Nataka kuwashtaki waislam!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Wana jf, mimi siko vizuri sana na sheria naombeni ushauri kama inawezekana nikawashtaki viongozi wa msikiti ulio jirani na nyumbani kwangu maana kila ikikaribia saa kumi na moja alfajiri wanatoa sauti kubwa kwa kipaza sauti, ambayo huwa inanisababishia usumbufu mkubwa nikiwa nimelala kiasi kwamba nimeanza kufikiria kuuza kibanda changu ili kuepuka huu usumbufu

Kabla sijakimbia nataka nijue kama naweza kushtaki mahakamani ili waache kufanya hivyo. Je naweza kuwashtaki? niya yangu si fidia nataka court injunction wasiendelee na huo utaratibu.
 
Jaribu kusema nao one to one. Wasiposikia tafuta wakili mzuri, lazima zipo njia za kufungulia mashtaka
 
Msikiti nyumba ya pili hujui vya kukutana nao? Huna rafiki jirani hapo ambae ni Muislam akakusaidia kukukutanisha nao basi?
 
Mwalimu wangu siku hizi umenikimbia kweli.

Ile ilimu uliyokuwa unanipa umemkabidhi nani anifundishe. Achana na malumbano bana.
 
Msikiti nyumba ya pili hujui vya kukutana nao? Huna rafiki jirani hapo ambae ni Muislam akakusaidia kukukutanisha nao basi?

Nilikuwa naye lakini ananiita mimi kafiri nahisi kama ananitukana hivyo nimeamua kuachana naye
 
Wana jf, mimi siko vizuri sana na sheria naombeni ushauri kama inawezekana nikawashtaki viongozi wa msikiti ulio jirani na nyumbani kwangu maana kila ikikaribia saa kumi na moja alfajiri wanatoa sauti kubwa kwa kipaza sauti, ambayo huwa inanisababishia usumbufu mkubwa nikiwa nimelala kiasi kwamba nimeanza kufikiria kuuza kibanda changu ili kuepuka huu usumbufu, kabla sijakimbia nataka nijue kama naweza kushtaki mahakamani ili waache kufanya hivyo. Je naweza kuwashtaki? niya yangu si fidia nataka court injunction wasiendelee na huo utaratibu.

........ hiyo njia ukiipata na mie itanisaidia ! kuna Kanisa jirani yangu linaitwa "wapo" kila IJUMAA kuanzia saa nne usiku linamwagwa SEBENE mpaka asubuhi, ukizingatia KANISA lenyewe wameezeka mabati tu juu ili wasinyeshewe na mvua ! pia alipoona mgao waDOWANS unamzingua kafunga kinu kikubwa kweli cha kufua umeme, ili aliendeleze libeneke! Bora wewe unaamshwa, sie hatulali kabisaaaaa !!!!

:crying:
 
Hivi kwanini ibada ya mtu iwe adha kwa mwengine? Serikali inahitaji kufanya kitu hapo, na kama haifanyi, wananchi wachache watakapochukua hatua huenda tukapata afueni kidogo.
 
Wana jf, mimi siko vizuri sana na sheria naombeni ushauri kama inawezekana nikawashtaki viongozi wa msikiti ulio jirani na nyumbani kwangu maana kila ikikaribia saa kumi na moja alfajiri wanatoa sauti kubwa kwa kipaza sauti, ambayo huwa inanisababishia usumbufu mkubwa nikiwa nimelala kiasi kwamba nimeanza kufikiria kuuza kibanda changu ili kuepuka huu usumbufu, kabla sijakimbia nataka nijue kama naweza kushtaki mahakamani ili waache kufanya hivyo. Je naweza kuwashtaki? niya yangu si fidia nataka court injunction wasiendelee na huo utaratibu.

........... hiyo njia ukiipata na mie itanisaidia ! kuna Kanisa jirani yangu linaitwa "wapo" kila IJUMAA kuanzia saa nne usiku linamwagwa SEBENE mpaka asubuhi, ukizingatia KANISA lenyewe wameezeka mabati tu juu ili wasinyeshewe na mvua ! pia alipoona mgao waDOWANS unamzingua kafunga kinu kikubwa kweli cha kufua umeme, ili aliendeleze libeneke! Bora wewe unaamshwa, sie hatulali kabisaaaaa !!!!!:crying:
Hizo njia mkipata na mimi zitanisaidia kuna ma-bar na majirani wengine hawana ustaarabu kelele from dusk till dawn.... sijui kwanini wasitengeneze vyumba soundproof....
 
Wana jf, mimi siko vizuri sana na sheria naombeni ushauri kama inawezekana nikawashtaki viongozi wa msikiti ulio jirani na nyumbani kwangu maana kila ikikaribia saa kumi na moja alfajiri wanatoa sauti kubwa kwa kipaza sauti, ambayo huwa inanisababishia usumbufu mkubwa nikiwa nimelala kiasi kwamba nimeanza kufikiria kuuza kibanda changu ili kuepuka huu usumbufu, kabla sijakimbia nataka nijue kama naweza kushtaki mahakamani ili waache kufanya hivyo. Je naweza kuwashtaki? niya yangu si fidia nataka court injunction wasiendelee na huo utaratibu.

Waswis walishindwa waislamu less than percent itakuwa hapa mkuu, nakuhakikishia hilo huwezi mpaka kiama
 
Hizo njia mkipata na mimi zitanisaidia kuna ma-bar na majirani wengine hawana ustaarabu kelele from dusk till dawn.... sijui kwanini wasitengeneze vyumba soundproof....

Wafikishwe mahakamani basi tutapata amani. Watu wengine wagonjwa wanapata tabu hawapati kulala au watoto wachanga.
 
Waswis walishindwa waislamu less than percent itakuwa hapa mkuu, nakuhakikishia hilo huwezi mpaka kiama

Kwani wewe huoni kwamba hii ni antisocial behaviour..... imani au starehe zako kwanini ziwe usumbufu kwa wengine... kama ni kuamshana kila mtu ana alarm clock yake au wewe unasemje.?

Nikijenga Bar mlangoni kwako au nikiwa ninaimba kwaya au disco jirani yako wewe utapenda?
 
Wafikishwe mahakamani basi tutapata amani. Watu wengine wagonjwa wanapata tabu hawapati kulala au watoto wachanga.

Hii itakuwa ngumu njia bora ni kwa wananchi wenyewe kuongea na kuelezana kuwa huu sio ustaarabu na ni usumbufu kila kata inaweza ikafikisha malalamiko kwenye uongozi wa kata ili wote kwa pamoja walalamike hili sio suala la mtu mmoja....., hii issue haipo ninapokaa ila nimeshakwenda kuwatembelea baadhi ya ndugu zangu, nikajiuliza hivi hawa wanaishi vipi...
 
Kisheria kwa mujibu wa mipangomiji, hizo sehemu za staarehe hazitakiwi ziwe karibu na makazi ya watu.
Sheria hiyo inakiukwa sijui kwanini hapachukuliwi hatua rasmi kwa kweli.
 
Mm pale kwangu kuna kanisa ikifika saa kumbi na mbili jioni na asubuhi hupiga yale makengele yao wananikera sana

sasa ukipata suluhisho nisaidie na mm ni wakomowe hawa vibwengo
 
Kwani wewe huoni kwamba hii ni antisocial behaviour..... imani au starehe zako kwanini ziwe usumbufu kwa wengine... kama ni kuamshana kila mtu ana alarm clock yake au wewe unasemje.?

Nikijenga Bar mlangoni kwako au nikiwa ninaimba kwaya au disco jirani yako wewe utapenda?

Kuna mambo yanakubalika kuna mambo hayakubaliki.
 
Hoja yoyote inayoletwa humu inaonyesha huyo mleta ni mwenye akili ya namna gani au mtazamo gani??? Ni vema ukatumia ikiwezekana 1/1 ya AKILI zako kabla hujaanza kuandika hoja kwenye jf
 
Kwani wewe huoni kwamba hii ni antisocial behaviour..... imani au starehe zako kwanini ziwe usumbufu kwa wengine... kama ni kuamshana kila mtu ana alarm clock yake au wewe unasemje.?

Nikijenga Bar mlangoni kwako au nikiwa ninaimba kwaya au disco jirani yako wewe utapenda?

step 1: tafuta suluhu kistaarabu. ikishindikana nenda step 2

step 2: peleka malalamiko rasmi serikalini (ngazi yoyote). ikishindikana nenda step 3

step 3: tafuta msaada wa kisheria. ikishindikana nenda step 4

step 4: nunua kipaza sauti chenye sauti kali kuliko cha huyo unayemlalamikia. akiwasha chake, unawasha chako.

am sure step 4 itachochea uwezekano wa step 1 au/na step 2 kufanya kazi.

give it a shot!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom