Nape atua studio za V.O.A, Afunguka kuhusu Rostam, Lowassa na Chenge

Anaharibika ...laiti angejua njia ya kutokea asingepoteza muda wake hapo hata kama baba yake alikuwa huko...
 
Hatuwaungi mkono wanaoitwa mafisadi lakini pia hatumuungi mkono adui wao namba 1 Nape! Tuko upande gani?
Both "mafisadi" and "adui yao namba1" are the same side of the same coin so in my opinion there are nothing like sides to choose from.
 
Haende zake huko!mineno neno ndio iliyo mjaa tunataka kuona vitendo na sio maneno!
 
Nape Nnauye ametua ktk studio za sauti ya Amerika(V.O.A) na kuzungumzia hali ya siasa ndani ya CCM.

Akiwa ameulizwa maswali ya mtego na uchokozi na mwandishi wa V.O.A Mary Mdoe kuhusu CCM kupoteza mvuto nape alikubali kuwepo kwa hali hiyo na kumtolea mfano Rostam kuwa alijiuzulu nafasi zake kwa kutekeleza maagizo ya NEC. Japo wakati akijiuzulu ubunge alitumia lugha ya "kisiasa"(kwa maelezo ya Nnape).

Kuhusu "wenzake" Nape alisema wanapeleka mswaada bungeni "kuzuia wafanyabiashara wasiwe wabunge"

CHANZO: Sauti ya Amerika (V.O.A)

Mswada anaupeleka yeye na nani?????
 
Sasa CCM wanataka nani agombee ubunge? Kama wafanyabiashara watazuiwa, wafanyakazi serikalini nao wawekewe vizingiti nani agombee sasa? Nchi hii ina shida, unapomwona profesa wa chuo kikuu au kamishina wizarani wanaacha kazi zao kwenda kugombea ubunge jua iko shida. Miaka mitano ya ubunge unapata matibabu nje ya nchi, pensheni inazidi ya profesa au daktari bingwa aliyeokoa maisha ya maelfu ya watanzania kwa miaka 25. Kwa namna hii, kila mtu atataka awe mbunge. TUNATAKA KATIBA MPYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nimekusoma vema ndugu yangu Kiti. Na haswa katiba itakayo weka haki mbele kwa raia wote na sio ujanjaujanja.
 
Nape anafanya kazi yake kama Katibu Mwenezi kwa ufasaha mkubwa. Amekuwa katibu mwenezi effective kuliko wote kwenye historia ya CCM kwa kipindi kifupi ambacho yupo pale. Anafanya kazi nzuri sana kupambana na mafisadi ndani ya CCM. Ni vita ngumu ambayo wenzake ndani ya CCM akiwemo Kikwete wote wanaiogopa na kukaa kimya wakimuacha yeye apambane peke yake.

Mtu yoyote anayepambana na ufisadi kama Nape anapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote. Hata kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA lazima umuunge mkono Nape kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi kwani hili ni jambo la kitaifa na si la siasa za ushindani.

Endelea kupambana Nape, Watanzania tunakuunga mkono!
u

Sina Uhakika na uelewa wako, kimsingi naudoubt, Hivi hii saga ndo umeisikia leo au unakurupuka tu nakujidhalilisha? Unaweza kweli kusema Nape ni effective? labda kwa kubomoa si kujenga. Mafisadi hawawezi kuwa EL, Chenge na RA peke yao, Unajua hela za EPA kapewa nani? Rais si ndo mwenyekiti wa chama tawala? Simon Group wanaitaka UDA na bado hela za EPA hawajarudisha, unawajua hawa wewe? au ndo kudandia train kwa mbele, pole.
 
Ni Bangalore ndiko alikokamua degree yake nadhani,ni moja ya majimbo India uko
Nape ivi hajui kuwa anatumika kwa manufaa ya watu fulani,chunga wasije kukutenga kama ganda la mua malengo yao yakitimia!
 
Sinema inaendelea. Masikio yetu yanafaidi burudani ya mikanganyiko ya kila siku ya Chama "Twawala". Mpaka ufike Mkutano wao Mkuu 2012, patakuwa hapatoshi!
 
Nape anafanya kazi yake kama Katibu Mwenezi kwa ufasaha mkubwa. Amekuwa katibu mwenezi effective kuliko wote kwenye historia ya CCM kwa kipindi kifupi ambacho yupo pale. Anafanya kazi nzuri sana kupambana na mafisadi ndani ya CCM. Ni vita ngumu ambayo wenzake ndani ya CCM akiwemo Kikwete wote wanaiogopa na kukaa kimya wakimuacha yeye apambane peke yake.

Mtu yoyote anayepambana na ufisadi kama Nape anapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote. Hata kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA lazima umuunge mkono Nape kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi kwani hili ni jambo la kitaifa na si la siasa za ushindani.

Endelea kupambana Nape, Watanzania tunakuunga mkono!
Ni kweli kabisa, lakini tatizo la Nape yeye anapambana na Mafisadi, wakati huohuo anapambana na wanaopinga ufisadi yaani CHADEMA. kwa hiyo lengo lake si bayana
 
Mkuu fareed maneno mazito sana.

QUOTE=Fareed;2756059]Nape anafanya kazi yake kama Katibu Mwenezi kwa ufasaha mkubwa. Amekuwa katibu mwenezi effective kuliko wote kwenye historia ya CCM kwa kipindi kifupi ambacho yupo pale. Anafanya kazi nzuri sana kupambana na mafisadi ndani ya CCM. Ni vita ngumu ambayo wenzake ndani ya CCM akiwemo Kikwete wote wanaiogopa na kukaa kimya wakimuacha yeye apambane peke yake.

Mtu yoyote anayepambana na ufisadi kama Nape anapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote. Hata kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA lazima umuunge mkono Nape kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi kwani hili ni jambo la kitaifa na si la siasa za ushindani.

Endelea kupambana Nape, Watanzania tunakuunga mkono![/QUOTE]
 
Nape Nnauye ametua ktk studio za sauti ya Amerika(V.O.A) na kuzungumzia hali ya siasa ndani ya CCM.

Akiwa ameulizwa maswali ya mtego na uchokozi na mwandishi wa V.O.A Mary Mdoe kuhusu CCM kupoteza mvuto nape alikubali kuwepo kwa hali hiyo na kumtolea mfano Rostam kuwa alijiuzulu nafasi zake kwa kutekeleza maagizo ya NEC. Japo wakati akijiuzulu ubunge alitumia lugha ya "kisiasa"(kwa maelezo ya Nnape).

Kuhusu "wenzake" Nape alisema wanapeleka mswaada bungeni "kuzuia wafanyabiashara wasiwe wabunge"

CHANZO: Sauti ya Amerika (V.O.A)
Haka jamaa kanakula posho za kidola dola baada ya kuona posho za madafu za kukampeni udiwani zimegoma, kameibukia USA. Nasikia kalienda kuhamasisha ushoga pale Houston. Njaa mbaya sana, unajikuta unafanya vitu, au unaongea mambo ambayo nafsi yako haikubaliani nayo kabisa. Ukitoka US nenda kwa Kameruuuni pale No10 downing street.
 
Wakubwa heshima yenu!
WAKATI MWINGINE NASOMA THREAD HAPA NASHINDWA KUELEWA HASA LENGO NI KUJARIBU AKILI ZA WATU WAZIMA AU NI UELEWA MDOGO....( kwanza stori imegeuzwa miguu juu kichwa chini)..kama lengo ni kusema nilichokisema na kwa utangulizi alioutoa anaonekana kasikiliza mahojiano na kuamua kupotosha alivyotaka.
Lakini yapo maswali najiuliza sana;
1. HIVI KWANINI WATU WANAJARIBU KUJENGA DHANA KUWA VITA DHIDI YA UFISADI NA RUSHWA NI YA NAPE NA SI VIJANA WOTE WA KITANZANIA BILA KUJALI ITIKADI ZAO KWANI NDO WAATHIRIKA WAKUBWA WA RUSHWA KWANI WANAPATA ATHARI ZAKE LEO NA KESHO?
2. HOJA ZINAZOTOLEWA ZINALENGO LA KUNIKATISHA TAMAA NA KUNIDHALILISHA UTU KUFIKIA KIWANGO CHA KURIDHISHA NAFSI ZA WATOAJI, LAKINI SWALI HIVI NANI ATAFAIDIKA NA NANI ATAPATA HASARA NIKIVUNJIKA MOYO LEO NIKAKAA PEMBENI?
3. HIVI NI KWELI BILA AIBU MTU MZIMA ANAKUJA HAPA KUDAI NAPE ANA NJAA NDO MAANA ANAPIGANA VITA ANAYOPIGANA? BILA AIBU ANADAI NAZUNGUKA KWASABABU NATAKA POSHO?????? UNAJUA UNACHOKISEMA AU KWASABABU WE MWIZI WADHANI WOTE WEZI?????
4. AFADHALI LEO MMOJA KASEMA NAPIGWA VITA HII KWASABABU NAPINGANA NA CHADEMA, HIVI ULITAKA TUKAE CHAMA KIMOJA???? UNAYEDAI NAJIDHALILISHA, NI MIE AU NI WEWE UNAJITAHIDI KUNIDHALILISHA KWA KUNIPACHIKA SIFA ZISIZO ZANGU NA MATUSI JUU??? USICHOTAKA KUFANYIWA USIFANYIE WENZAKO.

5. HOJA YA NAPE UTUMIWA INA UA HESHIMA YA VIJANA WENGI WA AFRIKA, KWAMBA LEO KIJANA AKISEMA BASI HANA AKILI ZAKE MWENYEWE LAZIMA ANATUMIWA!!!!!! HIVI VIJANA WA KIAFRIKA HAWANA UWEZO WA KUSEMA WANAYOYAAMINI WENYEWE MPAKA WATUMIWE????

> SITAKATISHWA TAMAA NA MANENO YENU YA KEJELI NA MATUSI YA NGUONI MNAYOTUKANA....NITASIMAMIA NINACHOKIAMINI KWANI NDO IMEKUWA HESHIMA YANGU SIKU ZOTE ILIYONIFIKISHA HAPA LEO MPAKA IKIPITA SIKU HAMJAMJADILI NAPE JAMVI HALINOGI KWA BAADHI YA WATU... SO SITARUDI NYUMA, ENDELEEENI KUPOTEZA MUDA KWA AMANI.
 
Huyu Jamaa kweli kilaza hajui hata Katiba ya Nchi yakwamba kila Raia wa Nchi hii anayo Haki yakuchaguliwa nakuchagua kiongozi/viongozi huo mswaada apeleke Nec wasituletee huo utumbo bungeni.
 
Hatuwaungi mkono wanaoitwa mafisadi lakini pia hatumuungi mkono adui wao namba 1 Nape! Tuko upande gani?

Nape na hao anaowatuhumu ufisadi wote ni mafisadi tu wanachogombea ni uroho wa madaraka, kiini cha ugomvi wao ni 2015. Hawana jipya wala hawastahili support ya watanzania, ndiyo wale wale.
 
Back
Top Bottom