Natamani kuwa na mwisho mwema kama Babu wa Loliondo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,928
Hiki ni mojawapo ya kifo cha furaha nilichowahi kushuhudia ...! Mzee Mwaisapile almaarufu kama Babu wa Loliondo ametwaliwa kutoka maisha haya.. Mwendo ameumaliza salama ... Kwa amani na kwa furaha... Alimuishi Kristo Yesu akamtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa

Maneno ya Mungu yanasema maisha ya mwanadamu ni miaka 70 na ukiwa na nguvu ni miaka 80, baada ya hapo unaishi miaka ya bakshish...Naamini mzee Mwaisapile kaishi na ya ziada

Hakuwahi kujulikana popote katika kazi yake ya utumishi wa kiroho kwenye imani yake ya Kikristo kupitia kanisa la Kilutheri..alihubiri na kutumika kwenye madhabahu ya Mungu mpaka anastaafu akiwa hana kitu chochote cha thamani cha kidunia zaidi ya kibanda cha nyasi alichokiita nyumba yake. Lakini hakuwahi kulalamika popote wala kumlalamikia yeyote

Mungu anaona yote ... Naye akamwambia.. Kwakuwa umenitumikia kwa uaminifu NITAUSHIBISHA MEMA UZEE WAKO! Mara paap! Kikombe hicho
Hakujitangaza popote iwe mitandaoni, kwenye vyombo vya habari ama kutembea na maspika ALITANGAZWA kwa sauti iliyoenda mbali sana
Hakuhangaika kutafuta wasaidizi na watenda kazi..! WALIKUJA wenyewe..
Hakuhangaika kuleta WALINZI wala kuwalipa POSHO watu walijitolea

Watu wakamiminika Loliondo toka pande zote za dunia kwenda Loliondo kupata kikombe cha babu kinachoponya magonjwa mbalimbali...Habari zake zikavuma na kutangazwa mpaka na vyombo vikubwa vya habari duniani

Akawa balozi mzuri aliyeitangaza Tanzania na Loliondo kwa uzuri baada ya eneo hilo kugubikwa na migogoro na kashfa zilizosababishwa na wanasiasa WAROHO wa mali
Wanasiasa na viongozi mbalimbali wa nchi yetu hawakuwa nyuma kwenye kwenda kupata kikombe cha Babu..Mungu akaushibisha mema uzee wa babu..Mchungaji mstaafu Mwaisapile..!

Lililo kubwa na la ajabu hakutoza fedha kubwa kwenye tiba yake ya kikombe! Alitoza mia tano tuu/500 na katika hiyo yeye alichukua mia mbili tuu/200 nyingine zikaenda kwa watenda kazi na wasaidizi wake.. Na wote walitumikia kwa uaminifu mkubwa..!
Tiba ile ilikuwa na maajabu mengi
Kupitia hiyo tiba utalii ukaongezeka
Kupitia hiyo tiba Tanzania ikazidi kujitangaza kimataifa
Kupitia hiyo tiba watu wakafanya sana biashara
Kupitia hiyo tiba watu wengi wakapona maradhi yao, wengine walikufa njiani na wengine hawakupona.. Kwakuwa kila kitu kina pande mbili
Kupitia hiyo tiba tuliwaona manabii na mitume wengi katika rangi zao halisi..Wivu ukawajaa na kuanza kumshambulia babu kwa kila hali..LAKINI KAMWE HAKUJIBIZANA NAO..Alimuachia Mungu aseme nao...

Atazikwa mazishi ya kawaida kabisa. Mwili wake hautataabishwa huku na kule wala hautanuka.. Atazikwa akiwa fresh kabisa bila kuanza kuoza akiwa bado duniani..pengine hatakumbukwa duniani lakini anayo nafasi yake mbinguni siku ya kiama...
Apumzike kwa amani mtumishi mwema na mwaminifu wa Mungu.. Natamani kuwa na mwisho mema kama yeye

Mungu nisaidie

giphy.gif

Nimekuelewa sana hapo mwishoni. Binafsi sivutiwi na tabia ya dunia ya sasa, na kwa baadhi ya watu ya kumuweka marehemu wiki kadhaa bila sababu, au kumgeuza kama kinyago cha maonesho.

Hata kumuona marehemu sura ya mwisho ni bora ingebakia tu kwa watu wake wa karibu, huku wengine wakimuona kupitia picha yake.

Apumzike kwa amani! Kiukweli aliwakamata wengi kwa kile kikombe chake.
 
Mimi sijui Kama Tiba yake ilisaidia wagonja au laa,Ila alichonivutia huyu mzee ni hakuwa na tamaa ya kuwa millionaire kuwa toza wateja wake pesa mingi,alilizika na 200/= tsh.tu basi. sawa na pesa ya kununua pelemende mbili tu .apumzike kwa amani mzee wetu!
 
Ile ni kama tiba yoyote ile
Baadhi itawaponyesha
Baadhi haitawasaidia kabisa
Baadhi itawadhuru
 
Nimekuelewa sana hapo mwishoni. Binafsi sivutiwi na tabia ya dunia ya sasa, na kwa baadhi ya watu ya kumuweka marehemu wiki kadhaa bila sababu, au kumgeuza kama kinyago cha maonesho.

Hata kumuona marehemu sura ya mwisho ni bora ingebakia tu kwa watu wake wa karibu, huku wengine wakimuona kupitia picha yake.

Apumzike kwa amani! Kiukweli aliwakamata wengi kwa kile kikombe chake.
Wengine walipona kwa imani na huo ndio muktadha wa kikombe...na illikuwa ni lazima ujushushe.. Ukienda pale na ukuu na sifa zako kikombe lazima kikukalishe.. Ama ukatumia ujanja ujanja hila na ubabe kufika mbele ya babu kikombe kiligeuka mma tuu
 
Sanaa ya kifo
 
Mimi sijui Kama Tiba yake ilisaidia wagonja au laa,Ila alichonivutia huyu mzee ni hakuwa na tamaa ya kuwa millionaire kuwa toza wateja wake pesa mingi,alilizika na 200/= tsh.tu basi. sawa na pesa ya kununua pelemende mbili tu .apumzike kwa amani mzee wetu!
Ile fursa wangeipata hawa wachungaji wetu nahisi kikombe kisingenunulika, wamejaa tamaa.
 
Back
Top Bottom