Ndalichako: Wanaodaiwa na HESLB tutaweka majina yao magazetini kuwashinikiza kulipa

Kama anafikiri kuweka bango la wadaiwa kwenye magazeti ndio suluhu ya kuwafanya walipe amechemka. Itakuwa ni habari kama habari zingine tu ambazo hazishtui watu.

Hivi kwa mfano mtu alikopa na tangu amalize chuo hajawahi ajiriwa zaidi ya kupambana na ujasiriamali watamkuta wapi?
Watamkuta kwenye database ya TRA labda kama atakuwa kapuku kabisa ambaye haja-qualify hata kulipa kodi..!!
 
Inategemea aina
Kama anafikiri kuweka bango la wadaiwa kwenye magazeti ndio suluhu ya kuwafanya walipe amechemka. Itakuwa ni habari kama habari zingine tu ambazo hazishtui watu.

Hivi kwa mfano mtu alikopa na tangu amalize chuo hajawahi ajiriwa zaidi ya kupambana na ujasiriamali watamkuta wapi?

Nasikia mabenki yatatumika kuwapata. Kwa wajasiriamali na hasa kama kasajili jina la kampuni na kufungua akaunti kwa jina hilo ni ngumu kuwapata
 
Mimi naona serikali ipo sahihi kushinikisha watu walipe deni heslb. Kwanza itasaidia vijana wengi wanaomaliza chuo kutumia zaidi ubunifu wanaopata kijiajiri ili wapate hela ya kulipa deni. Inasikitisha sana kuona tanzania ina wimbi la vijana wanaotaka kuajiriwa baada ya kumaliza masomo badala ya kufikiria njia mbadala ya kuondokana na hali hiyo ili kuondokana na hali ya utegemezi. Watanzania wengi ni wavivu na pia wana tabia ya kuchagua kazi. Hata kazi zenyewe wanazotaka bado wengi wao zinawashinda kufanya. Mfano mzuri muda mwiingine haiingii akilini kuona zamani walimu wengi walikua diploma na certificate lakini wanafunzi walifanya vizuri kwenye mitihani. Ila siku hizi tuna mpaka waalimu wa degree na masters lakini vijana waongiza kuvurunda kuliko hata zamani. Watanzania tuache uvivu na kuchagua kazi badala yake tupambane kikamilifu na hatimaye tuondokane na umaskini.
 
dawa sio kuweka magazetini solution ni kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaoshindwa kulipa...
Dawa pia, serikali kuwatambua pia wale waliolipa kama sehemu ya kuonyesha waliolipa na wasiolipa maana kuna watu wameshalipa lakini ikija issue ya kuwekana hadharani na wao wanawekwa kama hawajalipa kwa uvivu wa serikali kufanya sorting
 
Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema wana mpango wa kuweka majina ya wadaiwa na bodi ya mikopo kwenye magazeti ili kuwashinikiza walipe, amewaasa wadaiwa wakiwapo wabunge walipe ili majina yao yasiwekwe.

Kelele nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Waache kupiga kelele, kuhusu hii ishu ya ulipaji wa hii mikopo, tunataka actions sasa!! chinchilla coat
 
Kelele nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Waache kupiga kelele, kuhusu hii ishu ya ulipaji wa hii mikopo, tunataka actions sasa!! chinchilla coat
Kelele zimeanza tangu June 2009 na watu wakaanza kulipa kupitia kwa waajiri, ajabu wenyewe kama serikali wakapunguza kasi na zoezi kama lilisimama except kwa wale walioanza kulipa, alafu wanakuja tena kupiga kelele badala ya kuchukua hatua wakati majina wanayo tayari.
 
Katika kitu kinachonishangaza ni makelele kuendelea kuwa mengi mpaka sasa bila action hata kidogo. Wangechukua sample tuu, vijana kama 50 ambao hawajalipa halafu wawapeleke mahakamani, mimi ningeona wako serious. Ila hizi kelele kila siku zinanizidishia maswali tuu Jodoki Kalimilo
 
Upeleke mtu mahakamani ambaye hana ajira au hata mtaji wa kuanzia biashara hapo utakuwa umefanya nini? Watu wapo tayari kulipa hiyo mikopo changamoto ni kazi. Wengine mishara wanayo pata ni laki 3-5 bado alipe kodi ya nyumba,nauli ya kwenda kazini,kujikimu kimaisha, kuumwa,anasomesha ndugu....Maisha ni magumu kuliko watu wanavyo fikiria ndugu
 
Na watakuja na mikopo hewa hasa sisi ambao hatukuwa na vigezo vya kupewa mikopo!

Ngoja tuisubiri hiyo list
 
Badala ya kuweka magazetini, ingekuwa vizuri wayaweke kwnye tovuti yao ili watu waweze kuona kiasi wanachodaiwa na kupanga kulipa. Hii itasaidia kwa watu wenye nia nzuri wanaweza kwenda na kukubaliana namna bora ya kulipa kuliko kutisha watu kuwa watatangazwa kwenye magazeti ilhali kumbukumbu hazipo.
 
Bodi inapaswa kumwandikia barua kumlumbusha maana alijaza mawasiliano yake, wazazi, wilaya na Mthamini.
Ni kweli ila hata mdaiwa unapaswa kufatilia deni lako kama vile ulipokuwa unafatilia kama mkopo umeingia!
 
Ni kweli ila hata mdaiwa unapaswa kufatilia deni lako kama vile ulipokuwa unafatilia kama mkopo umeingia!
Mdaiwa afauatilie kwa kutumia utamaduni upi, kwaza hata Bodi ya mikopo watamshangaa kwa nini anafanya kazi ambayo sio yake. Hata Benki ukikopa sio kwaza yako kuambia waanze kukudai.
 
Mdaiwa afauatilie kwa kutumia utamaduni upi, kwaza hata Bodi ya mikopo watamshangaa kwa nini anafanya kazi ambayo sio yake. Hata Benki ukikopa sio kwaza yako kuambia waanze kukudai.
Basi haina shida kinachobakia dawa ya deni ni kulipa acha wafanye kazi ya kuwaweka wadaiwa kwenye mabango maana hamna namna nyingine watu wanabadili namba zao za simu haya masanduku ya posta wachache sana wafatiliaji acha waweke watu wapeane habari
 
Mi'nlichukua mkopo na nimeajiriwa lakini hawachukui mkopo wao!

Naomba mnijulishe ,alafu pia kama kuna zawadi ya mtoa siri ya walionufaika na walipo basi waseme maana nina jamaa zangu kibao
 
Back
Top Bottom