Naweza kumuoa huyu?

Nimempenda mjukuu wa shemeji yake shangazi yangu.

Ninampango wa kumuoa but binamu zangu wananikatalia eti ndugu.

Jamani hebu nipeni ushauri hapa
ushauri ndio huo umeshapewa na binamu zako au unataka tukuambie umuoe huyo mjukuu?
 
hiyo iko wazi kabisa huyo ni ndugu wa mbali sana hata mambo ya genetics hayawezi kuwaathiri katika vizazi vyenu. kila la heri
 
hiyo iko wazi kabisa huyo ni ndugu wa mbali sana hata mambo ya genetics hayawezi kuwaathiri katika vizazi vyenu. kila la heri
kwani wanawake wameisha bana mpaka akambanebane ndugu yake hata kama ni wa mbali kiasi gani
 
kwani wanawake wameisha bana mpaka akambanebane ndugu yake hata kama ni wa mbali kiasi gani

kwani mtu anapofanya uamuzi wa kumuoa fulani say Judith, ina maana wanawake wameisha duniani? kuoa si kuoa tu jamani? pia sioni kama ni kumbanabana bwana, huwezijua walikotokea
 
Njoo zanzibar uone mambo, mtoto wa baba mdogo anaelewa kama kawaida, ijekuwa huyo mtoto wa shemegi wa shangazi...
 
Nimempenda mjukuu wa shemeji yake shangazi yangu.

Ninampango wa kumuoa but binamu zangu wananikatalia eti ndugu.

Jamani hebu nipeni ushauri hapa

Mkuu,

Unapiga jicho watu wako wa karibu, Aouiii, wewe mkali...Aisee,wamekustukia. Na wengine watakuogopa sasa.

Wewe jogoo hasa, hapo hapo kibandani kwako!!

Kuna mtu aliwahi kuuliza humu JF,” yaani sielewi, hawa watoto wa Adamu na Hawa walikuwa wanaoana dada na kaka?”
Kama una jibu la suali hili, mkuu. Jibu la suali lako unalo mwenyewe !!
Good luck ! Itakapokuwa tayari ,utualike, tuje tukupongeze, mkuu.
 
hakua undugu hapo wala hamna damu zenu inayo changanya miilini mwenu.

du lazima umeshalala nae pia
 
Nimempenda mjukuu wa shemeji yake shangazi yangu.

Ninampango wa kumuoa but binamu zangu wananikatalia eti ndugu.

Jamani hebu nipeni ushauri hapa

Huyu mbona ruksa kutafuna wewe tu unachelewesha ukiona bado wanakubania mvimbishe tu kitaeleweka
 
kwani mpaka ule zizi la nyumbani? Mbona inawezekana msichana mzuri na anayefaa kuwa mke wako yupo 5km kutoka hapo ulipo? Na mwingine yupo 200km. Mjukuu wa shangazi yako, ni sawa na mjukuu wa baba yako (baba na shangazi ni mtu na dada yake), na ni sawa na mtoto wako. Upo hapo? Genetically sio safi sana. Kama kuna inferior traits kwenye ukoo wenu, zinaweza kujitokeza kwa watoto wako.

si mjukuu wa shangazi mkuu. Mjukuu wa shemeji ya shangazi yangu
 
kwani wewe maeneo unayokaa hakuna mabinti wengine wanaofaa kuolewa na wewe???. Acha tamaa ya fisi. Inawezekana wanaokukataza wanajua kikwazo kiko wapi.

nimeangaika sana. But this is my choice.... Tunampendana kuliko ujuavyo!
Haja ya moyo wangu imefika hapa mkuu
 
asiyeckia la mkuu... Usipende kupuuza ushaur wa wakbwa zako. Ww na hyo bnt hakna mlijualo dats y uliomba ushaur kw ndgzo, wackilze walchosema.

sijawaomba ushauri mkuu, nimetangaza nia..
 
kwani mtu anapofanya uamuzi wa kumuoa fulani say judith, ina maana wanawake wameisha duniani? Kuoa si kuoa tu jamani? Pia sioni kama ni kumbanabana bwana, huwezijua walikotokea

Namjua tangu primary, japo nilikuwa sijapangiwa huo undugu da judy, asante kwa kunipigania
 
akina mama bwana mambo ya kuoa matamu huyo alie kaa kimtindo ananimaliza sana anajiita first lady je umeolewa
 
Back
Top Bottom