Nape Nnauye atulizwa, ateuliwa DC Masasi

BADO tAMBWE hIZA NA mSABAHA ;MAMLUKI TOKA cuf!! Wameumizana sana kwemnye kura za maoni sijui atawapoza wangapi kwani wako wengi mno walioumia; ukianzia kwa wakina Kamala mpaka wakina Mwantumu Mahiza na hapo bado wakina Sarungi na wakina makwetta!! Jamaa kazi anayo.
 
Hongera kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya? Hii ni mojawapo ya zile kazi Jenerali anaita za kitarishi. By the way, ni nini kazi ya Mkuu wa Wilaya?
 
Jamani dada Shy-Rose Bangi asisahaulike jamani!

Shyrose angebaki tu na kazi yake naamini inamlipa vizuri ajitahidi kuwa hardworking...ukuu wa wilaya ubaya ni kuteuliwa bila taarifa na kuachishwa bila majadiliano....
 
Kiukweli nafurahi kuona vijana wanapewa madaraka makubwa kwani Nape ataingia katika list ya maD.C vijana ninaowajua wakina isack fransis...Fatma Ally,Fatma Mwasa,Sophia Mjema,Erasto Sima na Halima wa kilosa...pia kuna yule dk Norman....wengine siwakumbuki....ila VIJANA HOYEEEEE!!
 
Kiukweli nafurahi kuona vijana wanapewa madaraka makubwa kwani Nape ataingia katika list ya maD.C vijana ninaowajua wakina isack fransis...Fatma Ally,Fatma Mwasa,Sophia Mjema,Erasto Sima na Halima wa kilosa...pia kuna yule dk Norman....wengine siwakumbuki....ila VIJANA HOYEEEEE!!

Mhhh,

Sina hakika kama kuna cha kushangilia. Naona ni kama mchezo wa kumtuoia mtoto mwanasesere ili aache kukupigia kelele. Sina hakika kama wakuu walikuwa wanafurahia kukaa kwake mjini!
 
Nape Nnauye ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi
Benjamin Sawe
Maelezo
Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua ndugu Nape Moses Nnauye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Bwana Nnauye amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Said Ali Amanzi ambaye amebadilishiwa kituo chake cha kazi na kuhamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Kabla ya uteuzi huo Ndugu Nnauye alikuwa ni Katibu Msaidizi Idara ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa CCM Makuu Dar es Salaam wakati Bwana Said Ali Amanzi amechukua nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Ndugu Cleopas Rugarabamu ambaye alifariki mwezi Julai mwaka huu akiwa kwenye matibabu nchini India.
Uteuzi na uhamisho huo unaanza tarehe 10/9/2010.
Mwisho
 
Back
Top Bottom