Ugomvi wa Jirani na Mke/Mchepuko wake, Ulivyonigombanisha na Mke wangu

KotelaMamba

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
640
1,011
Wakuu, nimesema mke au mchepuko wa jirani kwasababu sina uhakika kama ni mke wake ama vipi.

Sisi tunaishi eneo moja tulivu sana, eneo moja wapo huku Bunju.
Tunakaribia Miaka Miwili tokea tuhamie.

Tuna jirani yetu, amehamia hana hata Mwezi so hatufahamiani zaidi ya kuonana njiani hasa nyakati za Asubuhi.
Jamaa huwa anampeleka mtoto wake kupanda school bus 🚌, huyo mtoto anaweza kuwa class Four au Three.

Ni kijana mpole sana, kwa mwonekano.

Kutoka kwenye Nyumba yake hadi kwetu ni kama mita 10-15.

Na nafikiri kwenye hiyo nyumba anaishi na huyo mtoto tu, au sijui kwasababu nimewahi kuwaona wao tu na ni asubuhi tu, Tunaokaa Nje ya mji tunaamka mapema sana kukimbizana na foleni, na tunarudi mida imeenda.

Sasa juzi kumetokea varangati ambalo limeleta mtafaruku.
Mida ya Saa Sita kasoro hivi usiku, tulianza kusikia kelele za Mwanamke kama vile anadai kitu, kutokea kwa jirani yetu huyo, zilianza chini chini hivi na baadae zikapanda.

Niliweza kusikia maneno machache na Jamaa akawa anaongea kwa hasira na kwa nguvu.

Wakaanza kutukanana, tusi kubwa ni kuitana Malaya, Jamaa anamwambia huyo Mwanamke wewe ni Malaya tu, yeye anamjibu Malaya ni wewe na baba yako, na maneno mengine mengine wakati huo kama vile kuna kitu wanagombania, inawezekana ni funguo.

Huyo Mwanamke anasisitiza jamaa ampe, mwamba kakaza, sasa sijui alikuwa amemshika kwasababu purukushani zilikuwa kubwa, Jamaa anamwambia atampasua, anamjibu huwezi kunifanya kitu ma.l.aya mkubwa wewe!!.

Hapo wife wangu yuko Dirishani anawasikiliza, mimi niko Kitandani sikutaka kuamka kabisa, gafla yule Mwanamke akapiga yowe moja la juu kabisa, kwa nyumba zilivyo sisi ndio tuko nao karibu kuliko nyumba za majirani wengine. Mabishano yao yalikuwa yamedumu kama dakika 15 hivi

Baada ya lile yowe la mwisho, nikasikia mkurumo wa gari, Wife akaniambia huyo jamaa anaondoka amka ukamzuie au ujue amemfanyia nini huyo Mwanamke, nikashtuka kidogo! Ile natafakari kwenye ile nyumba taa za ndani zikazimwa.

Wife akaniambia kuna mtu, huko ndani ila Kelele za yule Mwanamke na Jamaa hazikusikika tena. Wakati wote huo wife alikuwa anatamani niende nikaamulie huo ugomvi ambao sijui lolote.

Sasa gafla naona wife anachukua mto wake (pillow) anasema anaenda kulala chumba kingine, simply kwasababu nilishindwa kutoka na kuanza kunilaumu kwa mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu, ananiambia sina msaada wowote ule.

Wakuu kosa langu hapo ni lipi?

Unawezaje kuingilia ugomvi ambao hujui ulikotokea?

Naambiwa nina roho mbaya, kisa sikwenda na mimi dirishani kujaribu kuangalia kinachoendelea.

Ndoa ina miaka 6 hii ila bado sijamfahamu vizuri huyu wife wangu...Nahisi ana vichembe chembe vya u feminist.
 
Wakuu, nimesema mke au mchepuko wa jirani kwasababu sina uhakika kama ni mke wake ama vipi.

Sisi tunaishi eneo moja tulivu sana, eneo moja wapo huku Bunju...
Mnawatoaga wapi wanawake waropokaji?

Kwenye suala la mahusiano, mwanamke mwenye mdomo usio na breki kwangu hanaga nafasi.

Kusaidia majirani ni kuzuri lkn usiwe peke yako unaweza kuchomwa kisu ukawaacha wao wanakulana
 
Sikatai, nafikiri sikuwa na haja ya kuingilia kwa wakati ule.

Ungefanya chochote, hata ku simpasize ba Mwanamke, yani kweli unasikia ugomvi, nyumba kimya, mtu anatoka na gari usifanye kitu?

Hata kupiga simu police, labda kutoka nje sio busara, kaa na mwanamke onyesha concern naye, fanya jambo fulani, mke ni kumpety pety tu.

Amekuona tu u cant protect a Woman, ans probably u can't protect her, mimi siwezi kulala kabisa na kamwe nikisikia hizo sauti za mwanamke akipigwa.

Talk to your wife, admit a mistake in a way, and rudisha atmosphere nzuri, ume act like a boy, and not a Man, if she is worried, handle her, mbona ni rahisi sana, sio jambo dogo wala ulilofanya, ujawajibika.
 
Mnawatoaga wapi wanawake waropokaji?
Kwenye suala la mahusiano, mwanamke mwenye mdomo usio na breki kwangu hanaga nafasi.
Kusaidia majirani ni kuzuri lkn usiwe peke yako unaweza kuchomwa kisu ukawaacha wao wanakulana
Bora hata tungekuwa tunafahamiana.

Huku Dar inachukua muda sana ku catch up na Majirani, hasa kwa watu ambao pilika ni za kila siku.
 
Domestic violence ni suala tata sana. Ni kama wakati mwingine watu wanakuwa wanaigizq. Watapigishana makelele na kulia. Kesho wako pamoja vizuri wanacheka. Wewe uliyeenda kuamulia kwa nguvu unaonekana mnoko.

Si mambo ya kuingilia kabisa.
Si mchezo kuna kipindi niliwahi ingilia ugomvi tena ulikuwa Mwanamke na Mwanamke, ile kesi ilitafsiriwa vibaya mno.

Ikaonekana walikuwa wanapigana kwa sababu yangu ilihali siwafahamu kabisa yani.
Niliwakuta tu njiani wanadundana.
 
Back
Top Bottom