Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883

Serikali imeona kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusu taarifa za Wasafi FM kuzuia mahojiano kati ya Makamu Mwenyekiti, wa CHADEMA na kutoa taarifa kuwa maamuzi hayo yametokana na maelekezo kutoka juu.

Tangu kuingia kwa Serikali ya Awamu ya Sita kazini, jambo la kwanza alilofanya ni kufungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa na kutoa maelezo kuwa Wizara ya Habari ihakikishe kunakuwa na uhuru wa vyombo vya habari. Pia Mheshimiwa Rais amehakikisha uwepo wa demokrasia nchini ikiwemo uhuru wa watu wote kuwa huru kuzungumza bila kuzuiwa mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa vyama vyote vya siasa.

Kutokana na nia yake njema, Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yake aliagiza Wizara pia kuangalia ustawi wa vyombo vya habari kiuchumi na Wizara kuunda kamati ya kutathmini Hali ya Uchumi wa Vyombo vya Habari nchini. Kutokana na nia njema aliyonayo Mhe. Rais, hakuna uwezekano wa maelekezo yeyote ya kuingilia uhuru ambao amekuwa akiamini na kuujenga kwa vyombo vya habari nchini.

Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari kama dira yake ya kuendeleza dhana yake nzima ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi Kujenga Utaifa (4R Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuild). Serikali inawataka Wasafi media waseme ukweli kuhusu nini kimetokea, kwani Serikali haijatoa maelekezo yeyote kuhusu mahojiano hayo.

Imetolewa na WHMTH
Screenshot 2024-02-07 at 14-33-04 CamScanner 02-07-2024 14.20(1) - CamScanner 02-07-2024 14.20...png

Pia soma: Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

2. Tundu Lissu atakuwepo kwenye good Morning ya Wasafi FM kesho asubuhi...
 
View attachment 2897005

Pia soma: Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

2. Tundu Lissu atakuwepo kwenye good Morning ya Wasafi FM kesho asubuhi...
Wacha utoto
JamiiForums-1516604969~2.jpg
 
serikali au CCM tunajua serikali ya sasa iko answerable kwa CCM na ndio maana Makonda anaamrisha mawaziri na wanatema jasho vibaya mno
 
Hapo ni shida ni walio andaa kipindi bila kuwajuza wenye TV sasa jamaa wamekizuia wala hawajaambiwa na serikali…labda wameona wanakwenda kupata adhabu kutokana na watakaye muhoji ata hatarisha maslai ya kituo chao…Kimsingi wampigie Diamond kwanini amezuia kipindi maana yeye ndio ameweka hela hapo na ana jua uchungu wa kupoteza hela!
 
Back
Top Bottom