NAPE avimbiwa na MAWAKILI

Ni wakili gani anayetaka kuharibu rekodi yake kwa kesi isiyo na ushahidi maana inatakiwa uandae defence utaegemea wapi kama na ushahidi wa aliyoyatamka.Siku zote kuropoka kunaponza na kiburi pia au kulewa madaraka maana alipewa fursa ya kuomba radhi akakaidi.Ngoja tuone magamba wenzake watamuokoaje.
 
CHADEMA mnahangaika sana na kesi hii.....poleni sana!

Dogo Nape,

Kesi huwa haitabiriki, waweza shinda/shindwa. Vyovyote itakavyokuwa kwako hebu jaribu kuwa unasoma japo Maandiko kidogo ili utambue madhara yatokanayo na Kiungo Kiitwacho ULIMI......

MADHARA YA ULIMI

(YAKOBO 1: 26-27)
26Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, bali hujidanganya moyoni mwake, dini yake mtu huyo haifai kitu. 27Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.

(YAKOBO 3: 4-8)
4Au angalia pia meli, ingawa ni kubwa sana, nazo huchukuliwa na upepo mkali, lakini hugeuzwa kwa usukani mdogo sana, ko kote anakotaka nahodha. 5Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! 6Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu katika ya viungo vya mwili wetu. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanam. 7Kwa maana kila aina ya mnyama na ndege, wanyama watambaao na wanyama wa kila aina, ndege, nyoka na viumbe vya baharini wanaweza kufugwa na vimekwisha kufugwa na binadamu, 8lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani, Baba yetu na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. 10Katika kinywa hicho hicho hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo. 11Je, chemchemi yaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi? 12Je, ndugu zangu, mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Wala chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

....Kwakuwa huu ni ushauri wa bure kwako....Its up to you to pick it up or to ignore....
 
usishangae, za ccm wanaweza wakakataa, hao wakikupa hiyo kazi uhakikishe na ushindi ni lazima. kwa hiyo hiyo condition inawabana kila mmoja anaamua kutema kazi. utachukua hela ya mwana ccm halafu usishinde! unajuaje kitakachoendelea?
 
eti na wewe mleta mada ni great thinker! this is purely rubbish. huyo atakuwa si wakili. kunawalioua wazi tena kwa kuonekana lakini mawakili walijitokeza, hata marando anaenda kuwatetea wahujumu uchumi waliowazi kabisa.

Kama unaiita mada rubbish! na wewe unayeijadili rubbisha thread tukuiteje?
 
hii ni story ya vijiweni tu....hakuna wakili anaekataa kazi bhana haijalishi kesi ikoje tena hii ya kisiasa.....
 
CHADEMA mnahangaika sana na kesi hii.....poleni sana!
wakina ritz wako loyal sana kwako mwenezi wa magamba,..wako fasta kukupa yanayojiri jf,..majibu yako ya upole sana leo,something is not right..tundu lissu kafiwa na baba yake yeye mzima mtakutana mahakamni kwenu
 
Walimtuma akaseme mambo ya upuuzi na kichokozi huku wakijua mambo hayo ni hatari kwa amani na utulivu unaoimbwa ili hali hauko! Naye akakubali bila kufikiri akaenda kuyasema, sasa ajiandae mambo hayo kumtokea puani huku wakimcheka na kumdharau. Hatimaye, atakuwa amejifunza na kuwajua wakubwa wake wazuri na wabaya kati yao. Baada ya funzo atakalolipata, harudii tena ujinga huo wa kupokea na kupeleka tu kama robot.
 
Back
Top Bottom