Ndoa zetu na umiliki wa mali...kizungumkuti kingine!!

Yaani nyie wawili mnanifurahisha sana I just wish kungekuwia na uwezekano wa kufanya Husbunds ' Swap.....then mkirudi makwenu wake zenu wawajulishe maisha wanayoishi wanaume wenzenu wengine ..............

Babu DC.....inakuwaje pale ambapo upuuzi huo unafanywa na mwanaume....wote mwafanya kazi ila anataka uaccount every single cent of your salary tena kwa nguvu huku wa kwakek hataki kuaccount?? ........tena anakuachia majukumu yote ya ndani uyatimize wewe simply becouse anaishi kwkenye nyumba ambayo inahesabika ni ya kwako kwa kuwa umepangishiwa na ofisi?? and then hapo hapo kwenye kuaccount anakupiga tumizinga twa kati kati ya mwezi twa mafuta na vocha..............huyu unamweka wapi??

khee?! huyo naye vipi tena?
 
...lol! ...mstaafu, 'nahisi' hapo kwenye red pamekuponza ndio maana hujapewa 'LIKES' ..he he...
nakuunga mkono mia kwa mia kwa kauli hiyo. Potelea mbali lawama za Ooohh, "wewe ni mwanaume ni jukumu lako kunitunza." Crap!

Mkuu Mbu,

Nafurahi sana kuona kwamba una watu bado wanapenda kujadili issues. Naomba nisema hivi,.....Gharama ya kuacha mambo yaende kwa kudra za mwenyezi Mungu ni kubwa sana kiasi kwamba hatuwezi hata kuthubutu kuzi-quantify....LOL... Nashauri watu wakae chini wakubaliane wanataka kuishi vipi hata kama majirani wataona ni vichaa. It's their lives and they have to set up a good foundation for their best destiny...Mbali ya hayo ni kukaribisha matatizo...just to buy troubles!!

Kwa sababu hiyo sitajisikia vibaya mkuu Mbu kama watu wakinipa dislikes kwa kuyawake wazi haya mambo..Mwisho wa siku wao wenyewe ama watabeba hizo likes na kuniletea nyumbani au watatuma kwa posta!!

Mzee DC.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Yaani nyie wawili mnanifurahisha sana I just wish kungekuwia na uwezekano wa kufanya Husbunds ' Swap.....then mkirudi makwenu wake zenu wawajulishe maisha wanayoishi wanaume wenzenu wengine ..............

Babu DC.....inakuwaje pale ambapo upuuzi huo unafanywa na mwanaume....wote mwafanya kazi ila anataka uaccount every single cent of your salary tena kwa nguvu huku wa kwakek hataki kuaccount?? ........tena anakuachia majukumu yote ya ndani uyatimize wewe simply becouse anaishi kwkenye nyumba ambayo inahesabika ni ya kwako kwa kuwa umepangishiwa na ofisi?? and then hapo hapo kwenye kuaccount anakupiga tumizinga twa kati kati ya mwezi twa mafuta na vocha..............huyu unamweka wapi??

MJ1...Mpuuzi ni mpuuzi bila kujali ni HE au SHE...Katika mazingira ya namna hiyo huyo mwanamume hana tofauti na display toys wanazotumia kuonesha mavazi kwenye boutique/maduka!
 
Nimeona nami nichangie kidogo katika mjadala huu. Migogoro ndani ya ndoa hasa kuhusiana na mambo ya mali ni very complicated (kwa maoni yangu lakini).

Mimi nimeoa lakini mwenzangu simuelewi, alikuwa akifanya kazi mikoani mie nikiishi Dar. Sasa nikimwambia tujipange ili tufanye kitu cha maana mfano kujenga nyumba alikataa kabisa kwa madai kuwa anaweza kuchangia halafu nikaoa mwanamke mwingine.

Hata baada ya kufanikisha kumhamishia Dar nilimweleza tena tujipange kwa pamoja tujenge nyumba na kufungua miradi mingine lakini bado tena alikataa kwa madai kuwa yawezekana watu wengine (hasa ndugu wa upande wangu) pia wakafaidi - hapo hajui kama naye ana ndugu wanaoweza kufaidi BALI ADUI ni ndugu zangu. Kwa hiyo nimeamua kujipanga mwenyewe kwa jinsi nitakavyoona na kuweza.

Nilimsomesha kozi ya Certificate UDSM nikiwa na lengo la kumwendeleza hadi Diploma na baadaye Degree lakini wakati akisoma akawa anadai namnyanyasa kwa kuwa hajasoma - baada ya kumaliza kozi niligaili kumwendeleza Diploma baada ya kuona kumbe anasoma ili asinyanyaswe na siyo kwa maendeleo yetu.

Pia kuna suala la watoto, tukikorofishana kidogo tu anakataza watoto wasiwe karibu nami yaani tusiongee na anatishia kujitenga na kusema hata tukitengana sitapata watoto (yaani watoto ni mali yake binafsi).

Sipingi suala la kuandika wosia lakini kwa mazingira haya akinitamkia mambo ya kuandika wosia nitamhisi vipi? Naombeni mchango wenu. KUNA MDAU MMOJA AMEELEZEA HOJA YA MKE KUANZISHA MADA YA KUANDIKA WOSIA KWA MUMEWE
 
Kuna mchangiaji aliyesema kuwa mali kabla ya ndoa haiingizwi kwenye mirathi, mbona mie nahisi mtafaruku zaidi? Kwa hiyo kama kabla ya ndoa nilifanikiwa kujenga nyumba na baada ya ndoa sikujenga tena, hii inakuwa imekaaje? Manake kwa mtazamo wangu, ina maana zile za kabla ya ndoa zinaweza kuachwa kwa mtu yeyote kwa utashi wa mwenye mali. Sasa kama ndoa ina watoto si wanaweza kuathirika kwa maamuzi yetu? Manake kila mtu anavyopenda kuvutia kwake, si ajabu hizo za kabla ya ndoa zikaachwa kwa ndugu wa upande wa mmiliki wa mali hizo!

Hapa nafikiri zinaweza kutumika busara zaidi za wanandoa, kuhusu mali iliyochumwa kabla ya ndoa. Ila kama kila mtu kakomaza sura akiona uchungu wa mali zake, ndio tunarudi kule kuleeeee.....
 
mhh...wacha tu nibakie na hofu yangu kwa kweli...ndio nn hiki jamani?

Na hii hofu si ndio inatuongezea maradhi tena jamani? Tuite maisha hayatabiriki au ni nini hiki tena? Yaani...daah hata la kusema sina. Najiona kabisa ndotoni nikiitupia kiberiti hiyo nyumba!
 
Wamoja,

Maisha ya ndoa ni complex..wakati wengine wanafurahi na kutoa vicheko kila dakika, kuna wengine wanamwaga machozi kila sekunde. Ila yote ni maisha na tuko kwenye dunia moja. Nitapenda kuchangia zaidi kuhusu issue yako ila mengi tumeshayasema huko nyuma. Jitahidi kutafuta muda upitie kila kitu tulichoandika na kama bado unadukuduku tunaweza kuendelea hapa hapa au kwa PM. Issue yako ni kubwa ila inaweza kuwa simple sana ukijitahidi kuelewa jinsi mambo yanavyotakiwa kwenda katika mtazamo wa sheria.. Tutaendelea tena next time.
 
Kuna mchangiaji aliyesema kuwa mali kabla ya ndoa haiingizwi kwenye mirathi, mbona mie nahisi mtafaruku zaidi? Kwa hiyo kama kabla ya ndoa nilifanikiwa kujenga nyumba na baada ya ndoa sikujenga tena, hii inakuwa imekaaje? Manake kwa mtazamo wangu, ina maana zile za kabla ya ndoa zinaweza kuachwa kwa mtu yeyote kwa utashi wa mwenye mali. Sasa kama ndoa ina watoto si wanaweza kuathirika kwa maamuzi yetu? Manake kila mtu anavyopenda kuvutia kwake, si ajabu hizo za kabla ya ndoa zikaachwa kwa ndugu wa upande wa mmiliki wa mali hizo!

Hapa nafikiri zinaweza kutumika busara zaidi za wanandoa, kuhusu mali iliyochumwa kabla ya ndoa. Ila kama kila mtu kakomaza sura akiona uchungu wa mali zake, ndio tunarudi kule kuleeeee.....

Pole sana Dina,

Naona ujitahidi kutafuta ukweli juu ya haya mambo...kisheria na naamini utauona mwanga. Mambo unayouliza tulishayaeleza kwa undani sana. Kwa kuanzia hebu pitia posts zote tulizokwishabandika hapa halafu tuendelee na mada!
 
Na hii hofu si ndio inatuongezea maradhi tena jamani? Tuite maisha hayatabiriki au ni nini hiki tena? Yaani...daah hata la kusema sina. Najiona kabisa ndotoni nikiitupia kiberiti hiyo nyumba!

Binafsi naamini kwamba maisha yetu yanatawaliwa kwa kiwango kikubwa na uhuru wetu (+ujasiri) wa kufanya maamuzi (choices). Kwa hiyo tunaweza kuamua wenyewe, ama kuishi maisha kama ya ndege (hajui atakula nini next month) au kuyapeleka tunavyotaka. Ila choice ya kuishi maisha ya mashaka na hofu ni choice ya hatari sana. Personally, I would do anything to avoid!
 
Je, kuna ugumu gani kujadili mambo ya mali kwenye ndoa na kuweka kila kitu sawa?

ugumu ni pale ambapo upo ndani ya ndoa na unaona kabisa jinsi mwenzio alivyo na matumizi mabaya ya mali.
Wengine huamua kufanya mambo kisiri siri kwa sababu hawaaminiani.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom