Ndalichako: Wanaodaiwa na HESLB tutaweka majina yao magazetini kuwashinikiza kulipa

Wakimaliza kuweka hayo majina , serikali iyaweke na ya wale waliopata mgao wa fedha za escrow 75%
 
AAAAAAAAAAAAAAAhhhhhhhhhhhhhh udhalilishaji gani, mlipopata mlitangazwa hadharani lakini wakati wa kudaiwa hamtaki....yale yale aliyosema JPM yaani wale mafisadi wanaiba hadharani lakini ukiwatumbua hadharani wanalalamika na kutetewa eti haki za binadamu zinakiukwa....Hoja pekee yenye mashiko katika suala hili ni kwamba wengi hawana uwezo wa kulipa kwa kuwa hawana ajira, hiyo ndiyo hoja na siyo vinginevyo...
Mwambie hayaweke isiwe tabu kwanza msiba wa wengi kwetu sherehe.
Ila tumebwinya...na wengine tumepata degree thru that money kulipa tutalipa pale tutapokuwa tayari maana hata bodi ilikuwa inatulipa ilipokuwa tayari tena hadi tunung'unike.
 
tuna tatizo kubwa la kutopenda kulipa madeni hata kama uwezo unao tuache kudaiwa na serikali hata huku mitaani mtu anakukopa lakini kurudisha hataki watu wawekwe adharani na wakati wa kulipa waongezewe na gharama zilizotumika kuwatafuta na wale ambao hawajapata ajira ama hawajajiajiri utafutwe utaratibu maalumu
 
walimu tunadhalilika sana kisa kutoripoti hawataki kutupa nafasi nyingine ili tulipe madeni sasa wanadhani tutalipaje na mshahara wenyewe mdogo
 
Dawa ya deni ni kulipa. Hakuna mkataba wa mkopaji mpaka apate ajira ndio alipe. Amesoma kwa faida yake. Kulipa deni pia ni kipimo cha uungwana. Lakini namshauri mh waziri ajiridhishe na orodha atakayoweka magazetini. Watakaowekwa kimakosa wakiishitaki serikali maumivu ni kwa mlipa kodi.
 
kwani ukiweka majina kwenye magazeti ndio watu watalipa? tengeneza mfumo mzuri watu walete hela zenu! mi tangia muanze kunikata nahesabu tu!
 
CCM sijui ni nani kawaweka madarakani..
ndio akili zao hizo..
mingine utasikia sanamu la askari liondolewe liwekwe la yo yo yoo..
mara utasikia bunge lisioneshwe ili watu wafanye kazi..kwa nini wasiseme tv zizuiliwe kabisa kwani wengi hupenda kuangalia movie na tamthilia kuliko bunge..

yenyewe kupora madaraka yanaona ni sawa..
ila wewe kuvuna shilingi kwao maumivu..
 
Atuite kabisa kwenye interview anialike mimi nadaiwa..!

Nina hasira na serikali kunipotezea muda wangu miaka mitatu ukilinganisha na viela vyao wanavyotudai..
Elimu yenyewe tumepewa fake..!

Umenichekeshaje,elimu mliyopewa eti ni feki,rafiki ipeleke TBS ikafanyiwe assessment!
 
Umenichekeshaje,elimu mliyopewa eti ni feki,rafiki ipeleke TBS ikafanyiwe assessment!
Mkuu ujasikia kuvunjwa kea tbs ya elimu TCU sasa mkaguzi wa elimu mwenyewe ni feki atawezaje kusimamia watoa elimu wenyewe watoe elimu original??
 
Hebu mnaojua huu mfumo mtuambie wapi serikali imeshindwa kuwabaini wadaiwa.....??? Je ni kweli data za kumbukumbu zilipotezwa

Data lazima zipotee umesahau kuna majina mengine yaliyokuwa hewa na yalianzia huko huko jikoni?
 
Tatizo lingine la wale tunaowaita Viongozi, wengine wanaita kukurupuka.
1. Bodi ya Mikopo ipo kisheria, Ina taratibu zake za kutoa na kurejesha Mikopo hiyo.
2. Je sheria zimeshindwa kufanya kazi?
3. Nani mwenye dhamana ya kusimamia hili?
4. Ndalichako Kama waziri kazi yake Ni kusimamia sheria, kanuni na taratibu na wala sio kuja na mbinu mbadala wakati sheria ipo na inaainisha taratibu za kufuatwa.
5. Kutoa list ya majina kwenye magazeti ni kuingia gharama nyingine na kupeleka uraji kwenye mashirika ya Habari pasipo na ulazima.
6. Aeleze kwanza je taratibu zilizopo kisheria zimeshindwa au hazitekelezeki?
7. Kesho akichaguliwa waziri mwingine naye atakuja na mbinu mpya,yeye ataamua majina yasomwe redioni au kwenye TV.

Ndugu zangu, mawaziri sio watunga sera, taratibu,sheria au kanuni. Kazi yao ni kuhakikisha sheria, kanuni, sera na taratibu za wizara husika zinasimamiwa na kutekelezwa.

HESLB wana mfumo mzuri sana wa uhakiki na utambuzi, Kama wanajua namna ya kuutumia wanufaika hawawezi kukimbia maana taarifa walizoacha Bodi ya Mikopo zinatosha kabisa kuwatafuta na kuwataka kurejesha mkopo waliochukua
.
Mimi ni mnufaika na ninarudisha mkopo huo bila kushurutishwa wala sisubiri nione jina kwenye gazeti.
 
Kama mnaogopa kushainishwa basi lipeni pesa zetu. Kukopa harusi, lakini kulipa mnajifanya ni matanga. Lipeni na wengine wakopeshwe nao waende chuo.
 
Wapewe msamaha,alafu wadogo zako,ndugu na watanzania wngine wasomeje?
Waliosoma kuanzia 1995 wao walisomaje iwapo wa nyuma wamesamehewa na vigezo gani vilitumika kusamehe wa miaka hiyo ya nyuma tu.Kwanini hawakuwasamehe wa kuanzia 2000 kurudi nyuma?
 
Useless, haya magazeti yanatengenezwa na karatasi zinazotokana na kukata miti. Huyu mama asituharibie miti, wanaodaiwa wako wengi mno, ataprint wote? Hehehe aache utani. Internet ipo kwa kazi gani?
 
Back
Top Bottom