Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,797
- 12,239
SUMATRA ni mamlaka iliyo chini ya Serikali kudhibiti vyombo vyote vya majini na nchi kavu vinavyomilikiwa na mashirika ya umma na binafsi na siyo EWURA! Hivyo nauli ya vyombo hivi hupangwa na SUMATRANadhani alitaka kusema SUMATRA ambayo ina deal na surface and marine transport.
Ingawa pia tumeelezwa hapa kwamba waziri ana mamlaka kisheria kuongeza nauli ya kivuko.
Nadhani hapa ndipo kuna mkorogano, nani ni nani kwa sheria gani!
Kuhusu vivuko vya Kigamboni na vile vilivyomo katika maeneo mengine vinamilikiwa na Wakala wa Serilkali yaani TEMESA na hivyo mamlaka ya kuvidhibiti ni Wizara ya Ujenzi. Hivyo nauli za vivuko hivi unapangwa na Wizara moja kwa moja na si SUMATRA.
KInachogomba hapa ni kauli ya kibabe na kuwadharau wabunge wenzake ya MHe. Magufuli. Na hii ni tabia yake hata katika sherehe nyingine za kiserikali anapokuwa anawakaribisha wakubwa wake wa kazi kuzindua miradi ambayo iko katika majimbo yaliyo chini ya wapinzani hutoa maneno ya kejeli kwa wapinzani na viongozi wake wanabaki kukenua meno tu! Ni vizuri Rais na Waziri Mkuu waanze kumkemea ili kukomesha tabia hii