Ndoa kazi...!

mmm kwa hali hiyo kweli ndoa kazi. Maskini mwanaume namuoea huruma.
Au labda huyu mwanamke ana nyendo za pembeni anaogopa akimwambia mumewe ukweli maswali yatakuwa mengi mno wakati mshahara wake ni mdogo.
 
Ya nini ajue account yangu ina nini cha muhimu chakula ndani kipo anatekeleza wajibu wake wa kulipa ada ya watoto,na kutengeneza miradi ya familia ambayo wote tunatakuwa tunaendesha,kaninunulia mkewe gari na nyumba amejenga i dont nd to know abt his account nor he should know mine dears


Ya kweli hayo Mamzalendo?

Kwamba huna haja ya kujua financial details za mwenzi wako naye asijue zako??


Sina hakika kama nayaelewa haya, labda kwa sababu ni mtu wa generation ya nyuma sana!!


Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Nina urafiki sana na mdada mmoja ambaye ameolewa, mdada huyu tunafanya naye benki moja hivi. mume wake tuna urafiki pia lakini sio kihivo kama mke wake, nadhani ni kwasababu tunafanya naye ofisi moja. Wiki iliyo pita shemeji alinikopa laki! nikaahidi kumpatia jioni, kwakuwa mke wake yupo maternity live, naye kwa bahati alinipigia simu akiniomba nimuangalizie balance kwenye account yake, nilishikwa na butwaa kuona salio la ukweli. Nikajua hapa kuna tatizo.

Nilimkopesha shemeji laki moja akaniahidi atanirudishia baada ya wiki. Sikuishia hapo, nili mpigia mkewake simu nikimuazima laki moja nimrudishie baada ya wiki, bila tatizo, akanipatia.

They are very happy family!!!!!!!

Yani wa hivi wako wengi sana,wanawake wengi pesa zao ni zao tu,sio za familia,ila za mume ni za wote!!ndoa ndoano!!Mume akiishiwa hapewi hata senti,lakini yeye akiishiwa full kubembeleza.Kuna familia ninaifahamu yani mke akinunua kitu cha nyumbani sijui kuku wamepitishwa hapa ofisini,anaenda kumdai mumewe nyumbani,na siku hiyo hiyo kachukua mshahara,kalipwa hela kibao,yani huwa nachoka kabisa,tena anampigia kabisa simu eti kuna kuku hapa elfu kumi kumi nichukue wangapi maana mi sina hela ila wanakopeshwa,kesho nimletee,wakati anahela na atalipa cash,jamani mmh sijui watu wengine wanaishije!
 
Mna uhakika gani kuwa wamefichana?


Teacher Gaijin,

Comment yangu ilielekezwa hapo chini na siyo kwa wahusika waliotajwa na mleta mada au mleta mada mwenyewe!

Smile yawezekana pia hizo pesa kw acc ya mkewe zikawa sio za mshahara...Pili kama yale ya msingi tuliyokubaliana (cost sharing) kulingana na vipato vyetu ivi haya ya kuanza tena kupekenyua acc yake na kufuatilia sana hata ka annua increment sioni kama ni sawa.

Mzima wewe lakini?

Babu DC!!!
 
Last edited by a moderator:
Ndoa ni kitu fulani delicate sana itategemea kabla na baada ya ndoa ulijenga falsafa gani ya kuendesha family yako, yaani ni participatory or non participatory katika upande wa financial, kwani lakini umsome mwenza wako kwa upande wa financial management na ndipo unaweza ukatengeneza utaratibu wa kuendesha familia yako, kuna familia nyingine mwanamume ndiye mtumiaji mbaya wa hela na mwanamke akawa tight nad vice versa.

Kuna siku tulikuwa tunabishana kuhusu kumshirikisha mwenza wako katika mambo yako, jamaa akadai mke wako jaribu kumshiriki baadhi ya mambo na sio yote hasa yale yanayohusu kuweka kifuani kwa muda wote au kipindi fulani kwani mkigombea ambacho kwenye ndoa ni jambo la kawaida atachulia lile jambo ni rungu la kukufanya unyamaze,Kkuna jamaa alimwambia mke wake je unaweza kuvumilia na kutunza siri zangu na ubaya wangu wote kama mme wako, mke alijibu ndiyo,jamaa alikuwa na ugomvi na jamaa x baada ya kugundua alikuwa anamfukuzia mke wake na alipomuuliza mke wake alimjibu jamaa x ananisumbua sana na ananikera sana huku njiani kwani angejua mimi nimetokea kumchukia kwa kitendo cha kunisumbua akijua mimi ni mke wa mtu, jamaa akasema sawa mke wangu lakini angalia maisha haya magumu na magonjwa,Siku moja jamaa alichelewa kurudi nyumbani alipofika akamwambie mke wake, jamaa x nimekutana naye nikampiga hadi kumuua na nimemzika karibu na mgomba kule nje, kwa muda huo jamaa x alisafiri hivyo yule mwanamke akaamini kuwa ni kweli amaemuua, jamaa alijua siku ambayo yule jamaa x alikuwa anarudi, usiku akamchokozke wake na ukatokea ugomvi mkubwa na jamaa alimpiga makofi kadhaa, mke wakemuuaji mkubwa wewe na ndo maana unataka kuniua hata mimi, hivyo sikubali, wakalala mzungu wa nne,asubuhi jamaa akaanzia tena mjadala ule ulipelekea mgomvi kwani alijua yule jamaa x ndo siku ambayo alikuwa anarudi, yule mke wake alienda polisi kushitaki kuwa jamaa ni muuaji kwani alitaka kumuua na tayari amemuua jamaa x na amemzika palepale nyumbani kwake,polisi walichuukua 110 na yule mama, walipofika walimkuta yule jamaa anakunywa chai, walimkata na kumfunga pingu kwa sababu jamaa hakuwa msumbufu hakupigwa, yule mama aliulizwa amemzika wapi wapi alionesha wakaamua kumwambia afukue, walikute kuna mfuko (kiroba) kimefunga na kina damu damu watu wote waliamini kuwa jamaa kamuua jamaa x, walipoungua ndani walikuta mzoga wa mbuzi ambaye jamaa alikuwa na mbuzi, ghafla mbuzi yule alikufa na bwana mifugo alimwamuru amuzike kwani alikuwa mgonjwa. Na bahati nzuri kwa yule jamaa mara jamaa x ndo anarudi na kushangaa kwa jirani kuna watu wengi ikibidi asogee, jamaa alipoulizwa akaeleza kama hapo juu makubaliano yake na mke wake, Je unajifunza nini katika masuala uwazi na mawasiliano katika ndoa? kwani jamaa alisema sio kila kitu unapaswa kumshirikisha mke wako kwani mke wake na jamaa x walikuwa bado wapenzi.
 
we kijana mtoa mada unafanya kazi benki gani?nani kakufundisha kuleta stori za wenye akaunti ktk benki yenu hapa?utafanya watu tusiende kukopa kwa wafanyakazi wa benki ambazo wake zetu wana account huko tukiogopa UMBEA kama wako!

wengine wake zetu walinunuliwa hisa na wazazi wao toka wadogo akaunti always salio la ukweli,so ina maana tusiende kukopa kwingine au kila mara tukope kwa wake zetu?

kwa maoni yangu hilo ni jambo linaloweza kutokea hata ktk ndoa isiyo na matatizo,thats why you said "they are very happy family"

lakini pia angalia si ajabu jamaa hakuamini kwa mkewe baada ya kugundua ukaribu wako kwa mkewe hivyo kakutega akiomba hela kwako utapeleka umbea wako kwa mkewe....na umeshanasa kwa kujifanya mfukunyuku!kazi kwako jombaa!
 
Teacher Gaijin,

Comment yangu ilielekezwa hapo chini na siyo kwa wahusika waliotajwa na mleta mada au mleta mada mwenyewe!

Mzima wewe lakini?

Babu DC!!!

Mzima sana

Sina uzoefu kwenye suala tajwa lakini sidhani kama nitakuwa najua Bwana Mkubwa anakiasi gani kwenye account yake. Naona halinihusu hata kidogo.
 
Nakushauri kama unaweza kuintervene mwambie shemeji yako acheki na mkewe kama ana salio lolote, kama huwezi next time kopa kwa mama mpe mzee kisha mzee akilipa reudisha kwa mama as usual, ila kama ulivyosema ndoa kazi nimekubali ila shauri communication iwe nzuri btn the two. pole kwa majukumu, nina imani next time utakuwa mediator, I mean utarekebisha maugomvi yao.
 
Nakushauri kama unaweza kuintervene mwambie shemeji yako acheki na mkewe kama ana salio lolote, kama huwezi next time kopa kwa mama mpe mzee kisha mzee akilipa reudisha kwa mama as usual, ila kama ulivyosema ndoa kazi nimekubali ila shauri communication iwe nzuri btn the two. pole kwa majukumu, nina imani next time utakuwa mediator, I mean utarekebisha maugomvi yao.

Uliambiwa kuna ugomvi?
 
Yani wa hivi wako wengi sana,wanawake wengi pesa zao ni zao tu,sio za familia,ila za mume ni za wote!!ndoa ndoano!!Mume akiishiwa hapewi hata senti,lakini yeye akiishiwa full kubembeleza.Kuna familia ninaifahamu yani mke akinunua kitu cha nyumbani sijui kuku wamepitishwa hapa ofisini,anaenda kumdai mumewe nyumbani,na siku hiyo hiyo kachukua mshahara,kalipwa hela kibao,yani huwa nachoka kabisa,tena anampigia kabisa simu eti kuna kuku hapa elfu kumi kumi nichukue wangapi maana mi sina hela ila wanakopeshwa,kesho nimletee,wakati anahela na atalipa cash,jamani mmh sijui watu wengine wanaishije!

MJINI MIPANGO SIO PESA!!!! LOL! Bei ya LESSWIG ORIGINAL @ 500,000/= ni kuku wa miezi miwili ndani, ila ndo anaweka kichwani babu weee! Hapo bado kiatu cha PUMPS @ 150,000/= kariakooo UNADHANI KWA MTAJI HUO HELA YA MKEO ITATOSHA!!!!? Wakwanza kumsifia KATOKA BOMBA SANA asubuhi!
 
mjini mipango sio pesa!!!! Lol! Bei ya lesswig original @ 500,000/= ni kuku wa miezi miwili ndani, ila ndo anaweka kichwani babu weee! Hapo bado kiatu cha pumps @ 150,000/= kariakooo unadhani kwa mtaji huo hela ya mkeo itatosha!!!!? Wakwanza kumsifia katoka bomba sana asubuhi!
na hizi saluni ndo zinafanya wake za watu wamegwe ovyo maana kila wiki max 200,000 inahusu!
 
mbona unatetea sana gee...nawewe ndo principal zako nini mama

Sijawahi kuwa kwenye uhusiano na mwanamme unaowezesha hata kunijia wazo la kutaka kujua accounts zake zinasemaje benki, kwa hiyo bado haijawa principle yangu.


Ila nikiangalia ni hivi, sitakaa nijue mume ana kiasi gani kwenye account yake. Akitaka kujua yangu, that's alright, anaweza hata kuwa yeye ndo mtoaji pesa kwenye account hiyo.

Kwangu kuna vitu ambavyo naona nimuachie mwenzangu "privacy" yake, akiamua kuniambia hewallah, ila asipoamua hivyo, sio issue.
 
sijawahi kuwa kwenye uhusiano na mwanamme unaowezesha hata kunijia wazo la kutaka kujua accounts zake zinasemaje benki, kwa hiyo bado haijawa principle yangu.


Ila nikiangalia ni hivi, sitakaa nijue mume ana kiasi gani kwenye account yake. Akitaka kujua yangu, that's alright, anaweza hata kuwa yeye ndo mtoaji pesa kwenye account hiyo.

Kwangu kuna vitu ambavyo naona nimuachie mwenzangu "privacy" yake, akiamua kuniambia hewallah, ila asipoamua hivyo, sio issue.
issue sio a/c zinasemaje...ushirikiano muhimu bana
 
issue sio a/c zinasemaje...ushirikiano muhimu bana

Hakuna anaekataa kuwa ushirikiano ni muhimu.

Ila hatupaswi kuhukumu watu tusiojua makubaliano yao yakoje kwa kusikia tu umbea wa mtu mitaani
 
Back
Top Bottom