Ndugu wa Ahmed Msangi: Maisha yetu Hatarini; Hemedi Katumiwa!

Eti anasema "kwa akili ya kawaida hawezi kwenda kumteka,halafu baadaye aje kumuhoji",nani kasema polisi wa magamba wana akili za kawaida?

Inajulikana kuwa yeye ni mze wa torture,anaweza kutuambia ni akili gani huwa anatumia?

Ujinga huu wa kuingiza kila kitu kwenye siasa, je huu ni uhalifu wa kisiasa,maana naona watu wamegawanyika kivyama...Kama hyo Kim Kardhashian,unahitaji akili ama utafutiwe humu Kanye West wako itakusaidia...
 
Aliyetuma na alieyetumwa are equally guilty. Na hao ndugu na jamaa wa huyo mtekaji, wabadili majina yao yasijulikane kama wana undugu au hata uhusiano na mtekaji, kwani hata mimi nikiwajua, ipo sababu ya kulipiza kisasi nao wakaonja sehemu ya machungu aliyoyapata Dr. na Wale marafiki wa karibu wa huyo jamaa, nawashauri wamkwepe na kumwogopa kama ukoma, kwa kuwa huyo siyo mtu, anakula kwa kumwaga damu ya wasio na hatia. Mtekaji hakuwa na ubinadamu kabisa. Akionekana, auawe kwa kuwa auaye kwa upanga, auawe kwa upanga.
 
Dk. Ulimboka ashindilia serikali



Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 July 2012

DOKTA Steven Ulimboka bado anashikilia kuwa aliyemteka anafanya kazi ikulu, MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa kutoka ubavuni mwa kitanda chake hospitalini anakotibiwa, nchini Afrika Kusini zinasema, ana uhakika na anachosema na hasa sasa wakati hali yake ikiwa inaendelea kuimarika.
Kauli hii ndiyo inafanya dunia nzima itikisike pale serikali ya Rais Jakaya Kikwete inapochelewesha kuunda tume huru ya kuchunguza tukio la kuteka, kutesa na kujaribu kuua Dk. Ulimboka.
Dk. Ulimboka, ambaye hajahojiwa na polisi wa Tanzania juu ya aliowataja, bado anasisitiza kuwa alipokamatwa alikuwa na akili timamu na kwamba walioshona mpango hadi akatekwa anawafahamu fika, zimeeleza taarifa.

Mtoa taarifa amemnukuu Dk. Ulimboka akisema, "…ndugu yangu, hata sasa nawakumbuka."
Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa 26 Juni katika maeneo ya Leaders Club jijini Dar es Salaam; kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno; na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.

Daktari huyo, mwenyekiti wa jumuia ya madaktari Tanzania, aliokolewa asubuhi yake na wasamaria wema karibu na msitu huo, Bunju nje kidogo ya Dar es Salaam.
Taarifa hizi zinakuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS), Jack Zoka ni miongoni mwa waliounda mpango wa kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.

Hata hivyo, tayari Zoka amekana kushiriki njama hizo.
Wakati sakata la Dk. Ulimboka likiwa bado linaining'iniza serikali, mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kauli ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova juu ya aliyeitwa mtu anayeshikiliwa na polisi kwa madai ya kumteka Dk. Ulimboka.

Ijumaa iliyopita, Kova aliwaambia wandishi wa habari kuwa polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kuteka na kutesa Dk. Ulimboka akiwa katika kanisa la Ufufuo alikokwenda kutubu.
Lakini mchungaji Gwajima alitoa tamko Jumapili iliyopita akisema, "Serikali lazima ieleze vizuri. Huyo anayedaiwa kuja kanisani kwetu kutubu ni mgonjwa wa akili. Nawashauri kabla ya kumfanya chochote wampime akili kwanza," alieleza mchungaji huyo mbele ya waamini wake.
"Kwanza huyo mtu hajaja kwetu kutubu. Alikuja kuomba kukutana na mchungaji kiongozi," ameeleza Gwijima na kuongeza, "Lakini tulipomchunguza tukaona ni mgonjwa wa akili. Tukamchukua na kumkabidhi kituo cha polisi Kawe."

Gwijima amesema kama kutubu, basi mtu huyo angetubu huko kwao Kenya na kuhoji, "…kwani kwao Kenya hakuna Mungu?"
Bali katika hali nuyingine ya kustukiza, Kamanda Kova aliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu na kusema polisi hawako tayari kulumbana na viongozi wa dini.
Amesema suala la mtuhumiwa wake, Mulundi tayari liko mahakamani na "halipaswi kujadiliwa." Amesema jambo hili halitakiwi kujadiliwa na kwamba anayetaka taarifa zaidi juu ya mtuhumiwa, aende huko mahakamani siku kesi itakapotajwa.

Kamanda Kova anaonekana kuwa tofauti na rais wake ambaye licha ya kujadili suala lililoko mahakamani juu ya madaktari, alienda mbali hadi kuwafukuza kazi huku wakiwa wamefungwa na ombi la serikali yake mahakamani.
Taarifa kutoka Afrika Kusini zinasema hali ya Dk. Ulimboka inaendelea kutengemaa siku hadi siku.
"Kwa kweli, tunashukuru Mungu…afya yake inaendelea vizuri. Mimi mwenyewe nimeongea naye jana (juzi Jumatatu) na amenieleza afya yake inaendelea vema," ameeleza mmoja wa madaktari jijini Dar es Salaam anayefuatilia kwa karibu matibabu ya daktari huyo.

Amesema, "Madaktari wake wanaendelea na uchunguzi kuhusu figo zake ili waone kama zinaweza kufanya kazi au zinahitaji kuondolewa na kuwekwa nyingine. Lakini kwa jumla, matumaini ya kujumuika na Dk. Ulimboka wiki tatu zijazo ni makubwa mno."
Fuatana na kumbukumbu za Dk. Ulimboka mara baada ya kuokotwa kwenye msitu wa Mabwepande, ambako aliteswa, kutupwa na kuambiwa hakuna atakayeweza kumwokota. Zimechotwa kwenye mtandao wa intaneti wa U-Tube.

Aliyeandaa utekaji na mateso
Nilishawahi kumwona zamani, kwenye mgogoro (wa madaktari) ule mwingine, lakini mara hii alikuwa makini; akinitafuta akisema kwamba anataka kupata maelezo… ili aweze kutoa ushauri…Huyu bwana anafanya kazi ikulu…namfahamu kutokana na matukio ya kwanza…

Alivyoanza kuteswa
Walikuwa wananipiga usoni moja kwa moja, yaani ngumi zinatua usoni; ndo maana wakafanikiwa kunivunja meno. Na haya mengine yamelegea…unaona haya mengine ya chini yamepotea. Wamenipiga sana, nikafika mahali nikawaambia kwa hivi mlivonipiga, ni bora mkaniua.

Hatua za mateso
Wakanifunga miguu…wakakaza ile kamba; mikono yangu ilikuwa imefungiwa mgongoni. Walikaza kamba mpaka nikaona kama huku mikononi kulikuwa kunavimba. Hata miguu wakafunga sana. Basi wakaendesha gari, wakaendesha wakati huu kwa muda mrefu sana. Sikujua wanaenda wapi.

Kipigo na kiminyo
Wanakupiga na vitu vizito, huku wamebana na koleo… Walikuwa wananibana huku kwa mfano kama kuna vitu nakataa kusema. Kwa hiyo wanasema, yaani wewe kwanini husemi. Nikawaambia mimi…? Mpaka unapokubaliana nao wanakuachia.
Lakini kwa kweli mimi sijawahi kupigwa kama nilivopigwa…wala sijawahi kuona mtu anapigwa kiasi kile. Nilipigwa…mpaka unafika mahali unajaribu kuangalia unaona giza. Huoni kilichoko mbele yako, yaani giza. Wakati huku una fahamu zako, huoni.

Walichokuwa wakitaka
…wakati wote kule kwenye gari walikuwa wakisisitiza kuwa wee jamaa umeshatusumbua vya kutosha. Nikawaambia nimewasumbua nini? (Nikasema) …mimi nilikuwa kwenye mazungumzo; sasa kwenye mazungumzo ndo kusaini makubaliano? (Wakasema) …wewe unatakiwa kusaini makubaliano. Sasa makubaliano gani? Mimi sijawahi kukaa mahali nikakataa kusaini makubaliano yoyote. Na hakuna popote eti mimi nilikaa na watu…halafu ikashindikana kukubaliana.

Hali baada ya kipigo
Nakumbuka ilifika mahali nikawa natoka damu mdomoni, natoka damu kichwani; yaani natoka damu karibu kila mahali…
 
Hivi wewe ndiyo unataka tuamini haya? kama ni kweli alishiriki na anahojiwa kuhusu ushiriki wake ulitegemea aseme kwamba ni kweli yeye ndiye aliyemteka na kumtesa Dr. Uli?. Fikiri kidogo!

ndugu yangu, hata wafanyeje, ukweli hautaweza kufichika. hao wauaji lazima watasalimu amri. watapukutika mmoja baada ya mwingine
 
Huyu bwana lazima afe maana ukishindwa operation ya kutesa na kuuwa lazima ufe wewe maana umesababisha ku-leak siri za Serikali, kazi kwake lini afe hatujui ila anasubiri kifo chake.
Hawezi kumsainisha Rais operation ambayo ina-fail yeye na Kova lazima wachukuliwe hatua kali, Kova kazoea hii mara ya pili safari hii imekula kwake.
 
Huyu atakufa tu, bado umma unamsaka kwa udi na uvumba. Pona yake ajiue mwenyewe kabla hajakamatwa.
 
....Alichosema Dkt. Ulimboka nilipozungumza naye, ni kwamba simu moja ilidondoka, nyingine wale watu waliomteka wameichukua pamoja na wallet yake. Hivyo alikuwa ananitajia vitu vilivyopotea. Nilipomuuliza iwapo anakumbuka namba ya simu, aliniambia nikamuulize Dk. Deo. Sasa nashangaa mtu aliyepenyeza uongo huu kwamba alisema mimi ndiye niliyempora hivyo vitu… sielewi ni nani na ana malengo gani....

Duuu hapo kweney red panaonyesha kumbe ishu ya cm na wallet Dr ulimboka alizizungumzia tatizo ni kuwepo kwa stori ya kumdai jamaa daaaaaaaaa..................leteni source nyingi jamani tutajua ukweli sku moja mana hizi movie zina mafunzo yake japo nyingine za kihindi so uvumilie nyimbo zake.
 
Episode 4............
Du mm najua picha ilishafika -: THE END :- labda ni Egoli ambayo mwisho wake hatukuuona, kwani Stearling hauawi, na hao Ndugu waache Uongo huyo jamaa kazi hajaanzia hapo katokea huku Bara kapanda Cheo mpaka kafikia huko. Kwani yeye haitaki kazi au hajui Madhara yake, wako waliopitia huko kina Mrema, Kombe, Kitine sembuse Msangi?
 
Aliyetuma na alieyetumwa are equally guilty. Na hao ndugu na jamaa wa huyo mtekaji, wabadili majina yao yasijulikane kama wana undugu au hata uhusiano na mtekaji, kwani hata mimi nikiwajua, ipo sababu ya kulipiza kisasi nao wakaonja sehemu ya machungu aliyoyapata Dr. na Wale marafiki wa karibu wa huyo jamaa, nawashauri wamkwepe na kumwogopa kama ukoma, kwa kuwa huyo siyo mtu, anakula kwa kumwaga damu ya wasio na hatia. Mtekaji hakuwa na ubinadamu kabisa. Akionekana, auawe kwa kuwa auaye kwa upanga, auawe kwa upanga.
POLE SANA Hemed, my best friend of teenage days, lakini kwa style hii ya maisha katika kutaka mkono uende kinywani..., umenishtua..!
 
Hii ni hearsay his words against msangis.. Hata wakienda mahakamani dr uli akamtaja msangi.. Yeye atakataa atasema ninuongo hakuepo kesi itakaa mahakamani kwa miaka 20 kila mtu anakula bata
 
Hao ndio polisi wa Tanzania wamejifunza kuua na sio kulinda raia na mali zao hawajaanza leo tangu Gen. KOMBE Wale wafanyabiashara wa Mahenge na sasa walitaka kumwondoa Dr.ULIMBOKA lakini Mungu mkubwa wamechemka siri zote muda wa kujulikana umefika na kama serikali imehusika Watanzania wenye mapenzi mema na nchi hii tushirikiane kuiondoa madarakani kwakuwa sifa ya kuongoza nchi hawatakuwa nayo tena subirini tujue nani muhusika mkuu
 
Gazeti la Jamuhuri hadi kuitwa hivyo wajua wamiliki wake itakuwa kama Radio Uhuru!!!! Haya yetu macho pole Msangi na hongera gazeti la Jamuhuri kumsafisha lakini kumbukeni...'a man convinced against his/her will is of the same opinion' habari ndiyo hiyo!
 
Ndugu mmoja (jina kapuni kwa usalama wake), wa karibu wa bwana Ahmed Msangi , askari anayechukiwa kuliko kila askari hapa nchini kwa tuhuma za utekaji na mateso ya Dr. Stephen Ulimboka, amenukuliwa akilalamika kwamba ndugu yao ametolewa kafara na kuyaweka maisha yake hatarini wakati yeye alifanya kazi aliyotumwa na wakubwa.

"Ndugu yetu amechafuka sana jina kiasi kwamba anatembea kwa wasiwasi kila anakokwenda. hamedi hana amani na tunaona kama vile yeye alitumiwa wakati waliomtumia wamenyamaza na muda mwingine wanamfokea kwa kufanya uzembe. Sisi wenyewe tunafatwa na makachero wanaotuhoji maswali mengi wakati hata huko mabwepande hatukujui.

Hatujawahi kumiliki bunduki wala gari. Hatujui chochote na hatuna uhusiano na usalama wala polisi. Wasicdhanie watabakia milele kwenye madaraka. wataumbuliwa tu siku moja......chanzo, ndugu wa karibu wa bwana msangi

NB
Hatuwezi kuweka jinsia au anakoishi huyu mtu kwa usalama wake. Ila familia ya msangi inaishi kwa wasiwasi. Watu wanaosadikiwa kuwa usalama wanajaribu kutafuta ni habari gani wanazozijua (majina ya wakubwa) kuhusiana na utekaji wa Dr. Ulimboka.



Hii story inatakiwa iwe facebook na sio humu JF huu ni Uongo mtupu.
 
Haya ya Dkt. Ulimboka na Msangi sasa yametosha. Ndiyo tuna mpenda Dk. Ulimboka, na kwa kuwa upo hai, ukweli utajulikana tu tusitumie muda mwingi kuweka propaganda za kutunga kila siku.
 
Mimi nadhani hizi story za Dkt. Ulimboka na Msangi sasa zimeishatosha. Naelewa kuwa tuna mpenda sana ndugu yetu Dkt. Ulimboka. Kwa kuwa Mungu amemsaidia upo hai, ni vyema tukafikia mwisho wa hizi thread za kubuni kila siku ili akipona aweze kuelezea ukweli. Huenda huko aliko anaandika kitabu juu ya kilichomtokea sasa tuwe na subiri na kumwombea uponyaji wa haraka.
 
Back
Top Bottom