TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,720
- 10,220
Mke wangu mwezi uliopita aliota ndoto. Ndoto yenyewe ni hii:-
eti alikuwa ameniudhi, kwa hasira nikamwambia utanikoma.
Nikaondoka kwa hasira, niliporudi nikarudi na nyoka mkubwa sana aina ya cobra, akawa ananisihi nisimdhuru na huyo nyoka.
Kwa hasira nikamuwekea huyo nyoka kwenye mkono wake.
Nyoka akawa anamtafuna mkono na hakuwa na mtu wa kumsaidia.
Watu wote walikuwa wakimshangaa, na mwishoni akasaidiwa na shehe mmoja.
Tangu ameota ndoto hiyo upendo umeshuka sana ndani ya nyumba, hamna amani, muda wote ni mnyonge na hana raha kabisa.
Muda wote amekuwa akibubujikwa na machozi na amepoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.
Wapendwa naomba msaada wenu, je nifanye nini ili kurudisha furaha na upendo, pia imani na amani vilivyo potea??
Je hiyo ndoto ina tafsiri au maana gani?
Naamini JF ni kisima cha hekima nitapata msaada wa kutosha kutokana na busara na hekima zenu.