Ndoa zetu na umiliki wa mali...kizungumkuti kingine!!

Dark City;1904123]Ndugu yangu...bado naamini ndoa inahitaji makubaliano hata kama ni yale ambayo mnakubaliana kutokubaliana. Kukaa kimya ni hatari sana na pia kumzunguka mwenzio na kujitengenezea jinai moyoni. Nashauri watu wachukue hatua za kisheria katika mambo kama hiyo ili kupunguza risk za heart attack.

Mke au mume ambaye ni unrealistic katika matumizi (kama huyo anayejipamba dhahabu na kuishi nyumba ya kupanga) anatakiwa kuchukuliwa kama wagonjwa wengine na kudeal naye kwa mujibu wa sheria. Am I being too harsh???

Napendekeza tuwe na entrepreneurship marriage with everything on the papers na especially kama wanandoa wote wana uwezo wa kumiliki tangible assets. Hili haliwezekani?

Mkuu wewe umeshayafanyia kazi haya unayosema hapa au ni nadhalia tu? Tatizo litaonekana kuwa mtu yupo kimaslahi zaidi kama akipropose hii mada kwa mwenzi wake. Inaweza kuleta doa kwa mwenzi wako kama mada usipo-ipresent kwa umakini mezani. Ni muhimu lakini je itachukuliwaje na mwenzi wako?

Mengi ninayoyasema nayaishi. Ukihitaji ushahidi tuwasiliane.
 
Mnh, Nyamayao...kuna kitu sijakielewa hapa.
'Mfano;' Mumeo mtapokubaliana ajenge nyumba kwenye kiwanja chako kwa ajili wa watoto wenu, ni ujinga?
Ni alama gani za wakati anapaswa kuzisoma kwenye hili? ...DC msaada please. Sijawaelewa hapa.

Mbu,

Naomba kwanza tuwekane sawa. Mali ya mume au mke aliyochuma kabla ya ndoa haitahesabiwa kuwa matrimonial property kama endapo watakubaliana kwa maandishi kabla ya ndoa. Kwa maana hiyp hicho kiwanja cha dada ulichokiongelea kilikuwa ni mali ya ndoa na hakutakiwa kukiuza bila kumshirikisha mume wake.

Suala la mume kujenga kwenye kiwanja cha mke wake nadhani siyo tatizo. Ila ilibidi wakubaliane kabla ili ownership ya hicho kiwanza ileweke. Kwa hiyo kitendo cha huyo dada kukiuza ni hatari kwani wakienda mbele ya sheria kunaweza kuwa na mgogoro mkubwa ambao lazima utajeruhi ndoa yao.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Dark City;Asante Michelle kwa mchango wako. Sina hakika lakini nadhani sheria ya ndoa haiwatambui watoto kama warithi wa mali ya ndoa endapo hakuna wosia. Kwa hiyo kuandika majina ya watoto siyo suluhisho. Bado napendekeza kwanza tujitahidi kuelewa nini kinahusika kama mali za ndoa kwa mujibu wa sheria. Pili tujadiliane na wenzetu. Hakuna njia ya mkato!

Pia nawaonea huruma wanaume wanaojidai kuficha. Endapo Mke akitoa ushahidi kuwa hizo mali zilipatikana kwenye ndoa hata kama ziko sayari nyingine zitapigwa panga 50% by 50%. Kwa hiyo wanawake wajitahidi kufuatialia na kupata nyalaka za mali ambazo waume zao wanajidai kuficha. Hiyo ndiyo dawa yao watu wa namna hiyo!!.

Siyo kwa wanaume wenye kuficha mali zao, hata wanawake wanafanya mambo kama hayo. Tatizo hizo documents za mali zilizofichika utazipata wapi? Mtu akiamua kuficha hata hizo docs kuzipata ni kazi zaidi tu ya kusikia kwa watu

Pia na wewe ukiamua kufuatilia lazima utaweza ku-uncover zaidi ya 75% ambavyo mwenzio anakuficha. Hiyo si haba!
 
Mnh, Nyamayao...kuna kitu sijakielewa hapa.
'Mfano;' Mumeo mtapokubaliana ajenge nyumba kwenye kiwanja chako kwa ajili wa watoto wenu, ni ujinga?
Ni alama gani za wakati anapaswa kuzisoma kwenye hili? ...DC msaada please. Sijawaelewa hapa.

sana...mnatakiwa muanze na vyenu vya ndoa vya kubangaiza, tulivyokuwa navyo kabla ya kukutana tuviache vilivyo mpaka tutakapoona sasa tunaweza kujenga kwenye chako coz tayari tuna chetu, hata mie angejenga kwenye changu then akaniletea za kuleta huko mbeleni ningefanya kama huyo dada uliyemzungumzia...
 
Labda kama nakosea....Endapo hamkuweka makubaliano, mali mlizokuwa nazo kabla ya ndoa automatically zinakuwa za ndoa na mnazimiliki kwa 50 % @. Kwa maana hiyo hata ukifanya kama huyo dada ni kujidanganya tu. Ni ubabe ambao hauna misingi ya makubaliano ya kisheri. Kama nimekosea wanasheria watasahihisha!
 
cjui kama mie ndio nakosea lakini kwangu mimi tulivyokuwa navyo tuliviacha vilivyo tukaanza vyetu moja, na hata kama vipi nicngependa ajenge/nijenge kwenye kiamba chake, na hapa unamaanisha makubaliano ya kisheria? au mie sieleweki jamani sio kwamba ctambui/atambui kama nina hiki/na kile lakini ki2 kama pesa zinazotokana na tulivyokuwa navyo kabla vinamhusu mhucka mwenyewe.....
 
Mbu,

Naomba kwanza tuwekane sawa. Mali ya mume au mke aliyochuma kabla ya ndoa haitahesabiwa kuwa matrimonial property kama endapo watakubaliana kwa maandishi kabla ya ndoa. Kwa maana hiyp hicho kiwanja cha dada ulichokiongelea kilikuwa ni mali ya ndoa na hakutakiwa kukiuza bila kumshirikisha mume wake.

Suala la mume kujenga kwenye kiwanja cha mke wake nadhani siyo tatizo. Ila ilibidi wakubaliane kabla ili ownership ya hicho kiwanza ileweke. Kwa hiyo kitendo cha huyo dada kukiuza ni hatari kwani wakienda mbele ya sheria kunaweza kuwa na mgogoro mkubwa ambao lazima utajeruhi ndoa yao.

sana...mnatakiwa muanze na vyenu vya ndoa vya kubangaiza, tulivyokuwa navyo kabla ya kukutana tuviache vilivyo mpaka tutakapoona sasa tunaweza kujenga kwenye chako coz tayari tuna chetu, hata mie angejenga kwenye changu then akaniletea za kuleta huko mbeleni ningefanya kama huyo dada uliyemzungumzia...

...ok,...nimepata mitizamo miwili tofauti yenye muelekeo mmoja.
pre-nuptials ni muhimu sana, si jambo la kupuuzwa hata kidogo.
 
Wapendwa hongereni kwa mada nzuri,

Kwa mawazo yangu mimi, kwa kweli kama unampenda huyo ambaye umekubali kuishi naye mpaka kifo kiwatenganishe, sidhani kama itakuwa shida kumweleza mali zako zote na pia kuzimiliki kwa pamoja hata zile ambazo kila mmoja alikuwa nazo kabla hamjakutana. Ukiwepo upendo wa kweli, hakuna mashaka tena kati yenu.

Tatizo la ndoa nyingi, watu wanaingia kwa malengo fulani fulani hivi, hakuna upendo wa dhati, na hii inasababisha kutokuaminiana hata katika swala la umiliki za mali walizonazo.

Mbarikiwe!
 
sana...mnatakiwa muanze na vyenu vya ndoa vya kubangaiza, tulivyokuwa navyo kabla ya kukutana tuviache vilivyo mpaka tutakapoona sasa tunaweza kujenga kwenye chako coz tayari tuna chetu, hata mie angejenga kwenye changu then akaniletea za kuleta huko mbeleni ningefanya kama huyo dada uliyemzungumzia...

nyamayao nadhani uko sahihi kwa sababu kama kisheria mali zinazotambulika kama za pamoja ni zile zilizopatikana wakati mko pamoja basi sidhani kama ni sahihi kuhesabu mali ya mwenzako ambayo ulimkuta nayo kabla kama ya kwako. UNLESS kuna makubaliano KISHERIA au KIMAANDISHI kuwa mnakubali kudeclaire kuwa ni za pamoja kwa sababu maisha hayatabiriki, hata kama si ninyi wawili but lolote lawezatokea na hali huwa mbaya kama hakuna wosia wa kimaandishi juu ya mali hizo. Makubaliano ya mdomo tu hayatoshi ndo kama ya huyo ndugu yake kaka Mbu.

Ingawaje nafikiri wengi wetu huwa tunafungwa kwa upofu wa mapenzi na trust kuwa kwa mimi kushare naye pasipo makubaliano yoyote ni mapenzi but mapenzi ya siku hizi hayatabiriki bana. So kama mnakubaliana kiwanja alichonunua nyamayao wakati anasoma kijengewe nyumba ya kuishi na msukuma wake ni wazi inatakiwa iwe makubaliano ya kisheria au kimaandishi ambayo baadae mnaweza hata badilisha umiliki na kuwa wa familia kama ikibidi ingawa nayo ina madhara yake hasa kwa wale wanawake wasiojua sheria kwani siku baba akivuta kama ndugu ndo kama mie hawakawii kumpokonya au dhulumu maana itakuwa inahesabika kuwa ilichumbwa na kaka yao na itachukua muda sana kwa mmama kujieleza akaeleweka juu ya transfer iliyofanywa.

Labda kama nakosea....Endapo hamkuweka makubaliano, mali mlizokuwa nazo kabla ya ndoa automatically zinakuwa za ndoa na mnazimiliki kwa 50 % @. Kwa maana hiyo hata ukifanya kama huyo dada ni kujidanganya tu. Ni ubabe ambao hauna misingi ya makubaliano ya kisheri. Kama nimekosea wanasheria watasahihisha!

kusema ukweli makubaliano yenye ushahidi ni muhimu.......siku hizi nimejenga utaratibu wa kutoamini makubaliano ya sauti tu hapana .......... kuna rafiki yangu alipoolewa alimkuta mumewe ameshaanza kujenga nyumba msingi umesimama ingawa ujenzi ulikuwa unakwenda so slow......after ndoa shost akasema bwana mie nimechoka kuishi nyumba za kupanga bwana hebu tufunge mikanda tumalizie kibanda kule (nadhani hakukuwa na makubaliano yoyote ya umiliki) but mdada akachakarika akapata mkopo Benk mkubwa tu.....akasogeza mpaka kufikia hatua ya kuweza kuishi yaani ni vile Mr wake alikuwa anakataa kuingia kule ikiwa katika hali ile yaani bila finishing kama tiles na taa za getini!! (eti wenzie watamcheka!! na kila siku yuko juu ya kistuli!! anajenga heshima Bar!!)..... mdada akawa mpole anasubiri Mr.................aende China kuleta vifaa vya kumalizia urembo.

jamaa kenda China na Sweden kaleta vya kumalizia............ house warming party ilifanyika panoja na engagement party kwa mwanamke mwingine!! shost analia hadi leo............hakuwa anaweka risiti wala nini kuonyesha mchango wake. Ndo imetoka hiyo.
 
MJ1.....nieleweshe kidogo mae......cjakupata hapo, ina maana huyu kaka alioa mara ya pili tena?...mie ndio mambo cyataki hayo yakupeana wehu...
 
MJ1.....nieleweshe kidogo mae......cjakupata hapo, ina maana huyu kaka alioa mara ya pili tena?...mie ndio mambo cyataki hayo yakupeana wehu...
nyamayao tunajifunza mengi kweli dada yangu.......yes alioa tena dini yake ilimruhusu ingawa ndoa ya kwanza alioa bomani na akatiki pale paliposema ndoa ya mke mmoja kwenye cheti cha ndoa. Halafu kichekesho akasema ameamua kuoa kidini ili amrudie mungu wake amechoka kuishi maisha ya zina!!
 
Mzee DC asante kwa mada nzuri...naona umeanzisha hisia za watu kweli kweli!!
Kusema ukweli swala la kuandika urithi ni muhimu sana!Kama hutaki mkeo na wanao wasinyanyaswe na ndugu...wanao wa mama mwingine wasinyanyaswe na mke....wanao wa nje wasisahaulike....ndugu na familia yako wasinyanyaswe na mke andika urithi.Kina mama nao kama hutaki jasho lako lije kumilikiwa na mama wakambo ambae atawahesabia wanao slice za mikate asubuhi andika urithi na nani ungependa awe karibu na wanao zaidi ya baba yao!!

Nimeona mahali mmeongelea usiri wa yanayohusu urithi ila binafsi sioni tatizo lake.Zaidi ya kwamba kama kuna wenye tamaa waonaweza kukutanguliza kwa muumba kabla ya muda wako hamna ubaya wowote!!Actually ni nzuri kwa kiasi flani ikiwa familia ina mchanganyiko wa watoto kutoka kwa mama au baba tofauti!!!Nyumbani tunayo hiyo...na tunajua mzee amemwachia mkewe asilimia 30 ya kila kitu na inayobaki inagawanywa kwa watoto!!!Vitu kama hivi visipojulikana mwanamama anaweza akasababisha karatasi za urithi zisipatikane yeye apate 50% alafu watoto nao 50%....kitu ambacho kitafanya wale wasio wake wapunjike!!
Jali...andika urithi!
 
Naomba nijibu kwa ujumla na haraka haraka kabla kibarua hakijaota mbawa,.....LOL!!!

Kwanza, mapenzi ni dynamic...kwa hiyo tuache kujidanganya na ndoto za kwamba tunapenda/kupendwa sana kiasi kwamba nothing will happen tomorrow. Gharama ya kuweka vitu sawa kisheria ni ndogo kuliko kutoweka kabisa...Mbona tunakata insurance kila siku?

Nitajaribu kuomba wanasheria wanisaidie...Ila bado naamini mali mlizochuma kabla ya ndoa automatically zinakuwa shared kama hamkuweka maandiko sawa. Nadhani sheria inasema hivyo. You need to declare what should be or should not be counted as matrimonial properties kabla na wakati mko kwenye ndoa. Vinginevyo imekula kwako!

MJ1...Mambo ya kuoa au kutooa hayafuta haki za huyo dada. Mwambie tuwasiliane nimuunganishe na wataalamu. Ushahidi wa kwamba mali ni yao ya ndoa na huyo mke mwingine hana haki ya kuifaidi ni rahisi sana kuupata. I am sure hajachelewa.

Katika haya mambo tunahitaji kupeana si ujuzi tu bali na moyo wa ujasiri. But above all, we should stop to take things for granted.

Mzee DC.
 
nyamayao tunajifunza mengi kweli dada yangu.......yes alioa tena dini yake ilimruhusu ingawa ndoa ya kwanza alioa bomani na akatiki pale paliposema ndoa ya mke mmoja kwenye cheti cha ndoa. Halafu kichekesho akasema ameamua kuoa kidini ili amrudie mungu wake amechoka kuishi maisha ya zina!!

mhh...wacha tu nibakie na hofu yangu kwa kweli...ndio nn hiki jamani?
 
Naomba nijibu kwa ujumla na haraka haraka kabla kibarua hakijaota mbawa,.....LOL!!!

Kwanza, mapenzi ni dynamic...kwa hiyo tuache kujidanganya na ndoto za kwamba tunapenda/kupendwa sana kiasi kwamba nothing will happen tomorrow.
Gharama ya kuweka vitu sawa kisheria ni ndogo kuliko kutoweka kabisa...Mbona tunakata insurance kila siku?

Nitajaribu kuomba wanasheria wanisaidie...Ila bado naamini mali mlizochuma kabla ya ndoa automatically zinakuwa shared kama hamkuweka maandiko sawa. Nadhani sheria inasema hivyo. You need to declare what should be or should not be counted as matrimonial properties kabla na wakati mko kwenye ndoa. Vinginevyo imekula kwako!

MJ1...Mambo ya kuoa au kutooa hayafuta haki za huyo dada. Mwambie tuwasiliane nimuunganishe na wataalamu. Ushahidi wa kwamba mali ni yao ya ndoa na huyo mke mwingine hana haki ya kuifaidi ni rahisi sana kuupata. I am sure hajachelewa.

Katika haya mambo tunahitaji kupeana si ujuzi tu bali na moyo wa ujasiri. But above all, we should stop to take things for granted.

Mzee DC.

kaka hapo umenimaliza...umefunga kazi kabisa kabisa!
 
kuna tatizo jingine kwa wake wanaofanya kazi. hawa mali zao huzielekeza kwao na zile za mume ndiyo zinaonekana za familia! kama mume ni ***** fulani atakuwa anatumika bila yeue kujua. hata matumizi ya nyumbani utakuta kila jambo linaelekezwa kwa baba.mbaya zaidi mambo haya yanafanywa na wanawake wasomi ambao bado wametawaliwa na mfumo jike. kwa hiyo wanaume waangalifu wanakwepa kuweka taarifa zao za mapato na matumizi hadharani
 
.

Ukiona hivyo ujue wote ni wapuuzi. Siwezi kutoa gharama 100% wakati mama naye anfanyakazi. Mshahara wangu wote na kila senti yangu Mama anaijua na pia ni muhimu (ingawa si lazima nijue zake). Ila akianza kulete upuuzi eg. kununua gold za 1.5mil wakati tuna shida ya karo ni lazima tugawane majukumu. Siyo lazima kuweka wazi kila senti ila mkiweza inapendeza sana. Kitu cha msingi ni kuhakikisha kuwa wanandoa wana makubaliano...written or verbal but wakubaliane jinsi ya kuishi. Kuacha mambo yajiendeshe yenyewe ni kuwa irresponsible!!
 
...lol! ...mstaafu, 'nahisi' hapo kwenye red pamekuponza ndio maana hujapewa 'LIKES' ..he he...
nakuunga mkono mia kwa mia kwa kauli hiyo. Potelea mbali lawama za Ooohh, "wewe ni mwanaume ni jukumu lako kunitunza." Crap!
 
CRAP in Deed
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
.

Ukiona hivyo ujue wote ni wapuuzi. Siwezi kutoa gharama 100% wakati mama naye anafanyakazi. Mshahara wangu wote na kila senti yangu Mama anaijua na pia ni muhimu (ingawa si lazima nijue zake). Ila akianza kulete upuuzi eg. kununua gold za 1.5mil wakati tuna shida ya karo ni lazima tugawane majukumu. Siyo lazima kuweka wazi kila senti ila mkiweza inapendeza sana. Kitu cha msingi ni kuhakikisha kuwa wanandoa wana makubaliano...written or verbal but wakubaliane jinsi ya kuishi. Kuacha mambo yajiendeshe yenyewe ni kuwa irresponsible!!

...lol! ...mstaafu, 'nahisi' hapo kwenye red pamekuponza ndio maana hujapewa 'LIKES' ..he he...
nakuunga mkono mia kwa mia kwa kauli hiyo. Potelea mbali lawama za Ooohh, "wewe ni mwanaume ni jukumu lako kunitunza." Crap!

Yaani nyie wawili mnanifurahisha sana I just wish kungekuwia na uwezekano wa kufanya Husbunds ' Swap.....then mkirudi makwenu wake zenu wawajulishe maisha wanayoishi wanaume wenzenu wengine ..............

Babu DC.....inakuwaje pale ambapo upuuzi huo unafanywa na mwanaume....wote mwafanya kazi ila anataka uaccount every single cent of your salary tena kwa nguvu huku wa kwakek hataki kuaccount?? ........tena anakuachia majukumu yote ya ndani uyatimize wewe simply becouse anaishi kwkenye nyumba ambayo inahesabika ni ya kwako kwa kuwa umepangishiwa na ofisi?? and then hapo hapo kwenye kuaccount anakupiga tumizinga twa kati kati ya mwezi twa mafuta na vocha..............huyu unamweka wapi??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom