Nape: Huoni tofauti kati ya kauli yako na Dr. Slaa?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,797
12,239
Ningependa kujua kutoka kwa Nape - Katibu Mwenezi CCM kama haoni tofauti ya kauli aliyoitoa mwezi uliopita kuwa CHADEMA kimepata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili wake kutoka nje ili kufanikisha M4C na ile aliyoitoa juzi Dr Slaa - Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa chama chake ni moja ya vyama vya siasa ikiwemo CCM vinapata ufadhili kutoka nje wa kujijengea uwezo?

Natoa hoja hii kwa kuwa nimemsikia leo Radio One akijiandaa kutumia kauli ya Dr. Slaa kama utetezi wake mahakamani alikoburuzwa na CHADEMA ili athibitishe kauli yake!

USHAURI: Namshauri Nape aweze kuchemsha bongo lake kidogo ili aweze kutofautisha hoja ambazo zina implication ya kisheria vinginevyo atakiliza chama chake CCM!
 
Huyo Nape amekwisha kwenda alijojo asubiri huruma ya CDM tu, maana hata hao waliomtuma wamekula kona awakutegemea watu watafika mahakamani
 
Mkuu, unapoteza muda tu, hawa magamba wanayo namna yao nyingine ya kufikiri, hawatumii kabisa Ubongo huu kama wako, nenda umsikilize Mchemba kule Igunga, utakimbia!
 
Mkuu hata mimi baada ya kusikia kauli ya Nape leo Radio One nilishangaa mno! Sio tu kwamba kanukuu maneno ya Dr. Slaa exactly kama uliyoeleza kwenye post yako bali pia kakiri kwamba hata CCM inapokea misaada kutoka kwa vyama rafiki vya nje kwa ajili ya KUJIJENGEA UWEZO. Kwa kauli hii nilishindwa kabisa kumwelewa huyu dogo.

Hivi issue inakuwa kosa kwa kuwa tu Chadema nao wanapata hiyo misaada bali kwa CCM haina tatizo? Hoja kuu iliyopelekea Chadema kumshitaki ni "CHADEMA inapokea MABILIONI kutoka nje kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi"; hili hajalizungumzia kabisa bali hiyo hoja nyepesi na ya kitoto. Wanasiasa wengine nafikiri ni wapuuzi fulani tu.
 
Shida ya kuwa mwanasisiem unalazimishwa kutumia sehemu nyingine ya mwili wako kufikiri badala ya ubongo kama binadam wengine. Pole sana Nape
 
Baada ya Dr.Kafumu kutelekezwa mahakamani, sasa ni zamu yake.
 
Mtaalamu wa kupiga magitaa yeye na sheria wapi na wapi? Nepi hajui legal grounds.
 
Mkuu hata mimi baada ya kusikia kauli ya Nape leo Radio One nilishangaa mno! Sio tu kwamba kanukuu maneno ya Dr. Slaa exactly kama uliyoeleza kwenye post yako bali pia kakiri kwamba hata CCM inapokea misaada kutoka kwa vyama rafiki vya nje kwa ajili ya KUJIJENGEA UWEZO. Kwa kauli hii nilishindwa kabisa kumwelewa huyu dogo. Hivi issue inakuwa kosa kwa kuwa tu Chadema nao wanapata hiyo misaada bali kwa CCM haina tatizo? Hoja kuu iliyopelekea Chadema kumshitaki ni "CHADEMA inapokea MABILIONI kutoka nje kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi"; hili hajalizungumzia kabisa bali hiyo hoja nyepesi na ya kitoto. Wanasiasa wengine nafikiri ni wapuuzi fulani tu.
.................well said bro, ''Wanasiasa wengine nafikiri ni wapuuzi fulani tu''.....Nape ni mfano halisi wa hao wanasiasa. Nina imani siku moja atakuja kujutia kwa jinsi anavyokubali kutumiwa kizembe namna hii. Ajifunze mfano mzuri ni kwa yule askari ambaye aliuwa mwandishi Nyololo-Iringa, bila shaka alipewa maelezo kutoka kwa wakuu wake na baada ya tukioo wakajaribu kuficha ukweli ila walivyoona mambo yamekuwa magumu sasa hivi wameamua kumtoa kafara yule policcm. Hali itakuwa vivyo hivyo kwa kijana mwenzetu Nape ambaye anaburuzwa na vizee kwa manufaa yao.
 
Kenge huwa hasikii mpaka umtandike hadi damu zimtoke masikioni ndo ataskia.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu, unapoteza muda tu, hawa magamba wanayo namna yao nyingine ya kufikiri, hawatumii kabisa Ubongo huu kama wako, nenda umsikilize Mchemba kule Igunga, utakimbia!

Kwa sasa siwezi kwenda Igunga kwa kuwa nitatenda kosa la jinai kumcharaza Mchemba hadharani!
 
Wadau ebu tufanye kazi au mambo ya msingi tuache kumjadili NAPE kwa utumbo anaotoa.Huyo nape akili yake ni under 14 tumpuuze na upuuzi wake.Lets discuss important issues as GT
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!
 
Mkuu nadhani unatania tu!! Hainiingii akilini kwamba unategemea Nape apate uwezo wa kutafakari na kuchambua kauli za namna hii!!

Kwa upeo huo wa Bw. Nape namshauri hasiangaishe Mahakama, yeye atuandalie bilioni zetu tatu, aombe msamaha mbele ya mahakama na mambo yaishe!!
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Shinto!!!
Vilaza huwa nawaona lakini we kiboko!!
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Siyo kosa lako, kumbe wewe wa juzi!?
 
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!

Akili yako ndogo sana......Hoja kuu iliyopelekea Chadema kumshitaki ni "CHADEMA inapokea MABILIONI kutoka nje kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi"
 
Mipuuzi kama wewe inayofikiri kwa kuweka udini mbele mmebaki wachache sana. Na si muda mrefu unaweza ukajikuta umebaki peke yako.
Tatizo CDM walikuwa wanakanusha kuwa hawapokei pesa toka nje! Baada ya Nape Slaa anasema tunapokea ila sio nyingi! Wizi ni wizi tu hakuna wizi mdogo! Msijifanye Hamuelewi! ON top mnafadhaliwa na Chama chenye malengo ya Kikristo!
 
Ningependa kujua kutoka kwa Nape - Katibu Mwenezi CCM kama haoni tofauti ya kauli aliyoitoa mwezi uliopita kuwa CHADEMA kimepata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili wake kutoka nje ili kufanikisha M4C na ile aliyoitoa juzi Dr Slaa - Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa chama chake ni moja ya vyama vya siasa ikiwemo CCM vinapata ufadhili kutoka nje wa kujijengea uwezo?

Natoa hoja hii kwa kuwa nimemsikia leo Radio One akijiandaa kutumia kauli ya Dr. Slaa kama utetezi wake mahakamani alikoburuzwa na CHADEMA ili athibitishe kauli yake!

USHAURI: Namshauri Nape aweze kuchemsha bongo lake kidogo ili aweze kutofautisha hoja ambazo zina implication ya kisheria vinginevyo atakiliza chama chake CCM!

Nnape pitia kauli yako neno baada ya neno ili uone kama kauli yako na ya Dr. Slaa ziko sawa. Baadaye usije ukaona yanakulemea ukaanza kusema mbona hamkuishtaki CCM wakati ulikuwa unafanya kazi za CCM.
 
Binafsi sioni mantiki ya CDM kumpeleka Nape mahakamani kwa upuuzi kama huu
Ni ukweli ambao hatutaki kuukubali kwamba hii kesi kwa na nape ni kama kumsukuma mlevi chini
Hapo kabla CDM hakikuwahi kukiri hadharani kuwa kinapokea kiasi chochote cha pesa kutoka nje ya nchi, na baada ya Nape kupata taarifa CDM wanapata mgao kutoka nje ambao hata yeye anajua wanapata kwenye chama chake lakini akaamua kuutumia ukimya huo wa CDM kuwa wanapataa fedha toka kwa wafadhili na ndio inawatia kiburi ya M4C
Ukweli ni kwamba CDM wanapokea pesa kwa wafadhili na sio dhambi, na swala la kuvuruga amani anaweza kudai ni mara ngapi CDM wamedai nchi haitawaliki tena?

Sioni mantiki yoyote ya maana hapa katika hili
Sasa sijui haya mambo ya idadi ya pesa na zinatumikaje sio issue kwenye matamshi ya kisiasa
 
Back
Top Bottom