Ndoto ya mke wangu imepunguza upendo na amani kwenye nyumba yetu

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,661
9,981
Mke wangu mwezi uliopita aliota ndoto. Ndoto yenyewe ni hii:-

eti alikuwa ameniudhi, kwa hasira nikamwambia utanikoma.
Nikaondoka kwa hasira, niliporudi nikarudi na nyoka mkubwa sana aina ya cobra, akawa ananisihi nisimdhuru na huyo nyoka.
Kwa hasira nikamuwekea huyo nyoka kwenye mkono wake.

Nyoka akawa anamtafuna mkono na hakuwa na mtu wa kumsaidia.
Watu wote walikuwa wakimshangaa, na mwishoni akasaidiwa na shehe mmoja.

Tangu ameota ndoto hiyo upendo umeshuka sana ndani ya nyumba, hamna amani, muda wote ni mnyonge na hana raha kabisa.
Muda wote amekuwa akibubujikwa na machozi na amepoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.

Wapendwa naomba msaada wenu, je nifanye nini ili kurudisha furaha na upendo, pia imani na amani vilivyo potea??
Je hiyo ndoto ina tafsiri au maana gani?

Naamini JF ni kisima cha hekima nitapata msaada wa kutosha kutokana na busara na hekima zenu.
 
huwa sijishughulishi kutafsiri ndoto, muhimu ni kufanya maombi kwa imani zenu. mumkemee shetani na kuharibu nguvu zake, na kurudisha uwepo wa Mungu kati yenu. mnaweza kuongea na kiongozi wenu wa dini pia kwa sala na ushauri,
pole sana

Pole sana sikutegemea kama ndoto zinaweza kuwa na athari kubwa namna hii. Nadhani ushauri aliokupa King'asti ni mzuri sana hivyo ufanyie kazi labda utarudisha hali ya hapo nyumbani kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya ndoto hiyo.
 
Kwa elimu yangu ya Ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni Mkubwa ni dalili ya kuwa Mke wako ana Pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo Shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani Mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa Mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni Muislam mpelkee kwa Sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.
 
kwa elimu yangu ya ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni mkubwa ni dalili ya kuwa mke wako ana pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni muislam mpelkee kwa sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.
mmmhhh???
 
pepo hilo mkuu! Kemeeni katika jina la imani yenu kaka!!!
 
Kimsingi mimi ninachifahamu ndoto ni ndoto na kwa kawaida ni reflection ya mambo au mawazo yaliyofanyika mchana uliopita. Ungejitahidi kumuelewesha mkeo kuwa hiyo ni ndoto tu na kamwe haina uhusiano na tukio lolote la kweli.
Ukiona hali inaendelea nenda kwa viongozi wa dini wakusaidie.
 
naanini kuna ndoto zina maana japom si kila ndoto ina maana, mwotaji hujua ndoto yenye maana kutokana na kuzongwa na ndoto hiyo.

Kikubwa zaidi ya ndoto hizo ni maombi.
 
Kwa elimu yangu ya Ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni Mkubwa ni dalili ya kuwa Mke wako ana Pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo Shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani Mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa Mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni Muislam mpelkee kwa Sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.
Duuuuu!!!!!!!!
 
Mmmmh!ana haki ya kuogopa mie mwenyewe tu kwa kusoma nimeogopa mpaka nimetizama pande zote za hapa ofcn km kuna kitu!
Nawashauri uende mkaombewe na kumkemea huyo pepo,
Na muwe na utaratibu wa kufanya ibada fupi na kusali kabla ya kulala!
 
huwa tunasali kila siku kabla ya kulala, lakini mwenzangu tangu aote ndoto hiyo hataki hata kusali na mimi.
 
Mke wangu mwezi uliopita aliota ndoto. Ndoto yenyewe ni hii:-
eti alikuwa ameniudhi, kwa hasira nikamwambia utanikoma.
Nikaondoka kwa hasira, niliporudi nikarudi na nyoka mkubwa sana aina ya cobra, akawa ananisihi nisimdhuru na huyo nyoka.
Kwa hasira nikamuwekea huyo nyoka kwenye mkono wake.
Nyoka akawa anamtafuna mkono na hakuwa na mtu wa kumsaidia.
Watu wote walikuwa wakimshangaa, na mwishoni akasaidiwa na shehe mmoja.
Tangu ameota ndoto hiyo upendo umeshuka sana ndani ya nyumba, hamna amani, muda wote ni mnyonge na hana raha kabisa.
Muda wote amekuwa akibubujikwa na machozi na amepoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.
Wapendwa naomba msaada wenu, je nifanye nini ili kurudisha furaha na upendo, pia imani na amani vilivyo potea??
Je hiyo ndoto ina tafsiri au maana gani?
Naamini JF ni kisima cha hekima nitapata msaada wa kutosha kutokana na busara na hekima zennu.

usimwadithie mtu ndoto yako ni hatari..by M Mpoto
 
Mkuu, kwa upeo wangu wa kiimani, huyo ni pepo. Tafuta mchungaji wa ukweli mkaombewe kisha na nyie msimame katika neno.

Mapepo huwa yanajiinua kwa njia nyingi. Kuna kitu kinaitwa affliction. Unaweza ukaota kakayo au mamayo au mtu yeyote unayemfahamu anakufanyia kitu kibaya. Ukamchukia na kumsema kuwa ni mchawi. Kumbe ni wachawi wanatumia sura ya huyo mtu katika kukutorment.

Sali Zaburi ya 91 kila siku kabla ya kulala. Ni Zaburi ya ulinzi. Barikiwa sana
 
Ndoto ni reflection ya maisha ya mtu,sometimes huwa kama inakutaadharisha na jambo lijalo. Lakini pia huwa ni reflection ya yale uyawazayo. Vyovyote ilivyo tunashauriwa unapoota ndoto mbaya kemea imediately na uombe MUNGU akuepushie.
 
Mkuu, kwa upeo wangu wa kiimani, huyo ni pepo. Tafuta mchungaji wa ukweli mkaombewe kisha na nyie msimame katika neno.

Mapepo huwa yanajiinua kwa njia nyingi. Kuna kitu kinaitwa affliction. Unaweza ukaota kakayo au mamayo au mtu yeyote unayemfahamu anakufanyia kitu kibaya. Ukamchukia na kumsema kuwa ni mchawi. Kumbe ni wachawi wanatumia sura ya huyo mtu katika kukutorment.

Sali Zaburi ya 91 kila siku kabla ya kulala. Ni Zaburi ya ulinzi. Barikiwa sana

asante sana kwa ushauri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom