Natangaza 'kumdharau' January Makamba rasmi!

He is a right seed on a wrong part of barren land. lucky enough the seed has still a life
 
Speaker,
Unaweza kumlaumu sana Makamba lakini ukweli unabakia kwamba makosa sii yake bali mfumo wa bunge letu. yeye kama mjumbe wa chama ktk kikao cha chama wajibu wa kujibu mapigo kutoka upande wa pili japokuwa pia Makamba ni mwenyekiti wa kamati ya bunge (madini) nafasi ambayo hakutakiwa kuishika... Unafiki unatokana na muundo wa Bunge wenyewe maana hakutakiwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya madini bungeni, isipokuwa nafasi hii hupewa Upande wa Upinzani kuishinikiza serikali ktk utendaji kazi wake.

Unafiki wa Makamba unakuja pale anapochukua nafasi ya Upinzani hali yeye ni CCM, kupambana na Ngeleja na wizara yake (kinyume) akaonekana mwenzetu lakini anaposikia swala la kuiangusha serikali yake anabadilika na kuchukua nafasi ya chama kwa sababu yeye pia kapewa wajibu wa kutetea chama. Na kama mnakumbuka nafasi hii ilipokuwa imeshikwa na Zitto tuliona mengi sana machafu ya wizara ya madini lakini tumechezewa akili, jukumu hilo sasa wamelishika CCM wenyewe ikiwa ni pamoja na nafasi nyingine zilizoshikwa na chama tawala kama ile ya Lowassa naye bungeni. Haya yalikuwa sii makosa ila makusudi na Unafiki mzima wa chama hiki cha CCM chini ya mama Anna Kilango.

Huu ni unafiki wa serikali yenyewe kuweka makundi ndani ya chama chao hadi ndani ya Bunge, upinzani uliopo ni wa makundi ya JK vs EL na sio vyama na ndio maana Makamba anamtafuta Ngeleja kwa maslahi ya makundi yao na sii Kitaifa. Ukitazama vizuri waliopewa uenyekiti wa kamati za bunge kutoka CCM, wote ni kambi ya EL, Chadema walipewa sehemu kamati ambazo wao CCM walidhani wanaweza kukabiriana na mashambulizi japokuwa Zitto kawakamata pabaya na kuyavuruga makundi yao kumwajibisha Waziri mkuu..Ndio maana wao wanaendeleza hoja yao ya kuwa ni baadhi ya mawaziri wanaotakiwa kujiuzuru na sio ile ya Zitto ya kumwajibisha waziri mkuu.

Na hata ukitazama mawaziri ambao wanatakiwa kujiuzuru ni wale wa kambi ya JK sio ya EL na hakuna uthibitisho wowote wa makosa yao zaidi ya tuhuma. Leo hii tukitazama hao mawaziri ambao wametakiwa kujiuzuru hatuna ushahidi wa kutosheleza wao kujiuzuru - Hatuna isipokuwa wao CCM wenyewe wametafuta mabangusilo ili kuifubaza hoja ya Zitto. Hivyo, Makamba kama mwenyekiti wa kamati ya madni alitakiwa kuwa wa kwanza kutupa saini yake lakini vile vile wajibu wa chama chake unamkataza kuwa upande wa Upinzani hasa pale hoja inapotoka Upinzani.

Kwa hiyo mtoto wa nyoka ni nyoka tu, Makamba kusimama kama mwenyekiti wa kamati ya bunge haina maana ni Mpinzani hata kidogo tulipigwa changa la macho. Na asingeweza kuweka sahihi hoja ya Zitto kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mjumbe ktk kikao cha kujibu mapigo hivyo kumweka ktk unafiki..
 
January Magamba huyo mtoto ni mbaya sana,pindi akiwa pale mjengoni alifanya nini? Na sasa ni mbunge wa bumbuli,na huo ubunge aliupata kupitia mgongo wa baba yake mzee yusuph makamba pindi akiwa katibu mkuu wa chama cha majizi (ccm) makamba acha kulopoka kaa kimya uwaziri huupati ng'o
 
Pole sana kwa Fault ya kudhania J.Makamba kuwa ni Mbunge wa aina yake.Nakuonea huruma kula matapishi yako nadhani ulitambua kuwa atakuwa anakufurahisha kila siku kumbe ulikuwa unajilisha au kubwia unga wa ndele.Ndugu yangu elewa kila mtu ana utashi wake hivyo si rahisi kufurahishwa kila siku na haitokei kila siku ukawaza kitu sawa na mwenzako.Jifunze huyo J.Makamba hayupo bungeni kwa ajili ya kukufurahisha wewe.Inawezekana hata nawe ni mnafiki angalia thread yako hii mpya na ile ya zamani sasa una tofauti gani na J.Makamba?

Wakurogwa nimekuelewakwamba haufikirii vizuri kwa sababu
ya wachawi wanao sumbua akili yako,sikulaumu kwa hilo,sawa,tufanye na mimi ni mnafiki.
Unadhani unafiki wangu una madhara gani kwa nchi?
Mimi ni kiongozi wa maisha yangu,na familia yangu,siongozi
kundi la watu walonichagua na haitatokea.

Yeye ni kiongozi wa kundi,ingawa hali kumchagua pia lakini
kwa katiba mbovu hii tuna lazimishwa kuamini ana wakilisha
wana Bumbuli kweli.

Lakini kwa kofia hiyo,ni haki kwake kuwa mnafiki kiasi hicho?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi sio Januari tu, ccm hakuna hata mmoja mwenye upendo na nchi hii. Kwa nyakati tofauti na kwa maslahi tofauti (binafsi au ya chama) inaweza kudhaniwa kuwa ccm wana watu wachache wenye nafuu lakini ukitazama pica nzima hakuna kitu.
 
Sichukii kutofautiana mawazo na mtu katika jambo lolote,mana unaweza kudhan jambo flan ni kwa maslah ya taifa na ukawa na sababu ambazo kwako ni za msingi lakin mwenzako akaona vinginevyo kwasababu zinazomshawish yeye..ila nachukia unapotumia hila kuzuia wazo la mwingine hata kama linamantiki na kumnyima nafas ya kushawish wengine juu ya wazo lake/kudiscourage wengine hata kumuunga mkono, tena unafika mahali unajifanya hamnazo hata kama unaelewa kinacho. Walichofanya Makamba na Madam Anna sielew kina mantiki gan..Madam Anna kama jins alivyomezeshwa, kakurupuka akianza kwa kunukuu kanuni za bunge anazotaja kua zinaendana na katiba kua; wabunge wakitaka kuleta motion ya ktokua na imani na PM ni lazima waandike barua iliosainiwa na wabunge wasiopungua 20% ambao kwa idadi ya bunge letu ni wabunge 70 then wawasilishe kwa speaker 14 days before intended date of vote..after that akakurupuka"zoez linaloendelea la kupigishana sahihi ni batili kwakua mimi sina taarifa". Sasa taarifa ipi unayotakiwa kupewa mama zaid ya barua yenye saini sabini ambazo ndio zinatafutwa kwa hilo zoez unaloita batili?au hizo sahihi zinapatikanaje basi ili zoez la zitto lisiwe batili kwa mujibu wa kanuni zako?kama kanuni inatoa mwongozo wa namna ya kuandika barua yenye sahihi sabini pasipo kuzikusanya bungen ungefafanua. Hata hivyo huyu mama honestly nimefika mahali nashindwa kumlaumu kwan mara nyingi hua namuona kama hana uwezo wa kufikiri kwa haraka. Akipandikizwa kitu mradi ni cha chama chake nae huenda hewan bila kujiongeza. Lakin Makamba anaelewa kabisa alichofanya sio. Na unafiki wake uko hapa;mara ya kwanza hoja ya sain zitto aliitoa bungen na kutoa wito kwa kila mbunge mwenye nia njema na nchi, na anaeona kua ubadhilifu ulioripotiwa na CAG kufanyika katika wizara mbali mbali unamkera na unastahili hatua kuchukuliwa basi atie sain yake kwe hiyo barua kesho yake asubuh ambapo yeye Zitto alieleza atakua akikusanya sahihi hizo nje ya bunge. Hapa ndio mana hata kina Deo walitia sahihi .
Sasa yeye (Makamba) anapokuja kulalama eti mara nyingi tumekua tukiimba kua tunataka bunge la umoja na huku akijifanya kama hajui hilo zoez la kutia saini linaendaje,nakuhoji kama Madam ana taarifa ya zoez linaloendalea,tena anenda mbali na kudai kua anasikia kwe vyombo vya habari kuhusu hilo zoez!!!!???
Huu ndio unafiki kwan maombi ya saini yalitolewa bungeni na utaratibu uliwekwa wazi. Isitoshe saini zenyewe zilikusanyiwa bungeni na si kwe ofice za CDM.
Ye angekua muwaz tu na msimamo wake kua walichofanya mawazir wa ccm haoni kama kinawafanya kustahili kuwajibishwa au labla anaona kuwawajibisha kwa kupitia kumpigia vote of no comfidence PM ni excessive measures na haina maslah kwa taifa mi ningemuelewa kwakua huku ndio kutofautiana mtazamo kuhusu jambo fulani. Au angekaa tu kimya kwan kuna mtu angemuuliza?
Kama kweli maana nyingine ya Parliament ni kundi la mabundi basi hiyo ni tafsir sahihi na waliotia sahihi ni wachache wenye bahat mbaya waliolazimika kuchanganyika na mabundi katika kutetea nchi yao.
Ukitofautiana na mtazamo huu kwa dhati sikulaumu kwan n haki yako. Nawasilisha.
Hakuna sehemu ambayo J.Makamba amepinga we inawezekana una matatizo binafsi.Kimsingi utaratibu ndiyo ufuatwe katika kutekeleza dhamira iliyopo na siyo kufanya jambo kubwa kama lile kwa kukurupuka katiba na taratibu za kibunge lazima zifuatwe ili kumuondoa Pinda sasa huyu J.Makamba kakosea wapi?yani kuomba muongozo tu imekuuma sana hebu kuwa muungwana bana.Tumia uelewa wako vizuri katika hili.Wote tunakubali serikali haiwajibiki hivyo kuwawajibisha ni kutumia njia sahihi na siyo hiyo unayoitaka wewe.Bila shaka watanzania wengi tumeelewa sasa namna ya kumwajibisha PM sasa we unataka kama unavyowaza tukifanya hivyo nasi tutakuwa wamajawapo wa watu tunaotaka kuipeleka nchi mahali pabaya.Nafikiri huo ni utaratibu tu Mkuu.
 
Speaker,
Unaweza kumlaumu sana Makamba lakini ukweli unabakia kwamba makosa sii yake bali mfumo wa bunge letu. yeye kama mjumbe wa chama ktk kikao cha chama wajibu wa kujibu mapigo kutoka upande wa pili japokuwa pia Makamba ni mwenyekiti wa kamati ya bunge (madini) nafasi ambayo hakutakiwa kuishika... Unafiki unatokana na muundo wa Bunge wenyewe maana hakutakiwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya madini bungeni, isipokuwa nafasi hii hupewa Upande wa Upinzani kuishinikiza serikali ktk utendaji kazi wake.

Unafiki wa Makamba unakuja pale anapochukua nafasi ya Upinzani kupambana na Ngeleja na wizara yake (kinyume) akaonekana mwenzetu lakini inaposikia swala la kuiangusha serikali yake anabadilika na kuchukua nafasi ya chama kwa sababu yeye pia kapewa wajibu wa kutetea chama. Na kama mnakumbuka nafasi hii ilipokuwa imeshikwa na Zitto tuliona mengi sana machafu ya wizara ya madini akini tumechezewa akili jukumu hilo sasa wamelishika CCM wenyewe ikiwa ni pamoja na nafasiu nyingine zilizoshikwa na chama tawala kama ile ya Lowassa.

Huu ni unafiki wa serikali yenyewe kuweka makundi ndnai hadi ndani ya Bunge kisi kwamba upinzani uliopo ni wa makundi ya JK na EL. Ukitazama vizuri wote waliopewa uenyekiti wa kamati za bunge toka CCM ni kambi ya EL, Chadema walmepewa sehemu ambazo wao wanaweza kukabiriana na mashambulizi japokuwa Zitto kawakamata pabaya na kuyavuruga makundi yao yawajibike.

Na hata ukitazama mawaziri ambao wanatakiwa kujiuzuru ni wale wa kambi ya JK sio ya EL na hakuna uthibitisho wowote wa makosa yao zaidi ya tuhuma. Leo hii tukitazama hao mawaziri ambao wametakiwa kujiuzuru hatuna ushahidi wa kutosheleza wao kujiuzuru - Hatuna isipokuwa wao CCM wenyewe wametafuta mabangusilo ili kuifuabaza hoja ya Zitto..

Kwa hiyo mtoto wa nyoka ni nyoka tu, Makamba kusimama kama mwenyekiti wa kamati ya bunge haina maana ni Mpinzani hata kidogo tulipigwa changa la macho. Na asingeweza kuweka sahihi hoja ya Zitto kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mjumbe ktk kikao cha kujibu mapigo hivyo kumweka ktk unafiki..

Asante sana Mkandara.
Sasa ume nifumbua macho kwamba unafiki sio wa mtu mmoja mmoja bali
ni wa mfumo mzima,.....

Kumbe na J.M yuko sahihi pia,kwamba wanao "chonga sana" hawajui,ni
kweli nilikua sijui,kumbe kinacho endelea ni unafiki wa ajabu na
hadaa kwetu wananchi,.....salaaaaale.
 
Last edited by a moderator:
like father like son,,,,, Riz1 = J.Kikwete Januar .M= Y.makamba .............waweza kuendeleza list
 
Tatizo jingine la statement fupifupi kama hizo, maana halisi anaijua aliyeiweka. Sie wengine tunapapasa tu. Anaweza kuja hapa na kutoa maana tofauti na haya tunayojadili
 
...can U put it more open,how and where He cheated,which school and year of examz,sabu wa2kama hawa wako kibao na bila kuwaanika wanakuwa wanatamba sana street Mkuu,I wuld lov2c dataz in detailz....
Kaka kwa watu makini mnafiki huyu utamtambua tu... kumbuka wakati yuko ikulu alivyokuwa anatetea kila uozo.. alifanya nini alipoupata ubunge wa kulazimisha? Alitaka nafasi ya Ngeleja , hakuupata uwaziri akaanza unafiki.... sasa anaona kama Zitto kascore point, inamuuma , ni mnafiki wa kutupa.. but what do you expect from someone who cheated on a secondary school exam? and mind you he was like roughly 17 years old back then.... mtoto wa mbwa hawezi kugeuka kuwa njiwa!
 
yaani ukimwamimini mtu alieko ccm ni sawa na kula nguruwe msikitini ,,,...... ukiwa ccm kijana unakuwa mnafiki ukizeeka unakuwa mchawi kama mkapa.eti atamwambia jk arudishe mashamba meru wakati ni yeye aliyauza
 
Hana lolote zaidi ya ulevi wa madaraka hapa ndipo tunapokumbuka maneno ya vitabu vitakatifu kuwa ni vigumu kwa tajiri kuigusa pepo....
 
Mnafiki tu, mshenzi na miwani yake na visuti kama ndege John, yaani ni aibu sana kwa mtu wa umri wake kuwa na tabia kama ile, huyu ni wakumtosa Ubunge 2015, keshajiona sijui yeye nani, hivi huu uozo unaofanyika serikalini mtu anateteaje huu Ujinga jamani?
 
Jamaa alipewa kadi feki kibao za chama wakati wa kura za maoni ccm akazitumia kumchakachua mzee Shelukindo akapata ubunge bila jasho, ni zao haramu la kisiasa na lazima utegemee haramu kibao hapo
 
speaker ndugu yangu hakuna haja ya kumlaumu makamba hapa tatizo ni chama chake na wanachi wanaoendelea kukipigia hiki chama kura za ndio
 
Nilianza kumdharau january katika kipindi cha salama alipokuwa anaoshwa miguu live kwenye TV hivi January ni Public figure? Tumbafu January.
 
Back
Top Bottom