Nape atua studio za V.O.A, Afunguka kuhusu Rostam, Lowassa na Chenge

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Nape Nnauye ametua ktk studio za sauti ya Amerika(V.O.A) na kuzungumzia hali ya siasa ndani ya CCM.

Akiwa ameulizwa maswali ya mtego na uchokozi na mwandishi wa V.O.A Mary Mdoe kuhusu CCM kupoteza mvuto nape alikubali kuwepo kwa hali hiyo na kumtolea mfano Rostam kuwa alijiuzulu nafasi zake kwa kutekeleza maagizo ya NEC. Japo wakati akijiuzulu ubunge alitumia lugha ya "kisiasa"(kwa maelezo ya Nnape).

Kuhusu "wenzake" Nape alisema wanapeleka mswaada bungeni "kuzuia wafanyabiashara wasiwe wabunge"

CHANZO: Sauti ya Amerika (V.O.A)
 
Tatizo la huyu Bwana huwa anapenda kupigana huku amefumba macho..!
 
Huyu si kipaza sauti cha Nkwele?
Nape huyu huyu anayetuaminisha ubaya wa ccm ni rostam, chenge na lowasa....pumbaf sana.
Tatizo la huyu Bwana huwa anapenda kupigana huku amefumba macho..!
 
Huyu si kipaza sauti cha Nkwele?
Nape huyu huyu anayetuaminisha ubaya wa ccm ni rostam, chenge na lowasa....pumbaf sana.
Nape ni vuvuzela la JK, JK akitaka kukabiliana na hali fulani chamani anamtumia Nape. Tatizo la Nape hana msimamo kabisa, mara gamba mara sijui nini full kujichanganya.
 
Jamaa anatapatapa kila korna,kila kukicha utasikia mpya kuhusu Nnauye!Mfa maji huyo!
 
hamna kitu hapo bure kabisa, akifika Newyork ntajitahidi nimvae uso kwa uso ili nimweleze jinsi anavyojidhalilisha
 
aliweza kweli kuongea kwa ufasaha huyu maana hata lugha ya malkia ni shida tangu yuko bangaloo
 
Mwacheni aendelee na kampeni za kutaka EL na Chenge wafukuzwe chamani, will like to see the end of that drama!
 
Sasa CCM wanataka nani agombee ubunge? Kama wafanyabiashara watazuiwa, wafanyakazi serikalini nao wawekewe vizingiti nani agombee sasa? Nchi hii ina shida, unapomwona profesa wa chuo kikuu au kamishina wizarani wanaacha kazi zao kwenda kugombea ubunge jua iko shida. Miaka mitano ya ubunge unapata matibabu nje ya nchi, pensheni inazidi ya profesa au daktari bingwa aliyeokoa maisha ya maelfu ya watanzania kwa miaka 25. Kwa namna hii, kila mtu atataka awe mbunge. TUNATAKA KATIBA MPYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
This country bwana , watu wanakataaa vivuli vyao mara wanavikubali sijui tutafika kweli....
maana huyu jamaa kuna kipindi alikua anakiponda kinoma sisiemu sahivi kapewa kashavu eti chama kisafi na sifa kibao sa sijui kimebadilika baada ya yeye kupewa shavu??????????????
 
Nape anafanya kazi yake kama Katibu Mwenezi kwa ufasaha mkubwa. Amekuwa katibu mwenezi effective kuliko wote kwenye historia ya CCM kwa kipindi kifupi ambacho yupo pale. Anafanya kazi nzuri sana kupambana na mafisadi ndani ya CCM. Ni vita ngumu ambayo wenzake ndani ya CCM akiwemo Kikwete wote wanaiogopa na kukaa kimya wakimuacha yeye apambane peke yake.

Mtu yoyote anayepambana na ufisadi kama Nape anapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote. Hata kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA lazima umuunge mkono Nape kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi kwani hili ni jambo la kitaifa na si la siasa za ushindani.

Endelea kupambana Nape, Watanzania tunakuunga mkono!
 
By the time huyu dogo anamaliza hiyo ziara lazima tutasikia kuna jambo / mambo ameharibu...talking too much hata kama ni katibu mwenezi
 
Back
Top Bottom