mie nimeolewa kwa zaidi ya miaka 10. Mwanzoni nilikuwa mkweli sana kuhusu financial zangu kwa mume wangu..yani kila ninachokipata namwambia halafu tunajadili cha kufanyia..niliamini na mwenzangu yuko hivyo, lkn baadae nikaja kugundua kuwa haniambii ukweli kuhusu kipato chake(baada ya kugundua asset zake ambazo alinificha) na mambo kadhaa ambayo aliyafanya bila kunishirikisha..tuliongea ili tuyamalize na kila mmoja wetu asimfiche mwenzie, aliomba msamaha na akaahidi kujirekebisha lkn hajajirekebisha..kila mara nimekuwa nikigundua/nikiambiwa mambo anayofanya kimya kimya.. Nikimuuliza amekuwa akitahayari tu hana la kusema..nikasema hakuna haja ya kugombana kwa sbb ya kipato cha mtu, nami si ninacho cha kwangu?...nami nikawa naficha kipato changu, simwambii na wala hajui nina shilingi ngapi..nimefungua account bank nyingine naweka huko akiba na wala hajui(ile bank anayojua anayo na password na yuko free akitaka hela nampa kadi).. Nimejenga nyumba 1, hajui na sasa nategemea kujenga nyingine(sitegemei kumwambia vile vile).. Matumizi ya nyumbani nachangia km kawaida tena mara kibao namkopesha kwani mwenzangu hajui bajeti mara kwa mara anaishiwa hata ya mafuta(anaamua kupanda daladala)..
Kwa hivo tatizo ni nyie wanaume sio wakweli..wanawake ni wakweli pale mnapowashirikisha na wanajua bajeti..ni mara chache sn utakuta mwanamke kaishiwa hadi nauli
vipi siku ukipata ajali ukatoweka duniani au umeugua ghafla na madaktari wamesema upelekwe india? Mumewe kucheki acc hakuna kitu anabaki anakulilia na wewe huna fahamu.....
Me nikushauri tu kaeni chini muongee muelewane itapendeza sana vinginevyo haya siyo maisha