Natoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Prof. Jay katika kampeni ya kumpata fedha za kuhudumia wagonjwa wa figo

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Nitoe pole kwa Prof. Jay kwa machungu aliyopitia kipindi chote cha ugonjwa. Ninashukuru mwenyenzi Mungu kwa kuzidi kumpa nguvu na afya yakumtumikia.

Nimpongeze pia Prof. Jay kwa kuona upo umuhimu wa kuwa na foundation itakayosupport wagonjwa wa figo. Hii ni vision nzuri na nia njema kwetu ambao ni wazima na hata wale wagonjwa.

Naomba niwakumbushe Watanzania kwamba moja ya eneo tunalopaswa kulitolea sadaka na kuliendelea kila iitwapo leo ni eneo huduma ya Afya. Ukiwa mzima ni vigumu kutambua umuhimu wa hospitali, ila ukiugua unaweza ukatambua umuhimu uliopo.

Kupitia Jamii forumu naomba kuweka hapa challenge ya kukusanya fedha kwa kiwango ulichojaaliwa kuunga mkono juhudi za ndugu yetu huyu kupitia akaunti zilizowekwa kwa umma.

Tukifanya hivi tunaweza kuokoa maisha yetu na maisha ya ndugu zetu wasio na uwezo wa kujihudumia. Hata wewe fedha nyingi usipotafakari na kuona kwamba fedha zinaisha ukiugua utaweka kiburi. Ila ukitambua kwamba fedha ni kitu cha kupita utawekeza Sehemu ambayo siku ukifilisika basi utapata msaada.

Karibuni tumuunge mkono mwenzetu
 
Back
Top Bottom