehe natamani nirudishe muda nyuma turudiane khaaaaaaa
mwenzio labda break imeishaaaa hahhahahhaha hapa ndipo nasemaga shikamo mapenzi fyuuuuuu
 
"Kitambaa cheupe kikiingia DOA JEKUNDU huo ni UCHAFU na hakifai tena ..... lakini hilo DOA JEKUNDU mkiliweka wenyewe ni PAMBO ....

Mapenzi yetu yameingiwa na UCHAFU cause siwezi kuwa na mpenzi ambae hana hela .....
Tafuta hela tena siku ukizipata nishtue ..."

Kamwe sitoweza sahau hiyo kauli ... NEVER
khaaaaa watu wana roho ngumu kweli
 
Ex bf wa kwanza aliniambia "hatuwezi kudate nina mtu wangu niache." Nilikua nampenda kuliko kitu chochote. Hiyo statement iliniumiza sana. Namshukuru Mungu baada ya miaka miwili niliweza kumove on nikapenda tena japo nimetendwa tena.
Daaah,,,pole sana.Uzuri ni kwamba hujatendwa mara mbili na mtu mmoja,,,move on and time will heal
 
"angalia namba hii kwenye m-pesa ina jina la nani"
kajasho flani kembamba kakanitiririka mpaka mikononi!

Sijui nilikukosea nini Mary!!
huwa nasikilza nyimbo ya Mandojo & Domo kaya - nizikwe hai .....huwa machozi yananilenga machoni......
 
Mimi ilikuwa hivi

Shani:Sijaziona siku zangu

Me:What nikavurugwa kabisaaa nikawaza sina kazi maisha magumu ndo kwanza nipo shule nikamjibu,Mimi siko tayari kuwa na familia kwasasa.
Alichonijibu sasa...!!

:Kwani me nimekwambia ya kwako.

Mpaka now niko milembe toka 2012 sema ni kiongozi wa vichaa tu wananiamini kidogo wamenipa na simu .
Hakika ''Unakula ili uishi''
 
Kuna wanawake nliwaumiza, nawahurumia na nliwaomba msamaha ila hakuna nliewahi mtolea kauli chafu. Mara nyingi mapenzi yalikua yakiharibiwa na umbali maana nlikua nasafiri sana, hivo nkienda sehem miezi miwili mitatu natafuta mtu, nikiondoka hua sikumbuki. Ila hadi leo wote nawasiliana nao vizuri.
Kuna mtu aliuumiza moyo wangu vibaya
"Upendo wangu kwako sijui umeenda wapi, na sina ndoto tena ya kuolewa na wewe. Samahani, sijui utaiambia nini familia yako" ilikua ni kama wiki kadhaa toka nimepeleka posa kwao.
Ila nikasahau japo yeye sijamsahau, nikaoa mwingine.
 
Sijawahi kukuahidi kuwa nitakuoa ....maneno haya aliyasema baada ya Mimi kumkuta na mwanamke mwingine wakati Mimi tayari Nina mtoto wake wa mwezi mmoja...sitayasahau hadi kufa kwangu..
Dah Pole mkuu,lkn sasaiv mtoto yupo fresh,?Baba ake ana mtunza?Pole mkuuu
 
Mbwa wangu anaitwa donald trump
e4f060e6cd6763fa63e7ecbf96371d48.jpg
 
Kugundua ananicheat na baada ya kuuliza akanijibu kistaarabu kabisa ww sie nnaekupenda bali ni yule mwngin..kidogo nizimie na aliniomba msamaha kbs kwa kunidanganya tukaendelea kua marafiki wa kawaida na sikumuwekea chuki baada ya miaka 3 akajirud na machoz juu kua hakua sahihi na anachokihitaj kwani anahiskukaa mbali na mm kimapenz amegundua ni mm ndie anipendae zaid.
ni kweli hukumwekea chuki?..
.sikumfanyia hiyana niko nae mpk ss ila nnavyompelekesha Mungu ndie anajua na sina mapenz nae km mwanzo na hivyo kapata kaz nzuri mbona nafaidii
kwa nini unampelekesha na huna mapenzi nae kama hukumwekea chuki?..kuna ukakasi hapa.. zaidi ''alikujibu kwa ustaarabu''
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom