Nape Nnauye atajwa kuandaliwa kuwa Katibu Mkuu CCM

Hawa ni watu wawili tofauti sio tu kielimu bali hata kimakuzi, kimalezi na uwezo wa kuongoza. Katibu Mkuu wa CCM ajaye ni Dr Asha-Rose Migiro. Wanasheria wengi ni makatibu wazuri sana.

Uanasheria wake utafua dafu kwenye mfumo na kundi litakalomwingiza madarakani?
 
Kila la Heri na Iyo 1st ElevEn yao Mpya ...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mkuu hao 5000 walioomba wamesukumwa na nia ya dhati ya kuongoza, tamaa ya madaraka, matumbo au kukomoana?
Maana haifai tu kutaja idadi ya waombaji. Ukijitendea haki kujijibu nia hasa ya waombaji utajua kama chama kinakufa au la
Muhimu ni kwamba ni WATANZANIA wenzetu wa aina zote walioomba UONGOZI ndani ya CCM. Ni nini kiliwasukuma kufanya hivo hilo tuwaachie wao wenyewe. Idadi hiyo ni kubwa kwa chama chochote cha SIASA nchi hii. UHAI wa chama ni wanachama na vikao.
 
Mh! kwa ccm yote yanawezekana
Gazeti la RAI toleo la leo limeripoti habari linazodai ni za uhakika na kutoka ndani ya chanzo cha uhakika kwamba Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye anaandaliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kuchukua nafasi ya Willson Mukama.

Pia Dr Asha-Rose Migiro inadaiwa atateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kuchukua nafasi ya Mzee Pius Msekwa.

Nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi anatarajiwa kuwa William Ngeleja Mbunge wa Sengerema na aliyewahi kuwa waziri wa Nishati na Madini.

Ukweli wa taarifa hizi unaonekana ni wa uhakika kwa sababu Nape Nnauye na Asha Migiro hawajagombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.


 
Muhimu ni kwamba ni WATANZANIA wenzetu wa aina zote walioomba UONGOZI ndani ya CCM. Ni nini kiliwasukuma kufanya hivo hilo tuwaachie wao wenyewe. Idadi hiyo ni kubwa kwa chama chochote cha SIASA nchi hii. UHAI wa chama ni wanachama na vikao.

Hakuna anayefuatilia siasa za nchi hii atakayesema CCM inakufa kwa kupungukiwa wanachama. Kifo cha CCM ni kifo cha kimfumo na ndio kifo kibaya kwa chama chochote cha siasa. Sisiem walitumia njia hii kuiua NCCR, na sasa ugonjwa huo walioupandikiza upinzani unawatafuna wenyewe
 
Uzuri mmoja wa huyu mama ana akili na mawazo yanayojitegemea. Haogopi. Hatishwi na sio mwekezaji kwenye SIASA. Hana makundi.

Ni sawa. Hata mimi nakukubalia hoja yako. Lakini akiendelea na attitude hiyo system itam-phase out
 
Waliojaza fomu kuomba UONGOZI ndani ya CCM kuanzia ngazi ya wilaya hadi NEC-TAIFA ni zaidi ya elfu tano. Hiki ni chama cha kufa leo au kesho kweli? Na hapo haujaweka idadi ya waliogombea kwenye ngazi za mashina, matawi na kata ambao ni wengi zaidi ya hawa wa ngazi kubwa.

Hiki chama kipo sana tu na namna moja ya kupambana nacho sio kufikiri au kuota tu kwamba kinakufa. Mtakuwa mnajidanganya kwa sana tu au hampo ndani ya TANZANIA. Kumbukeni pia kwamba CCM kiliundwa na mtu makini sana.

Kwenye nchi ya watu million karibu 40 kupata vichaa 5,000 kugombea chama mfu si tabu sana !

Hahaaaaah ! ni magoigoi wa fikra tu wanaweza kuyaona maisha ya ccm yakiwa marefu ! Chama kinachobembeleza wasomi kujiunga nacho , chama kinacghostuka kuona msomi anagombea , hakiwezi kuwa chama chenye Umri wa Kutosha , kinakaribia Kufa na kuzikwa.
 
Hakuna anayefuatilia siasa za nchi hii atakayesema CCM inakufa kwa kupungukiwa wanachama. Kifo cha CCM ni kifo cha kimfumo na ndio kifo kibaya kwa chama chochote cha siasa. Sisiem walitumia njia hii kuiua NCCR, na sasa ugonjwa huo walioupandikiza upinzani unawatafuna wenyewe
Mfumo wowote wa chama cha SIASA unatengenezwa/unarekebishwa na:
-Chaguzi kama hizi. Unapata VIONGOZI wapya sanjari na mawazo mapya pia;
-Vikao. Hakuna chama kingine cha siasa nchi hii kinaifuata na kuitekeleza vizuri kalenda yake kama CCM;
-Mapato. CCM kwa sasa inakomba kwenye hazina yetu zaidi ya bilioni moja kila mwezi kama ruzuku;
-Mawasiliano. Hakuna chama chenye mawasiliano mazuri na wanachama wake kama CCM.
 
Angekuwa na akili asingeshindwa vibaya kutekeleza majukumu yake UN hadi Ban Ki Moon akaamua kum-fire!
Hii uliisikia kwa Ban Ki Moon mwenyewe? Nilichokisikia mimi hata Ban mwenyewe alikuwa aondoke akabembelezwa na Marekani kwa kuwa hana madhara kwao.
 
Kwenye nchi ya watu million karibu 40 kupata vichaa 5,000 kugombea chama mfu si tabu sana !

Hahaaaaah ! ni magoigoi wa fikra tu wanaweza kuyaona maisha ya ccm yakiwa marefu ! Chama kinachobembeleza wasomi kujiunga nacho , chama kinacghostuka kuona msomi anagombea , hakiwezi kuwa chama chenye Umri wa Kutosha , kinakaribia Kufa na kuzikwa.
Kwenye hawa 5000 wamo maDr wa shule na watiba; wa Digrii mbili lukuki; wa darasa la saba tu; watanzania wa nyanja zote; makabila yote; dini zote; rika zote; hata vichaa wamo pia.
 
Alhamisi, Septemba 27, 2012 10:12 Na Mwandishi Wetu


*Migiro Makamu Mwenyekiti
*Nape Katibu Mkuu
*Ngeleja Katibu Mwenezi

UONGOZI mpya wa CCM sasa uko ndani ya bahasha. Kilichobaki ni uamuzi wa kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC ) kufungua bahasha hiyo na kuweka siri hiyo wazi.

Kumalizika kwa vikao vikuu vya chama kunatoa taswira ya uongozi mpya wa CCM, hasa kuzingatia kilio cha muda mrefu kutoka kwa wanachama kuisihi CCM irejee kwenye uasilia wake.

Sasa ni sura mpya na taswira mpya. Kauli ya Mwenyekiti Taifa, Rais Kikwete kuwa "Hatuwezi kuwa na Chama cha wazee tu, hapana, tumeona tuwape nafasi vijana wengi, tena wasomi waweze kugombea…Ni muhimu kupata sura mpya ya chama na taswira mpya kwa kuingiza wasomi", ni kauli inayoashiria mabadiliko makubwa katika CCM yanayotarajiwa.

Anaendelea kusisitiza akiwaeleza wajumbe wa NEC, kuwa "lengo ni kuunda timu ya ushindi ya Chama kwa mwaka 2014 katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, na mwaka 2015 katika Uchaguzi Mkuu."

Nasaha kwa wale "wenye ndimimbili" anasema kuwa "isiwe nongwa ukiwa basi ni kulalamikia chama hiki kimefanya nini, ukishafikia hivyo wewe haukuwa na moyo na chama ila moyo wako ulikuwa na shida ya uongozi."

Wakati hali ikijiri hivyo, hali ndani ya chama inaripotiwa kuwa ni tulivu hata mara baada ya kupita panga la kung'oa visiki, hii ikiashiria kuwa sasa chama kinajivua ‘gamba', na hii imepokewa kwa shangwe na furaha na wana-CCM wengi.

Watu wanaanza kupata matumaini makubwa, hasa wanachama na wananchi waliokuwa wameanza kupoteza matumaini.

Chanzo kutoka ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu Taifa ( NEC ) kilisema hali ndani na nje ya ukumbi imepokewa vizuri kutoka kwa watu wa kada mbalimbali ambao wametoa mawazo yao kuhusu matokeo ya kuchuja majina ya wagombea ndani ya CCM, na kutemwa kwa baadhi yao, hasa wanaodhaniwa wamekosa maadili na mwalekeo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kuhusu uchujaji na upitishaji wa majina ya wagombea kuanzia Kamati ya Maadili, Kamati Kuu ( CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC ) zinasema kazi ya kupitia majina imekamilika na ilikuwa ngumu.

Kazi ya kupitia majina ya wagombea ilifanywa na Kamati ya Maadili kupitia majina ya waliopendekezwa na vikao kutoka wilayani na mikoani.

Imeelezwa kuwa idadi ya wagombea 2,853 waliomba kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama, na wengine 2,104 waliomba nafasi za uongozi kupitia jumuiya za Chama. Vikao vyote vilifanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama.

Matazamio ya wananchi wengi ni kuona wajumbe wa vikao hivyo wanafanya uchaguzi sahihi na makini kupata watu watakaoleta mabadiliko makubwa na kuwa viongozi bora katika chama hicho, ambao watakuwa na uwezo na dhamira ya kweli ya kusimamia sera na kuwa wabunifu wa mikakati ya kukuza uchumi na kuhakikisha serikali inatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

Moja ya safu ambayo ni nguzo na muhimili ni nafasi ya wasaidizi wa karibu wa Mwenyekiti Taifa, wakiwamo Makamu wa Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi.

Katika Chama, hao wanaelezwa na wachambuzi wa masuala ya siasa kuwa ndio hasa wana uzito wa pekee wa kuwezesha kupeperusha vyema bendera ya chama na kuiaminisha CCM katika jamii ndani na nje ili iendelee kukubalika.

Tathmini, utafiti na uchambuzi unaonyesha kuwa upepo unavuma kuwaelekea aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro, kushika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti Tanzania Bara, Katibu Mkuu kuwa Nape Nnauye na Katibu Mwenezi na Itikadi ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kushika nafasi ya Nape ili kwa pamoja wasukume mbele gurundu la CCM hadi mwaka 2015.

Imeelezwa kuwa CCM sasa inataka kuwa na viongozi wenye uadilifu, shupavu, hodari na wenye kukitetea chama. Aidha, kuwa na timu ya ushindi wa chama na si ushindi wa mtu binafsi, na kuachana na viongozi wenye ndimimbili.

Wachambuzi hao wa siasa na tathmini wanaeleza kuwa chama kiendelee kuwa taasisi si mtu kuwa zaidi au juu ya chama, dhana ambayo ni potofu.

Nukuu ya Baba wa Taifa inawakumbusha wajumbe wa Kamati ya Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa kwamba, "chama dhaifu huzaa serikali dhaifu".

 
aiseeee bora ngeleja arudi kwenye siasa....alikuwa amepumzishwa mapema mno
shakebutt.gif
 

Lakini sikuliona JINA la ASHA-ROSE MIGIRO kwenye nafasi zozote za kugombea CCM-NEC POSITIONS...

Pia Sikuliona JINA LA NAPE NNAUYE kwenye Nafasi zinazogombewa...

Na Huyu Kaka yetu NGELEJA ?

HII SIO KWELI KABISA... Wataigonga CHINI CCM...
 
wanaangamia kwa kukosa maarifa jamani!wanamacho hawoni,wanamasikio hawsikii.wanawaza kuiba tu.tuweni makaini wananchi.
 
Back
Top Bottom