Natafuta mchumba muathirika

hapo kwenye RED, sijui nikupe hongera au thanks,
any way, natumaini utapata roho yako inachohitaji...ni vyema ungemtaarifu huyo aliyekuwa mpenzi wako ili awe makini siku zote, maana kama alikuwa tayari kwako, anaweza kuwa tayari kwa mwingine..

Ningeweza kumtaarifu lakini nafahamu vema tabia zake, katika mapungufu aliyo nayo ni pamoja na kukosa ustahimilivu hivyo atatangaza kwa watu bila kutumia busara.
 
Ingekuwa busara zaidi kama ungemfahamisha huyo mchumba ako wa mwanzo, kuliko kutoka mbio na sababu zingine, kama umeweza kuweka hii kitu hapa jamvini umeogopa nini kumwambia mchumba kwamba wewe ni muathirika??anyway kama alikuelewa its fine bt nahisi ume''break her heart indeed''.

Ndugu yangu, Heri ya Lawama kuliko fedheha hapa jamvini nimemudu kujianika kwa sababu nina GAMBA.
 
uliupataj pataje? pole sana ndugu yangu .

Swali gumu kidogo sina uhakika kama ni saluni au mchumba wangu wa awali ambaye alikufa kwa ajali ya gari. Nasema hivyo kwa sababu kabla hatujakutana kimwili tuliwahi kupima na wote tulikuwa hatuna maambukizi na sijawahi kukutana kimwili na yeyote baada ya kupima zaidi ya yule marehemu.
 
Pole sana mkuu, lakini hapo kwenye red mkuu, umenishtusha sana, hivi saluni nazo zinachangia maambukizi? ni hatari eeh!
 
Pole sana mkuu, lakini hapo kwenye red mkuu, umenishtusha sana, hivi saluni nazo zinachangia maambukizi? ni hatari eeh!

Sina uhakika labda nasikia kwa watu sijui kama kuna ukweli ndani yake nafikiri wanaofahamu watatupa majibu.
 
Pole ndugu! Naiman kwa mungu hakuna lisilowezekana. Hivyo usichoke kumwomba mungu. Mungu akutangulie.
 
Popote ulipo nenda ktk hospital uliza ward za waathirika/wenye ukimwi watakuonyesha jichagulie mwenyewe! Au nenda tume ya kudhibiti ukimwi watakusaidia kumpata mwandani wako!

we umeshapima eti? Umetema pumba na umedhalilisha hadhi yako. Jaribu kutumia busara kidogo unapochangia
 
Usimnyanyapae coz ni binadamu kama wewe, hakuna mwanaadamu aliyemkamilifu chini ya jua! Huwezi jua leo kwake na kesho itakuwa kwako. Au unadhani umekamilika kwa kiwango gani??
Popote ulipo nenda ktk hospital uliza ward za waathirika/wenye ukimwi watakuonyesha jichagulie mwenyewe! Au nenda tume ya kudhibiti ukimwi watakusaidia kumpata mwandani wako!
 
Swali gumu kidogo sina uhakika kama ni saluni au mchumba wangu wa awali ambaye alikufa kwa ajali ya gari. Nasema hivyo kwa sababu kabla hatujakutana kimwili tuliwahi kupima na wote tulikuwa hatuna maambukizi na sijawahi kukutana kimwili na yeyote baada ya kupima zaidi ya yule marehemu.

hizi tetesi za saluni nilizisikiaga siku nyingi. Watalaam tunaomba msimamo wenu mtushushe pressure tafadhali
 
Vijisenti, natanguliza shukurani kwako kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na Mungu wako. Sasa basi nakushauri ongea na Nafsi yako hai, utapata mchumba mwadilifu, atakayekupenda na kusaidia katika maisha yenu. Pia nakupa moyo, mkabidhi Mungu maisha yao utaona tofauti na maisha yako ya siku zote.

Kila la kheri!
 
Mungu akubariki kwa kumfikiria mwenzako na kutotaka kumuambukiza

ILA
Kuna tatizo wengi watu hawaelewi mie nimesumuliwa na wanaoelewa virusi

Kuna aina mbili ya vijidudu hivyo na kwa sasa unajisikia bado unaafya yako hivyo unaweza kuwa na vijidudu niseme A ukaenda kulala na mwenye vijidudu B hapo ndugu yangu vyote hivyo A na B vikichanganyika ndugu yangu tayarisha jeneza mapema

Kwa hiyo ni vyema kuendelea kujilinga ili usije kutana na mwenye vidudu vya aina isiyo kwako

I hope hii itasaidia katika maisha yako. Wengi wana dhani unavyofikiri na zaidi bila kujua kuwa kuna kujiumiza zaidi na imewakuta wengi sana na wangeweza kuwa hai hadi leo
 
Huu sio wakati wa kuangalia mwenzako alipojikwaa bali ni kumshauri zaidi nini afanye kwa maisha yake ya baadae
 
pole sana usife moyo, kuwa na imani,, hii dunia wote tunapita,
ila mimi makushukuru kwa uamuzi uliochukuwa wa kutotaka kuambiza wengine
ubalikiwe kwa hilo.
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

Pole Mkuu. Sikupi pole kwa sababu ya HIV ila kwa sababu ya wanyanyapaaji na jinsi ambavyo wanaweza kukutisha na ukatishika. Aidha sikusudii kukupa moyo. Nakusudia kukwambia ukweli. Kufa, au kufa mapema hakuna uhusiano wa moja kwa kwa moja na kuwa na HIV ila kuna uhusiano na uzushi wa wanajamii na hofu/upweke ambao wewe utauruhusu. Cha msingi, kwanza kubali una HIV, ndugu ukishaweza hili utakuwa umejiongezea miaka kama 35 hivi, kwa kukubali hili tu. Pili cheki afya yako kwa namna unavyoshauriwa hospitali. Tatu ukishapata mwenza ambaye naye anafuata masharti ya hospitali na ana afya ya kawaida safi sana, tena sana. Nne, endelea na mipango yako ya kimaisha, jenga nyumba, nunua gari, shabikia Manchester UTD (kwanini ushabikie Arsenal wakati hawachukui vikombe?), endela na biashara zako, enfdelea kupiga pamba, endelea na ubishi wako wa siasa, endelea na masihara yako, endelea kumwamini Mungu, endelea na ucheshi wako, endelea kuwa member JF, endelea kuwa Rafiki Yangu. Bora mtu akukatishe tamaa kuliko wewe kujikatisha. Nina bro wangu ambaye tunajua ni HIV+ for about 13 yrs now. Tuko naye na wala huwa hatuwazi kuwa ni HIV+ zaidi ya kubishana naye juu ya mambo ya siasa.

Pole sana mkuu, lakini hapo kwenye red mkuu, umenishtusha sana, hivi saluni nazo zinachangia maambukizi? ni hatari eeh!

hizi tetesi za saluni nilizisikiaga siku nyingi. Watalaam tunaomba msimamo wenu mtushushe pressure tafadhali

Hakuna ushahidi wa uhakika kuwa saluni zinaambukiza. Mazingira ya mtu kuambukizwa saluni ni lazima kwanza mnyoaji wa kwanza (HIV+) akatwe na mashine kiwango cha kutoka damu japo kidogo na mnyoaji wa pili anyolewe haraka sana may be within seconds, naye akatwe ili aambukizwe na wakati huo huo mtu wa saluni asiwe amepaka mashine spirit wala poda wala delay yoyoye. Jambo hili halitokei katika mazingira ya kawaida. Hivyo ukiambukizwa very likely ni mazingira mengine na si saluni, la msingi hakikisha mwenye saluni anasafisha mashine walau kwa poda kabla haujanyolewa wewe. Ikumbukwe pia mashine hizi hupata joto na hewa ya oksijeni ambapo virusi havivumilii mazingira haya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom