Nchi mpya zinazotarajiwa Afrika

Mikoa ya Kusini ni bomu linalosubiri kulipuka. Rasilimali kibao zimeanza kuwatoa imani na utu Watawala wetu. Na mazowea ya uporaji na kutojali ni kichocheo cha ndoto ya wanakusini. Gesi toka Songosongo inawanufaisha watu wa mikoa mingine Gesi ya Mnazi Bay ikiunganishwa na ile ya Songosongo kuelekea Mwanza (rejea mipango ya NSSF kujenga bomba Mnazi Bay- Dar-Mwanza) itakuwa uamsho tosha kwa wenyeji wa huko. Tusubiri tuone!
..Watawala wetu bado akili zao ziko ndani ya chupa uwezo wa kufikiri kwa mapana hawana zaidi ya kubwatuka kwenye majukwaa. haingii akili mikoa ya Lindi na Mtwara kutoke gesi lakini gesi hiyo inaamishwa kwenda mikoa mingie utadhani wenyeji wameshatosheka.....Sijui ndio hawa wanaitwa wanafikiri kwa kutumia makalio???
 
Mada hii ni ya muhimu sana, hali halisi tuliyonayo africa inatisha na kuchochea uhitaji wa kujitenga kwa maeneo yenye sifa zinazofanana aidha za kijiografia, kiuchumi, KIUTAWALA, nk.
Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi zitakazogawanyika kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu, Kigoma wana sababu,Kila siku wanasema wametengwa, Kagera wanazo sababu zao pia, kila kanda wanasababu na sababu hizo ni muhimu kwao.
Nitaonekana mbaya machoni mwa walio wengi kwa mfano huu, lakini binafsi sioni kwa nini tusiwe na nchi nyingi ndogo zinazowajali watu wake kuliko kubaki na nchi moja kubwa jinga kama ilivyo Tanzania inayowajari wachache na kuwapuuza wengi.
Tofauti ya bei za bidhaa muhimu ndani ya nchi hii inatoshereza ku-justify umuhimu wa kujitenga na dar es salaam, mfano lita moja ya mafuta ya petrol leo ni sh.2300 kule kagera na lita hiyo hiyo ni sh. 21140 dar es salaam, hii tunaambiwa inatokana na umbali kati ya dar na huko kagera. wakati huo huo lita hiyohiyo inauzwa sh. 1800 za kitanzania kule Kigari, Rwanda. Kama umbali kati ya dar na bukoba unasababisha maisha magumu kuan sababu gani ya wana kagera kuendelea kushabikia utanzania.

Mgawanyiko na UTENGANO wa aina yoyote sio mzuri lakini pia ni mzuri kama unalenga kuinua maisha ya watu kuwatoa pabaya kuwapeleka pazuri. Kama malengo ya kutengana ni kuukimbia unyonyaji na unyanyasaji kuna sababu gani ya KUTOTENGANA?
Kama leo tunajivunia kuwa watanzania, si kwa sababu africa iligawanywa na KUTENGANISHWA?
Kama nia ya kujitenga na kutengeneza nchi nyingi zinazotawalika kwa amani kuna sababu gani ya kutojitenga?
 
Ninasikitishwa sana na maoni na matarajio haya....
Je nilini Africa iwe moja kama Taifa?
Ambapo tutakua na sauti yenye ngungu na moja yamajaifa makubwa duniani kwasababu we are the engine of West & East industries.(raw materials)+ we have all factors of production in here.


AMERICAN DREAM WAS NEVER A DREAM, AMERICAN DREAM WAS A DE JAVU.
AFRICAN DREAM IS MORE THN ILLUSION.
AFRICAD DREAM IS LIKE ABANDONED STREAM.
WHERE ARE WE?
 
Baada ya Sudan ya Kusini kujitenga kutoka main Sudan na kuongeza idadi za nchi katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla, inaonekana inaweza kuwa chachu kwa baadhi ya majimbo ama nchi kumegeka,
inaweza kuongeza nguvu kwa nchi zilizokuwa kwenye maelekeo huo na pia inawweza kuwa chachu kwa nchi/majimbo mapya, baadhi ya majimbo na nchi hizo ni kama ifuatavyo
1)TAnzania
Kwa hali ya kisiasa na nchi kukosa mwelekeo wa kujua ni kipi cha kushika kwanza, kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kutoka kwenye muungano,

2) DRC
Ni miongoni mwa Nchi kubwa kabisa Barani Afrika na duniani
Tatizo kubwa la DRC ni Majimbo yaliyogawanjwa kwa minajili ya ukabila, Congo DR pana ukabila mkali kabisa, Baadhi ya Province za Congo zimeendelea sana na sababu zinazotoka kwenye province ambazo ziko nyuma kimaendeleo ni kuwa hizo zimeendelea kutokana na viongozi

3) Morocco
Polisario wamepigana kwa miaka mingi mno kutaka kutoka Morocco na kuwa na nchi yao ya Sahara Magharibi, haya mapinduzi ya nchi za kiarabu na kupatikana kwa uhuru wa Sudan ya kusini ambao walikuwa almost wanafanana kwenye kutafuta uhuru wao,inawatia Chachu kubwa kwa watu wa sahara Magaharibi, kuongeza nguvu zao za kudai Nchi "yao"

4) Somalia na SomaliLand nchi inayojiendesha yenyewe lakini bado haijajitangazia uhuru wake,

5) Baada ile issue ya Biafra Nigeria inaonekana kana kwamba bado wapo Pamoja, lakini muendelezo wa siasa za Kidini na Kikabila zinaonyesha wazi uwezekano wa nchi kumegeka

mitizamo yenu ni ipi wana JF
Hizo nchi hapo juu ukioondoa Somali, zinaweza tu kujitenga hiwapo itathibitishwa kuwa wana mafuta ya kutosha kuchimbwa kwa zaidi ya miaka mia moja (100)...!

Wanachotakiwa ni kuongea tu na wakubwa wa hii dunia na kuwahakikishia tenda zote wanakamata wao tu basi.... zengwe litatengenezwa... baada ya hapo Damu zinamwagwa baada muda nchi zinagawanywa.
 
Hizo nchi hapo juu ukioondoa Somali, zinaweza tu kujitenga hiwapo itathibitishwa kuwa wana mafuta ya kutosha kuchimbwa kwa zaidi ya miaka mia moja (100)...!

Wanachotakiwa ni kuongea tu na wakubwa wa hii dunia na kuwahakikishia tenda zote wanakamata wao tu basi.... zengwe litatengenezwa... baada ya hapo Damu zinamwagwa baada muda nchi zinagawanywa.

...hii ndio point,hizo sababu zingine za kikabila bila motives za kiuchumi hazina maana na wakijaribu kujitenga tuu litatumwa jeshi kuwaswaga kama ng'ombe na mtajuta kuzaliwa maana mtafungwa jela mpaka wajukuu zenu
 
Mkuu mbona vitisho sasa,nirudi kwenye maada kama hizi nchi hazikuwepo na mipaka ya yaleo iliwekwa na wakoloni basi yamezekana kuundwa upya au nyingine kuudwa tena.Mfano Kigoma na Kagera zinalingana karibu na Rwanda na mikoa hii inaweza kuunda Taifa na likasimama ila sishawishi hivyo bali la Tanganyika halikwepeki mandugu kwa sasa.
 
Tunahitaji Chagga National yetu.
Mkishajitenga hamtakuwa salama, mtaendelea kujitenga tu wamarangu kivyao, wamachame kivyao, waoldmoshi kivyao, warombo kivyao, wakishumundu kivyao n.k
 
nimesoma uzi huu ikaja ghafla kauli ya warioba kuhusu muungano mwalimu alivyo uacha na sasa ulivyo ila tungojee yajayo
 
Kujitenga kwa Tanzania ni jambo Gumu sana, kwa bahati mbaya, hakuna mkoa wala kanda una/inayo/ojiweza kwa asilimia zote bila kutegemea mkoa mwingine, utegemezi huu unaifanya nchi yetu kuendelea kua moja.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom