Maxence Melo: Kiongozi ukishakuwa kwenye ofisi ya umma kukosolewa ni haki yako

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Fuatilia mahojiano yanayoendelea wakati huu Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akizungumza kuhusu Matumizi salama ya mitandao ya kijamii.



Matukio ya wananchi kukamatwa sababu ya kumkosoa kiongozi fulani, hii imekaaje?

Maxence
: Mwananchi ana haki ya kupata taarifa kutoka kwa kiongozi, na kama kiongozi hatazitoa ni haki kwa mwananchi kumsema, kuwakamata ni kuvunja haki za watu.

Wananchi wana haki ya kupata taarifa taarifa, viongozi wanatakuwa kuelewa wanaongoza watu wanaojielewa na wasiojilewa, viongozi wanatakiwa kuwa na ngozi ngumu na waelewe zama hizi sio zama zile.

Maxence ameongeza kuwa viongozi wawaeleweshe wananchi pale ambako wanakuwa hawajaelewa, na siyo kuwachukukulia hatua watu wanapotoa maoni yao au kuwapa watu mipaka ya kuongea isipokuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizokubaliana kuwa amevuka mipaka, mfano mtu akihamasisha mtu fulani kuuliwa.

Kuna ukomo kwa mtu binfasi kupeleka taarifa zake binafsi katika mitandao ya kijamii?

Maxence
: Taarifa binafsi za mtu zinatakiwa kuheshimiwa na kulindwa na taratibu na sheria za nchi husika, ndani na nje ya mitandao, na za watoto zaidi.

Ama umezipeleka wewe au lah, una haki ya kudai haki kudai hako yako na kuhakikisha faragha yako inalindwa. Ni bahati mbaya sana, wananchi ambao ni wahusika wa taarifa (data subject) wengi hawajui haki zao.

Pamoja na kuwa kuna Haki, kuna Wajibu pia. Unapokubali kurekodiwa, ukaenda kwenye tukio la aina fulani ukarekodiwa, au ukaenda mahali ukaambiwa toa taarifa zako ukatoa mwenyewe wewe ndio utakuwa umesababisha madhara (yakitokea) kukufika!

Vipi ikitokea mtu amejirekodi kwa matumizi yake binafsi halafu mtu/blogger akichukua video ya hiyo na akaipost kwenye mitandao ya kijamii bila ridhaa yake, hili limekaaje?

Maxence
: Kwanza lazima watu waelewe, chochote kinachoingia mtandaoni si chako tena!

Ikiwa mtu alirekodiwa wakati wa faragha, kitendo hicho cha kurekodi tukio la faragha ni kosa kisheria! Ukikamatwa na vyombo vya dola (mf. jeshi la polisi) ukiwa na ponografia kwenye simu yako ni kosa hata kama ulikuwa unajirekodi wewe mwenyewe kwaajili ya kujiona, makosa mengi ni ya wanaokubali kujirekodi.

Kuna wale wanaokuwa kwenye mahusiano, unaambiwa naomba ujipige picha unitumie, tuko kwenye ulimwengu wa digitali na matumizi ya AI ambapo picha inaweza kuongezewa vitu (manipulated), picha video zako zitakavoja kwakuwa ulikuwabali kurekodiwa, usilaumu, mjinga ni wewe, hata kama ulijidanganya kwamba unapenda, kumbuka kupenda ni jambo jingine na kujirekodi ni jingine ambapo inamaanisha umekubali kuingia kwenye makosa.

Mtadanganya haitafika popote au hamtavujisha, lakini mtu wa inawezekana asivujishe mmoja wenu akaja kuvujisha fundi wa simu, ambapo anaweza asihamishe video zile na kuzitoa kutoka kwenye simu yako moja kwa moja bali akabaki na kopi.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo naiona kwa wengi wanadhani simu ukiiwekea password ndio wameilinda, hapo hujalinda simu unakuwa umeweka ili watoto wasije wakaichezea na kuiharibu.

Kuchukua chochote kilichokuwa kwenye simu haiitaji akili kubwa, ni kidogo tu na kila kilichokuwa kweye simu yako kuhamishwa, bila mtu kushika simu yako wakati mwingine.

Kwa hiyo ni kujitahidi kutokuwa na picha chafu, au video za aina yoyote chafu kwa sababu kuna gharama ya kubwa ya kulipa kwenye hilo hata baadhi kufikia hatua ya kujiua.

Vijana wengi hawatumiii mitandao ya kijamii kwaajili ya jiendeleza na kufanya mambo ya kimaendeleo, wewe kama mdau unashauri nini katika hili?

Maxence
: Siwezi kuwalaumu vijana, wanatumia mitandao vizuri. Mitandao haipo kwaajili ya kuandika habari za siasa, au kuafuta pesa pekee, hata kuonesha sura yako Dunia ijue kuwa unaishi ni matumizi mazuri kwako! Tusijaribu kuwapangia watu kuwa matumizi mazuri ya mtandao ni kuanzisha biashara ili uweze kupata hela, sio sawa.

Kama anaweza kutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na marafiki zake wa zamani akawapata ndio kitu kizuri kilichompeleka mtandaoni yeye, vizuri. Lakini kama uko mtandaoni kutafuta fursa ukaweza kujiajiri kupitia mtandao na ukapata hela, hiyo pia ni vizuri.

Kwahiyo wewe unayepata hela usiwapuuze wale wanaotumia tofauti na malengo ya kutafuta pesa, vile mtu anatumia kifaa chake cha digitali, mtandao ndivyo ilivyo sahihi, mradi tu hajavunja sheria za nchi.

Kuna watu wanatumia JamiiForums wamepata wake, kuna watu wanatumia JamiiForums wanauza sana biashara, kuna watu wametumia JamiiForums kupitia Stories of Change kimesaidia vijana wengi kupata pesa, kuna fichua uovu ambayo imesaidia wananchi wengi katika kutoa kero mbalimbali za masoko, barabara, maji, nk, vimetatuliwa na mamlaka husika.

Hivyo siyo lazima kupiga pesa, unaweza kutumia mitandao kwaajili ya kusukuma viongozi wako kupata uwajibikaji, unaweza kutumia wewe mwenyewe kwaajili ya kupata umaarufu, nk, vile wewe unataka ndicho mtandao utakupa.

Tusilaumu mitandao tukidhani kwamba mitandao yenyewe ndio inatengeza kitu, watu wale wale unaowaona mitandaoni ndio wale wale unaowaona mtaani.

Tulipotoka mwaka 2020 kipindi cha uchaguzi badhi ya mitandao ya kijamii ilifungwa, ilikuwa haipo kabisa, je mtu binafsi anatakiwa kupangiwa kuwa kwa wakati huu mtandao huu hautakiwi kuutumia ukizingatia tunaelekea kwenye uchaguzi wa 2025?

Maxence
: Sijui, hakuna aliyezima mitandao 2020 ni bahati mbaya kuna watu wanadhani mitandao ilizimwa 2020, hakuna aliyezima mitandao. Ni vizuri watu wakaelewa kuzima inamaana haifanyi kazi, haipo kabisa, mitandao ilikuwepo, kuna kitu kinaitwa blockage - uzuiaji wa kufikia mitandao hiyo. Hii ni ukiukwaji wa haki za watu na tusicheke na mtu yoyote anayekuja na lugha yoyote kwamba hizi ni haki zetu, tuna haki ya kupata taarifa bila kujali mipaka ya nchi anayekuzuia kufikia X, TikTok, Clubhouse ni adui yako, usimchee hata kidogo. Kuna kosa gani wewe kutumia mitandao hiyo?

Yawezekana kuna mtu mmoja au wawili wamefanya kitu kisicho ndani ya mtandao fulani, sasa watu wawili wamewakaza mnataka kila mtu asifikie huko? Ni kosa kubwa sana. Viongozi wetu au yeyote anayejaribu kufanya kitu kama hicho amekosa ubunifu wa kushughulika na wahalifu.

Usikoseshe watu zaidi ya milioni 38 utamu wa shughuli fulani kwasababu wewe kuna watu wawili au watatu wamekukwaza, hatuwezi kuishi hivyo kwasababu, mtu anayefanya hivi ukimchekea leo kesho atafanya zaidi kwasababu anajua anaweza kufanya zaidi na huna cha kumfanya!

Namaanisha hata ikitokea wakati wa uchaguza wa 2024/2025 akithubutu mtu yoyote kufanya sidhani sidahni kama suala la haki za kidigitali anayetakiwa kuwa mtetezi ni Maxence peke yake kwasababu aliyeathirika 2020 siyo Maxenxe peke yake, tushirikiane kukemea uhuni wa aina yoyote.

Vipindi vya uchaguzi huwa vinagubikwa na taarifa nyingi ya upotoshaji hasa kwenye majukwaa ya mtandaoni, je kuna mikakati ya aina yoyote ya kuweza kuzuia suala hili ukizingatia watumiaji ambao wanakuwa hawana namna ya kujua kama taarifa hii ni sahihi au lah?

Maxence
: Tunatambua kwamba taarifa potofu/upotoshaji ni kitu ambacho hakijaanza leo, kipo tangu zama za babu zetu, kinafanyika kwenye vyombo vya habari, magazeti enzi hizo, redio, lakini naomba mkumbuke mtoshaji mkubwa siyo mwananchi mamlaka, wanaweza kukwambia uchumi unaenda vizuri na watu wote mkakubali lakini mkijishika mfukoni hali ni mbaya, na mwathirika mkubwa wa upotoshaji huu ni mwananchi.

Mamlaka ikidanganya unaweza kuwambiwa kwamba ilikuwa ni bahati mbaya, mwananchi akidanganya kamata weka ndani, au mwanasiasa akisema uongo unasema hizo ni siasa na propaganda mwananchi akisema uongo unasema kamata huyo weka ndani/mshughulikie/huyu alikuwa anapotosha kwenye mitandao, hivyo muelewe upotoshaji ulikuwepo tangu enzi.

Ili kukabiana na hili JamiiForums tulianzisha jukwaa maalum linaloitwa JamiiCheck, la kwanza Afrika la aina hiyo kutokana na hitaji la wadau wengi kuhitaji wa sehemu ambako wao watashiriki kwenye mchakato huo. Mtu akikutana na taarifa yoyote kutoka mtandao wowote anaweza kuweka JamiiCheck kuuliza hiki kitu kikoje, ndani ya masaa 2-24 kitakuwa kimefanyiwa kazi, tuna wataalamu ambao wamefunzwa wanakusaidia kuweza kujua ukweli wa taarifa husika.

Tusilaumu mtandao kuwa ndio unaochangia kuongeza taarifa potofu hapana, ongezeko la watu duniani na ongezeko la watu wanaotumia mitandao linawafanya watu wengi kuweza kupokea taarifa na kudhani kwamba ni ukweli na kutokana na nyenzo/njia za ufikiaji ambazo watu wanazo taariza zinakuwa zinasambaa kama kwa kasi ya mwanga.

Kwaajili ya kuhakikisha jambo hili linarahisishwa JamiiCheck mpaka sasa imeshapitia maudhui zaidi ya 400 kusaidia watu kujua masuala ya Kiafya, Kisiasa, Kiuchumi nk zikieleza taarifa zilizotolewa, ukweli wako na palipokuwa panapotoshwa, na kuna vingine vinakuja kama tetesi na vinakuwa kweli basi utaambiwa jambo hili na la kweli.

Hatujaishia kufanya hivyo tu, tumeanzisha urahisi wa kusaidiana wataalamu wengine kwenye uwanda huu, kuna watu walikuwa wanatuona kama chombo cha habari, ili kurekebisha na kuondoa dhana hiyo tumeanzisha mradi maalum wa kujenga uwezo kwa wana habari.

Tunajenga uwezo wa wanahabari takribani 300 nchi nzima na tunashirikiana na klabu 28 za waandishi wa habari nchini, lengi ni kuwa na waandishi wa habari wanaondika habari zenye tija, maslahi ya umma na habari za uchuguzi na pia kuwasaidia wanapoona habari waweze kujua viashiria vinavyopelekea taarifa ziweze kuwa na uongo hata kama kiongozi au mamalaka imetoa taarifa utajuaje kuwa kuna viashiria hivi vimechomekewa kuna namna wanahakikisha kupotosha umma.

Tunafanya hivi kuhakikisha kwamba tunamsaidia mwananchi kufanya maamuzi sahihi akiwa na taarifa sahihi.

Katika ulimwengu huu wa sasa wananchi wengi hawajui kuhusu masuala ya tarifa binafsi wala faragha wewe kama mdau wa haki hizi unaweza kumshauri afanye kitu gani na kipi asifanye?

Maxence
: Wananchi watambue sheria imewekwa kwanza kwaajili ya kuwalinda wao wakiwa ni namba moja, ni vizuri tutakapoanza kutoa elimu kwa umma kuhusiana na haki na wajibu wao wasikilize kwa umakini. Tutafanya hivyo kwenye mitandao ya kijamii, nje ya mitandao ya kijamii, katika vyombo vya habari, kuhakikisha kwamba wnanchi wanajua haki yao ya faragha na inalindwaje kw amujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Shida ninayoiona watu wanaangalia leo na jana wanasahau kuna kesho. Aina fulani unayoweza kupigwa, taarifa zinazoweza kuchukuliwa kwako leo ukiwa na njaa, hamu ya kujulikana, kuwa maarufu au kuonekana inaweza kuwa na madhara miaka mitano au kumi ijayo ikiwa wewe ni mtu mwingine.

Kumbuka kila baada ya miaka mitano wewe siyo yule wa jana na kwasababu hiyo, leo huenda hauna nafasi katika nafasi ya kimaamuzi au hujawa kiongozi, kesho ukaja kuwa kiongozi video iliyochukuliwa miaka kumi iliyopita inaweza ikasababisha usipate nafasi ya kazi, inaweza kusababisha usiwe kiongozi wa nchi. Kwahiyo tunataka pia uelewe una wajibu wewe kujilinda kabla mamlaka hazijakulinda ukisubiri mamlaka zikulinde au usubiri upate madhara ili uende kulalamika inaweza ukawa umechelewa sana, mwisho wa siku jinsi ya kurejesha kile kilichopotea inachukua muda sana.

Wamiliki wa taarifa (data subjects) waamke, mtu unaomba namba ya simu we unagawa tu, upo kwenye sherehe wanarekodi na wewe unacheza tu kurekodiwa, kuna gharama, unapita sehemu mtu anakuomba naamba ya passport unatoa tu bila ya kujihoji, na hujui taarifa hizo anapeleka wapi, unakosea.

Kwa wakusanyaji na wachakati wa taarifa ni vizuri tukawa tunawaheshimu watu. Tuache kutumia taarifa za watu kwa biashara kwaajili ya kujitafutia umaarufu. Walimu wanaorekodi watoto shuleni, wanawapiga picha na kuweka kwenye mitandao wanakosea sana, wanavunja sheria za nchi. Wazazi wasiruhusu watoto kupigwa picha ovyo na kuwekwa kwenye mitandao bila ya kuwa wameridhia.

Wananchi wasiache kuhoji kwanini kwa kila anayeomba taarifa kutoka kwako kwasababu ni haki yako.
 
Fuatilia mahojiano yanayoendelea wakati huu Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akizungumza kuhusu Matumizi salama ya mitandao ya kijamii.



Mwananchi ana haki ya kupata taarifa kutoka kwa kiongozi, na kama kiongozi hatazitoa ni haki kwa mwananchi kumsema.

Wananchi wana haki ya kupata taarifa taarifa, viongozi wanatakuwa kuelewa wanaongoza watu wanaojielewa na wasiojilewa, viongozi wanatakiwa kuwa na ngozi ngumu na waelewe zama hizi sio zama zile.

Maxence ameongeza kuwa viongozi wawaeleweshe wananchi pale ambako wanakuwa hawajaelewa, na siyo kuwachukukulia hatua watu wanapotoa maoni yao au kuwapa watu mipaka ya kuongea isipokuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizokubaliana kuwa amevuka mipaka, mfano mtu akihamasisha mtu fulani kuuliwa.

Kupongezwa na Kusifiwa ni stahiki ya kiongozi pia 🐒
 
Sio Kwa Tanzania yetu

Unaweza kumkosoa Kiongozi Kwa lengo la kutaka ajirekebishe lakini akageuka kukuona adui yake

Hii inaweza kupelekea hata upoteze Uhai ama ushikishwe adabu kwa kupigwa na kujeruhiwa🙌
 
Back
Top Bottom