Ndugulile: Magufuli hajui sheria, anakurupuka tu...

Tunapoelekea siku tutaambiwa tuwe tunalipia kila Pumzi Buku tuvukapo kigamboni watu lazima Wahame!
 
Waziri anayehusika na mfumko wa Bei ni yupi maana Bidhaa zishaanza Kupaa Juu Na maisha yameanza kuwa juu kuliko Dodoma...
Wananchi itabidi nasi tuwe tunapewa Posho
 
hiyo ni strategy ya kuwaondoa kigamboni ili bush aingie kilaini

Hii naikubali inaweza ikawa ni triki ya kuwahamisha kijanja,any way naipongeza sana serikali kwa kuzidi kuwakasirisha wananchi,mpaka ije kufika 2015 kitakuwa kimeeleweka.
 
Watanzania sometimes lazima tujilaumu, kile kivuko kinavukisha watu wangapi kwa siku?
Nina uhakika kinaweza kuingiza milioni 20 kwa siku, ukitoa gharama unaweza kupata 5-10m a day by just charging 100.
Something is wrong somewhere.
 
Kuna kigezo kimoja Magufuri alikitumia aliposema Mshahara wa Miaka kumi na sita iliyopita kima cha chini kilikuwa ni 45,000/= Rates ya Dollar ilikuwa ni $500 na kiwango cha sasa ni 150,000/= Rate ya Dollar ni $1750

So Mshahara wa 45,000/= ni sawa na Dollar $90 ----1996
Na Mshahara wa 150,000/= ni Sawa na Dollar $86 ----2011

HApo Sasa Mshahara Umepanda au Umeshuka???
Tumethubutu, tumeweza na tuna songa mbele....Kidumu chama cha Mafisadi....
 
Ni kweli kipo chini ya wizara yake lakini nafikiri SUMATRA ndio wanamamlaka ya kupanga bei wakishirikisha wadau. Suala linalomwandama Mgufuri hapa ni kauli ameshindwa kuwasilisha hoja yake kwa maskini lakini nauli kuwa 200 sifikirii kwamba ni tatizo kubwa. Hii inatufundisha viongozi wanatakiwa wachunge midomo yao kwani siku moja tu unaweza ukaharibu sifa zako zote

Kwako ni ndogo lakini kwa wenzako ni kubwa sana. Fikiri mtu anayefanya shughuli zake K'koo na anakaa Tungi au Mjimwema. Tungi-Kigamboni,300/=; Pantoni-200/=; Kivukoni-K'koo 300/=. Jumla kwenda na kurudi ni 1600 per day. Assume ni siku moja kwa wiki havuki, kwa mwezi atatumia 41,600/=. Sasa hebu tia akili.
 
leo kwa suala la nauli kupanda ndo wanadai wananchi wataumia, lakini suala la posho hawakuonekana kulipinga, nonsense
 
Hivi mnajua kuwa sio wavukao tu walioongezewa? Kwa mfano gari ndogo imepanda kutoka sh 800 hadi sh 1,300 na baiskeli ya miguu mitatu imetoka sh 200 hadi sh 1,800 nani anaumia hapa?
 
hivi hakuna uchakachuaji pale? Mi nilitoa sijui sh ngapi nikarudishiwa sijui sh ngapi... Nililipia watu wanne.Hesabu za harakaharaka, nikaona nimekatwa sh 600 au 400 kwa kichwa..
 
Hebu fikiria baiskeli ya miguu mitatu kutoka 200 hadi 1800 ongezeko la sh ngapi ukilinganisha na gari ndogo kutoka 800 hadi 1300. Nani anaumia hapa kama sio mlalahoi, tabu iendelee tu watu tutie akili!
 
Live Channel Ten Mbunge wa Kigamboni Anamuumbua live Live Magufuli na Wazara yake kuwa Hawana haki ya kuongeza Nauli Mpya kwani hiyo mamlaka amaepewa EWURA tena lazima Wadau washirikishwe...

EWURA, kwan ndo wanapanga nauli?!!
 
Hebu fikiria baiskeli ya miguu mitatu kutoka 200 hadi 1800 ongezeko la sh ngapi ukilinganisha na gari ndogo kutoka 800 hadi 1300. Nani anaumia hapa kama sio mlalahoi, tabu iendelee tu watu tutie akili!
Malima alisema Upandishaji huu hautamguza Raia wa Kawaida? Sasa wenye Guta nao ni Matajiri?
 
suala la nauli ya kivuko hata wadau wangejadiliana isingebadili chochote ila na wananchi pia tuangalie je unaweza kulinganisha nauli ya mwaka 96 na leo hii ? Fikiria hicho kivuko unapewa wewe unaweza kuendesha kwa gharama ya sh mia?
 
Back
Top Bottom