Natamani kujua waliompa kura Rais Magufuli wanajisikiaje sasa

Najisikia flash tu maisha magumu nayasikia kwenye mitandao tu wamtaani huku wanasema hawajawahi ona maisha yamekuwa mepesi tangu uhuru sasa tatizo sijui ni nn
 
Usilolijua ni usiku wa giza. Mimi naamini kuna waliompigia kura Magufuli wakijua watapata neema na maisha yao yatakua rahisi kama ilivyokua mwanzoni.

Natamani kupata maoni yao na kujua maisha wanayoishi sasa hivi. Poleni kwa mliojiaminisha goodlife inaweza kuwepo bila kuhangaika

Good day
Tunapeta na tunamshukuru Mungu kuwa kura zetu hazikuharibika, JPM ni chaguo la Mungu! Tunaomba kwa Mungu aendelee kukaza hivi hivi au aongeze zaidi, heshima inarudi! Asiyefanya kazi na asile!!
 
Mimi pia nilimpigia kura yaani nsjisikia burudani sana achani nchi iwekwe sawa, tulieni hivyo hivyo
 
Mimi binafsi najisikia furaha sana, niliwaamini chadema, ila baada ya gia kubadiulishiwa hewani, nikamchagua tingatinga Magufuli. Sijawai kujuta na sitojuta.
Wale mlioshabikia ukawa mnajisikiaje sasa
Kwani kilo moja ya mchele unayo uziwa ww ni tofauti na mtu anaeshabikia ukawa???
 
Sijawahi kujutia uamzi wa kumpa magufuli kura yangu.
Nilimpigia Magufuli kama Magufuli si kufuta itikadi za vyama maana sina chama.
Wengi wetu hawajajua anacho fanya lakini baada ya muda wataelewa.
 
Mmh! Sipaoni pa kumfurahia wala kumchukia japo namba hazisomeki kotekote kwa tuliompa na wasiompa hatutofautiani.
Huogopi kuitwa mchochezi?
 
Dah...Mie najisikia furaha kubwa sana.. amechora mstari mbele kabisa unaowatenganisha wezi wa Mali ya umma na wazalendo...JPM amewatia rangi wezi, mafisadi na wajanjawanjanja..sasa hivi hata gizani unawatambua kiurahisi sana...long live JPM
 
Usilolijua ni usiku wa giza. Mimi naamini kuna waliompigia kura Magufuli wakijua watapata neema na maisha yao yatakua rahisi kama ilivyokua mwanzoni.

Natamani kupata maoni yao na kujua maisha wanayoishi sasa hivi. Poleni kwa mliojiaminisha goodlife inaweza kuwepo bila kuhangaika

Good day
Tuliompigia tunaona raha mstarehe kabisa na wala hatulalamiki isipokuwa kwa wale wanaoisoma namba na ambao hawakumpigia kura kama wewe ndio mnaolalamika
 
Pakua wimbo unaitwa SHILINGI wa kwake BEN POL feat. STEREO Kuna mstari unasema "Ushuani uswahilini usawa huu umekaba kama nini"
 
Back
Top Bottom