Natafuta mchumba muathirika

Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.
Mkuu pole na mtihani ulio kupata. Ushauri wangu ni kwamba, waone wale jamaa wa ANGAZA au Njia Paanda (Cloud FM), kwa ushauri nasaha, ila sijui ofisi zao zipo wapi. Nadhani ukiulizia ulizia unaweza kuelekezwa wapi zilipo.
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

Hongera sana kwa ujasiri! Nimesoma post zote, fuatilia ya 3D. HIV ni situation na si ugonjwa! Have fun, don't think about it, enjoy life in a healthy manner na just remember since u posted this Uzi, watu wengi wamekufa na sio kwa HIV!
I hate people wanaona waathirika Kama ni watu wenye death sentence!
Utampata mwenzi, awe +ve or -ve lakini anayekupenda nawe utampenda! God bless you!
 
Mkuu pole na mtihani ulio kupata. Ushauri wangu ni kwamba, waone wale jamaa wa ANGAZA au Njia Paanda (Cloud FM), kwa ushauri nasaha, ila sijui ofisi zao zipo wapi. Nadhani ukiulizia ulizia unaweza kuelekezwa wapi zilipo.

Jamani, watoa lecturer; shida ya mtoa mada ni mchumba, preferably aliyeathirika.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kila la kheri mkuu
kila mtu anawake hapa dunianai..
saa nyingine tunawakataa, saa nyingine tunawaacha, na saa nyingine tuko nao
wako yupo endelea mbele kaza mwendo "don't give up na utafanikiwa...
Every thing is possible that's the beauty of living ...
 
unaweza hata oa ambae hajaathirika na usimwambukize mkuu,inategemea na umakini wenu
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

Tunaomba contact zako hapa kuna wachumba watatu wote wapo tayari na wanagombea nafasi hiyo sasa sijui unataka wa cd4 ngapi mana naona kuna mmoja kachoka hapa na angomea nafasi hiyo
 
Vijisenti, natanguliza shukurani kwako kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na Mungu wako. Sasa basi nakushauri ongea na Nafsi yako hai, utapata mchumba mwadilifu, atakayekupenda na kusaidia katika maisha yenu. Pia nakupa moyo, mkabidhi Mungu maisha yao utaona tofauti na maisha yako ya siku zote.

Kila la kheri!

Ahsante
 
Mkuu pole na mtihani ulio kupata. Ushauri wangu ni kwamba, waone wale jamaa wa ANGAZA au Njia Paanda (Cloud FM), kwa ushauri nasaha, ila sijui ofisi zao zipo wapi. Nadhani ukiulizia ulizia unaweza kuelekezwa wapi zilipo.

Ahsante, nimeshauriwa mambo mengi sana. Hata hivyo namshukuru Mungu ni saa oja ya kwanza tu ndio niliokuwa kwenye wakati mgumu lakini muda wote uliofuata niko kawaida hata hapa ninapokujibu sina wasiwasi niko kawaida kabisa ila sijui kama ni makosa ya washauri au ndio utaratibu wenyewe kwani sijashauriwa chochote kuhusu mahusiano.
 
Mkuu nimekushauri uwaone hao wataalam, kwani kupitia kwao, unaweza kufanikisha kusudio lako...!
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

ooh! Jamani! Pole sana.
Mungu akusaidie upate ukitakacho.
 
Nimegundulika nina virusi vya Ukimwi baada ya kwenda kupima kwa hiyari, sina tatizo lingine la kiafya pia nina cd4 za kutosha hivyo sijaanza kutumia dozi.

Mweleze pia bado una nguvu za kuchakachua kiukweli ukweli,ndo maana ni vizuri kumpata mwenzio ili usitangetange huku na kule na kuendeleea kuwaathili wadanganyika wengine...

Bravo kwa uamuzi mzuri huu!
 
Nimesoma comments zote, nimegundua kuwa somo la kutowanyanyapaa waathirika bado wengine hawalielewi, kuna watu wanachoongea na mtoa mada anachosema havihusiani, kuna wengine wana huruma sana yote kwa yote huyu vijisenti ni mstaarabu sana.
 
Swala si kuwa aliupataje jamani...tuache masihara yeyote laweza mfika. Tumshauri tu aweze kumpata ampendaye....sidhani kama kuna mtu ambaye hana ndugu au jamaa wa karibu aliyeathirika. Keep on.... utampata tu.
 
Hongera kwa kujitangaza ila mii ushauri wangu ni kwamba,kama huyo mchumba ukimpata basi tulia nae kwa sana na acha kabisa yale mambo yetu ya mabinti, kula matunda kwa wingi, fanya mazoezi, do this az b4, usifikirie sana hii kitu ukimwi,coz itakumaliza,cd4 zako hazitapungua na utaishi kwa matumaini sana!!

Sizinga ili suala si mchezo likikukuta, mpaka akili ikae sawa unakua umepitia mawazo ya aina yote. Naamini mpaka vijisenti kafika stage hiyo ya kujituma kupima na kuamua kutulia na kutafta mchumba hivyo vitu tayari anavitambua. issue iko kwa wale ambao hata wazo la kupima hana na kisha athirika.
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

Big up saana. May you achieve your goal na upate the wife you deserve.
 
unaweza hata oa ambae hajaathirika na usimwambukize mkuu,inategemea na umakini wenu

Akioa ambae hajaathirika kwa nia ya kuto muambukiza itawapa shida kidogo upande wa kupata mtoto. Imegundulika kua kwa uangalifu na umakini waathirika wanaweza za mtoto ambae haja athirika mradi wawai clinic.
 
Vijisenti, inatia moyo sana kusikia kutoka kwako jinsi ulivyolipokea hili. Kama walivyosema wengine...pengine ni muhimu pia kuendelea kujitambua wewe kama wewe kwanza kabla ya kujiwekea label ya uathirika. Hii label itakurudisha nyuma. Ni kweli kwamba huwezi kupingana na hali lakini isiwe ndio jambo la kuanzia wewe kutazamwa. Wagonjwa wa kisukari nao ni waathirika kama walivyo wa malaria, saratani na mengine mengi. Hebu endelea na maisha, piga mzigo, jitazamie afya yako, lishe bora. Mchumba atakuja kwa wakati, yule anayekufaa na pengine hata si huyo mwathirika unaemtafuta. Unaweza pata mwathirika na akakupa mateso ya moyo ile mbaya (ama furaha by the way). Kama ni wako atakukubali hata siku ukimwambia hali yako.
Kuna dada/mama mmoja anaitwa Asunta Wagura (unaweza kuangalia kazi zake kupitia google) kutoka Kenya, huwa nikisoma makala zake kila jumatano katika gazeti la Daily Nation nafarijika sana. Anaeleza vizuri mapito yake katika safari kama hii na kila siku huwa najifunza jambo jipya toka kwake. Nafikiri wale ambao bado wanarusha mawe wakati wanaishi kwenye nyumba za vioo wakisoma makala zake zitawasaidia. Ni elimu tu wanakosa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom