Nape: Huoni tofauti kati ya kauli yako na Dr. Slaa?

Ningependa kujua kutoka kwa Nape - Katibu Mwenezi CCM kama haoni tofauti ya kauli aliyoitoa mwezi uliopita kuwa CHADEMA kimepata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili wake kutoka nje ili kufanikisha M4C na ile aliyoitoa juzi Dr Slaa - Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa chama chake ni moja ya vyama vya siasa ikiwemo CCM vinapata ufadhili kutoka nje wa kujijengea uwezo?

Natoa hoja hii kwa kuwa nimemsikia leo Radio One akijiandaa kutumia kauli ya Dr. Slaa kama utetezi wake mahakamani alikoburuzwa na CHADEMA ili athibitishe kauli yake!

USHAURI: Namshauri Nape aweze kuchemsha bongo lake kidogo ili aweze kutofautisha hoja ambazo zina implication ya kisheria vinginevyo atakiliza chama chake CCM!

Hata mimi nimemsikia NAPE,nafikiri anadhani CHADEMA na hasa Dr Slaa ni watu wenye kufikiria hovyo na wenye uelewa mdogo kama yeye. Nina amini NAPE ametegwa kirahisi sana na CHADEMA watammaliza muda si mrefu. Kuna tofauti sana katika kauli aliyosema NAPE na alichoongea Dr Slaa..na CHADEMA walijua NAPE atadandia hoja ya Dr na yet Dr ikabidi aongee tu ili yatimie..Hivi unaweza kwenda kusema mahakamani ndiyo wanafadhiliwa kutoka nje na ushahidi ni maneno ya Dr ? Hivi kweli utashinda kesi kwa kipuuzi namna hii? yaani maneno ya Dr ndio ushahidi tena yaliyotoka baada ya kauli yako? NAPE ataangukia pabaya sana,nafikiri bado hajajua kutumia vizuri akili zake chache kufikiria vizuri..Tusubiri
 
Hivi kwa nini hatuwezi kujadili bila kuweka imani za watu?

Kwanini tutumike kuwa gawa watanzania?

Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!
 
Binafsi sioni mantiki ya CDM kumpeleka Nape mahakamani kwa upuuzi kama huu
Ni ukweli ambao hatutaki kuukubali kwamba hii kesi kwa na nape ni kama kumsukuma mlevi chini
Hapo kabla CDM hakikuwahi kukiri hadharani kuwa kinapokea kiasi chochote cha pesa kutoka nje ya nchi, na baada ya Nape kupata taarifa CDM wanapata mgao kutoka nje ambao hata yeye anajua wanapata kwenye chama chake lakini akaamua kuutumia ukimya huo wa CDM kuwa wanapataa fedha toka kwa wafadhili na ndio inawatia kiburi ya M4C
Ukweli ni kwamba CDM wanapokea pesa kwa wafadhili na sio dhambi, na swala la kuvuruga amani anaweza kudai ni mara ngapi CDM wamedai nchi haitawaliki tena?

Sioni mantiki yoyote ya maana hapa katika hili
Sasa sijui haya mambo ya idadi ya pesa na zinatumikaje sio issue kwenye matamshi ya kisiasa
Utakuwa huna kumbukumbu nzuri,hii sio mara ya kwanza CDM kutoa ufafanuzi,kumbuka semina za kunduchi beach hotel.CDM walikuwa pale na CCM pia,na maneno yalikuwa kama haya sasa.
 
Binafsi sioni mantiki ya CDM kumpeleka Nape mahakamani kwa upuuzi kama huu
Ni ukweli ambao hatutaki kuukubali kwamba hii kesi kwa na nape ni kama kumsukuma mlevi chini
Hapo kabla CDM hakikuwahi kukiri hadharani kuwa kinapokea kiasi chochote cha pesa kutoka nje ya nchi, na baada ya Nape kupata taarifa CDM wanapata mgao kutoka nje ambao hata yeye anajua wanapata kwenye chama chake lakini akaamua kuutumia ukimya huo wa CDM kuwa wanapataa fedha toka kwa wafadhili na ndio inawatia kiburi ya M4C
Ukweli ni kwamba CDM wanapokea pesa kwa wafadhili na sio dhambi, na swala la kuvuruga amani anaweza kudai ni mara

ngapi CDM wamedai nchi haitawaliki tena?

Sioni mantiki yoyote ya maana hapa katika hili
Sasa sijui haya mambo ya idadi ya pesa na zinatumikaje sio issue kwenye matamshi ya kisiasa

Sababu ya kushitaki ipo,nafikiri na wewe mjadala haujakuingia sawa sawa
 
Binafsi sioni mantiki ya CDM kumpeleka Nape mahakamani kwa upuuzi kama huu
Ni ukweli ambao hatutaki kuukubali kwamba hii kesi kwa na nape ni kama kumsukuma mlevi chini
Hapo kabla CDM hakikuwahi kukiri hadharani kuwa kinapokea kiasi chochote cha pesa kutoka nje ya nchi, na baada ya Nape kupata taarifa CDM wanapata mgao kutoka nje ambao hata yeye anajua wanapata kwenye chama chake lakini akaamua kuutumia ukimya huo wa CDM kuwa wanapataa fedha toka kwa wafadhili na ndio inawatia kiburi ya M4C
Ukweli ni kwamba CDM wanapokea pesa kwa wafadhili na sio dhambi, na swala la kuvuruga amani anaweza kudai ni mara ngapi CDM wamedai nchi haitawaliki tena?

Sioni mantiki yoyote ya maana hapa katika hili
Sasa sijui haya mambo ya idadi ya pesa na zinatumikaje sio issue kwenye matamshi ya kisiasa

kutokana na maelezo yako aither kuna kitu huelewi ama hukusikia kauli yanape vizuri ama ulisikia lakini hukuelewa
ishu kubwa sio kupata hela kutoka nje yanchi , Maneno yanape yalikua makali sana na hata kwawatu wenyebusara tuliliangalia marambili na kama chadema wasingefungua kesi mahakamani watu wangewezakuamini

ubaya wa maneno ya nape unakuja pale alipo sema chadema wanapata misaada nje nakuiweka nchi rehani (yaaani kwamaneno mengine nape anataka kutuambia chadema wanauza Tanzania kwamisaada wanayopokea) na hicho ndo anachotakiwa kuthibitisha
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Heh huyu nae vipi na katokea wapi na udini wake?!!!
 
aaaah huyu dogo anajamba tu humu jf.kacheze kombolela na watoto wenzako nje.unaongelea udini?shame on you.
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Udini udini udini, shauri yako na endeleza dudu hili kwa juhudi zako zote but matokeo yake hata ukiwa kaburini hayatasahaulika.
 
Anakakesi nyingine ya kujibu mahakamani kwakusema Dr. Slaa anazeeka vibaya! CHANZO: NAPE MNAUYE THIS MORINING FROM REDIO ONE NIPASHE! (14/09/2012)
 
.................well said bro, ''Wanasiasa wengine nafikiri ni wapuuzi fulani tu''.....Nape ni mfano halisi wa hao wanasiasa. Nina imani siku moja atakuja kujutia kwa jinsi anavyokubali kutumiwa kizembe namna hii. Ajifunze mfano mzuri ni kwa yule askari ambaye aliuwa mwandishi Nyololo-Iringa, bila shaka alipewa maelezo kutoka kwa wakuu wake na baada ya tukioo wakajaribu kuficha ukweli ila walivyoona mambo yamekuwa magumu sasa hivi wameamua kumtoa kafara yule policcm. Hali itakuwa vivyo hivyo kwa kijana mwenzetu Nape ambaye anaburuzwa na vizee kwa manufaa yao.

Ni houseboy wachama! kuna viongozi wakubwa wa ccm wanautumia mdomo na meno yake kutafunia mchanga na yeye hajashtuka bado kwasababu ya kiherehere na njaa zake.
 
Nape ni Kielelezo cha ccm kuishiwa watu wa kushika nyadhifa za juu katika Chama ! na ndio maana huyo poyoyo anawiza na punguzni mwingine Le Mutu sijui ! wote ni Wajinga , wazembe na Wavivu.
 
nape hana jipya huku ni kuhaha tu sheria ngoja imunyoshe kwanza maana anajifanya anajua kumbe bwenge
 
Tatizo la Nape ni Jazba.

TATIZO SIO NAPE, Pale Dr Slaa (PHd) ametumia kitu kinachoitwa offside trick. Nape naye Kwa uvivu wake wa kufikiria (au kwa kutumia kiungo kingine badala ya ubongo kufikiria) akaja na jibu rahisi kwenye hoja nzito. Ameshaingia kichwa kichwa. Hapa akikutana na wazee wa hoja nzito,wanasheria waliobobea(Lissu, Safari, Marando, N.k.) jasho litamtoka mpaka sehemu ambazo hazistahili kutoka jasho. Ngoja akaumbuke na magamba wenzake huko high court. M4C 4REVER
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Shinto, unajua maana ya wizi???? Je Tanzania imekuwa haipokei misaada kwa watu au mashirika ya Kikristo?? We vipi? Mbaya zaidi CCM imekuwa ikipokea hela kutoka chama cha EPA
 
Back
Top Bottom