MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,927
- 6,849
you live by the sword and die by it! No other way.ndugu mmoja (jina kapuni kwa usalama wake), wa karibu wa bwana ahmed msangi , askari anayechukiwa kuliko kila askari hapa nchini kwa tuhuma za utekaji na mateso ya Dr. Stephen Ulimboka, amenukuliwa akilalamika kwamba ndugu yao ametolewa kafara na kuyaweka maisha yake hatarini wakati yeye alifanya kazi aliyotumwa na wakubwa.
"ndugu yetu amechafuka sana jina kiasi kwamba anatembea kwa wasiwasi kila anakokwenda. hamedi hana amani na tunaona kama vile yeye alitumiwa wakati waliomtumia wamenyamaza na muda mwingine wanamfokea kwa kufanya uzembe. sisi wenyewe tunafatwa na makachero wanaotuhoji maswali mengi wakati hata huko mabwepande hatukujui. hatujawahi kumiliki bunduki wala gari. hatujui chochote na hatuna uhusiano na usalama wala polisi. wasicdhanie watabakia milele kwenye madaraka. wataumbuliwa tu siku moja......chanzo, ndugu wa karibu wa bwana msangi
NB
hatuwezi kuweka jinsia au anakoishi huyu mtu kwa usalama wake. Ila familia ya msangi inaishi kwa wasiwasi. Watu wanaosadikiwa kuwa usalama wanajaribu kutafuta ni habari gani wanazozijua (majina ya wakubwa) kuhusiana na utekaji wa Dr. Ulimboka.