Ndalichako: Wanaodaiwa na HESLB tutaweka majina yao magazetini kuwashinikiza kulipa

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema wana mpango wa kuweka majina ya wadaiwa na bodi ya mikopo kwenye magazeti ili kuwashinikiza walipe, amewaasa wadaiwa wakiwapo wabunge walipe ili majina yao yasiwekwe.

 
Unaweka majina ya nni?
Kwenye ualimu walidai kuna grant na mkopo. Grant hatukutakiwa kurejeshs ila sasa tunarejesha zote na retation fee.
Isitoshe ilitakiwa walau wanaofanya kazi kwenye public sector wangepewa hata robo ya msamaga wa mkopo kama motivation. Cha ajabu unaajiriwa na govt. msalary njiwa na bado wanakata mule mule sawa na wale wanaotumikia private sector wenye mishahara mikubwa na kwa faida ya bwana kheri.
Hvi vitu tunaomba vifanyiwe marekebisho lkn hamna lolote.
 
dawa sio kuweka magazetini solution ni kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaoshindwa kulipa...

tatizo sio kushindwa watu wapo tayari kulipa lkn bodi inashindwa kuweka mechanism nzuri ya kuwafikia.. halafu wakati mwingine mtu unalipa mkopo mpaka unaisha lkn ukihama kazi na kwenda ofisi nyingine unakuta rekodi zako zinaonyesha unadaiwa deni lile lile.. hiyo bodi ijipange kwanza kabla ya kuanza kuwadhalilisha watu magazetini.. mi nishamaliza deni lkn nishahawahi kutangazwa kama mdaiwa sugu na kunisababishia usumbufu mkubwa.. nilipowauliza wakaniomba msamaha na kusema hawatarudia tena lkn wakarudia tena.. sasa hivi wakinitangaza tena sikubali lazima niwashitaki
 
Kama anafikiri kuweka bango la wadaiwa kwenye magazeti ndio suluhu ya kuwafanya walipe amechemka. Itakuwa ni habari kama habari zingine tu ambazo hazishtui watu.

Hivi kwa mfano mtu alikopa na tangu amalize chuo hajawahi ajiriwa zaidi ya kupambana na ujasiriamali watamkuta wapi?
 
Hii bodi ina matatizo sana, wanashindwa nini kuwabana waajiri kuhakikisha wanaodaiwa wanalipa? Sio wote wanaokwepa ila mfumo uliopo sio rafiki kabisa, kwanza nna wasiwasi sana kama wanakumbukumbu sahihi za waliochukua mkopo, waliotoa, waliomaliza na masalio ya wanaodaiwa. Isingewezekana watu wamalize madeni lakini waendelee kudaiwa.
 
Mh hapo naanza kuamini wanaosema kunahujuma zilifanywa na watendaji wa Bodi ya mikopo kwenye kumbukumbu za wadaiwa, kabla hawajaweka magazetini si bora wangetengeneza mfumo kwenye website yao wenye kuonyesha jina la mdaiwa, place of birth, chuo alichosoma, course aliyosomea, mwaka na kiwango anachodaiwa
 
BOOM kwao lilikuwa tamu ,,sasa kimbembe..!
Yaani acha tu, kuna kijana mmoja kanikera kweli...amempotezea muda binti wa watu...alipomtoa huko kwao kanda ya ziwa...amekaa naye karibu miaka miwili na zaidi sasa hivi anamefukuza na hataki kumpa nauli kurudi kwao. Binti kampeleka mahakamani....! Huku mitaani kijana anatamba anasema atawakomesha wanaomshauri huyo binti kumshitaki...maana ela anayo analipiwa 'asilimia mia ' na Loan board!!! Ni kijana mmoja yupo chuo kimojawapo kikuu hapo Morogoro. Inakera sana...walipe!
 
Mbona hakuna mkakati wa ajira kwa waliokopeshwa? Wengine wanatumikia vyeo vya vilevile walivyokuwa navyo kabla hawajajiendeleza, angalia/tengenezakuongeza fursa.
 
Back
Top Bottom