Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
..Watawala wetu bado akili zao ziko ndani ya chupa uwezo wa kufikiri kwa mapana hawana zaidi ya kubwatuka kwenye majukwaa. haingii akili mikoa ya Lindi na Mtwara kutoke gesi lakini gesi hiyo inaamishwa kwenda mikoa mingie utadhani wenyeji wameshatosheka.....Sijui ndio hawa wanaitwa wanafikiri kwa kutumia makalio???Mikoa ya Kusini ni bomu linalosubiri kulipuka. Rasilimali kibao zimeanza kuwatoa imani na utu Watawala wetu. Na mazowea ya uporaji na kutojali ni kichocheo cha ndoto ya wanakusini. Gesi toka Songosongo inawanufaisha watu wa mikoa mingine Gesi ya Mnazi Bay ikiunganishwa na ile ya Songosongo kuelekea Mwanza (rejea mipango ya NSSF kujenga bomba Mnazi Bay- Dar-Mwanza) itakuwa uamsho tosha kwa wenyeji wa huko. Tusubiri tuone!