Ndoa siyo umri, ndoa ni ukomavu wa akili unatokana na malezi

Nov 15, 2019
35
113
Imekuwa kawaida sana kwa nchi nyingi barani Afrika na hata duniani kujaribu kupinga ndoa za mapema na Tanzania ikiwemo. Kigezo kikubwa kimekuwa kitajwa kuwa umri kati ya muoaji na muolewaji.

Baada ya tathmini fupi nimekuja kugundua kuwa suala la malezi lina nafasi kubwa katika ndoa kuliko umri. Hivi sasa TUNAONA akina dada wengi wenye umri wa kutosha wakiolewa na kuachika licha ya uzuri na urembo wanaojisifia nao. Na katika hali ya kushangaza tumekuwa tukishuhudia ndoa za vijana waliooana wakiwa wadogo miaka 18,19, 20 hadi 25 zikidumu sana.

Malezi ya familia zetu yanatukomaza wachache wetu na kutupa ujasiri wa kupambana na changamoto za dunia hivyo kuwa rahisi kuvumiliana na mbilinge za ndoa. Lakini pia kuna wale watoto unaokuta wameielewa kimaandazi, yaani toka azaliwe kichwa chake hakijawahi kuwaza njaa au shida. Huyo hata akiwa na miaka 30 alikiolewa hatodumu endapo atakutana na mazingira ambayo hajawahi kutengenezewa au kuyaishi kabla.

Ongezeko la single mothers chanzo chake kikubwa ni hicho. Single mother ni mwanamke aliyefiwa na mme wake, hao wengine ni Makahaba (Malaya). Kama mme yupo halafu umelelewa katika maadili kitendo cha kuvumilia kupewa Mimba hakiwezi kukufanya uogope kuvumilia ndoa, uvumilivu lazima uwepo.

Miaka ya mtu naendelea kusisitiza siyo Kigezo cha kudumu kwenye ndoa, ndiyo maana unakuta familia moja mabinti wake wote ni mwendo wa kubeba Mimba na kuachika, au nyingine unakuta ni mwendo wa kutumiwa na kutelekezwa na hawaelewi. Hiyo ni shida ya malezi.

NDOA NI MALEZI SIYO UMRI!
 
Tuwalee watoto wetu katika maadili mema hasa wa kike
 
Mkuu uko sailing 100% sema waliokosa malezi ndio watapinga hili, imagine unamuaproach mtu kwa nia ya ndoa, lakini cha kushangaza analeta drama za uboy friends na girl friends huyo bado hajakomaa kwa ajili ya ndoa, hata kama alishawahi kuolewa akaachika na ukilazimisha hiyo ndoa haina maisha marefu, kama unataka kuoa jaribu kuangalia yule ambae yuko tayari kwa ndoa, usimlazimishe mtu ambae bado hajajua ndoa ni nini.
NIMEMALIZA
 
Hiyo imeenda ndugu. IMEENDA.
 
Wenyewe wanadai FAHARI WAWILI AWAISHI ZIZI MOJA...ukiona ndoa zimedumu ujue KunA mmoja kati ya wanandoa kaamua kujifanya mjinga...!​
 
Back
Top Bottom