Nape apata aibu Serengeti

Ndugu zangu,
Jamii Forum ni social platform yenye heshima sana. Ni sehemu ambayo watu tumezoea kupata mambo ya msingi sana ikiwa ni pamoja na mijadala yenye masilahi kwa Taifa letu.

Lakini kwa mtiririko wa sasa kwa baadhi ya watu kutupia tu habari ili mradi wawe hewani siku hiyo si jambo jema na wala halina afya kwa forum hii. Tabia hii tusipo ikemea mapema itapelekea forum hii kupata taswira ya udaku kitu ambacho binafsi nisingependa kamwe.

Ushauri wangu ni kwamba watu watumie majina yao halisi humu maana naamini itawasaidia kutafakari kabla ya kuandika chochote. Vinginevyo itakuwa ni udaku form kitu ambacho forum kubwa kama hii haitafanana nayo.

Kama huu uongo wa mchana kweupe kabisa eti Nnape kazomewa Serengeti.

Nawasilisha.
nakuunga mkono kwenye majina ila kwenye kuzomewa kwa nape ni ukweli na wewe si ulikuwa gamba la kuvuliwa kule arusha?
na huyu dogo si kasema baada ya igunga waanarudi kwenye magamba?
 
Nape Ndungu Mpendwa, ni nani aliyekuloga hata ukaamini kilo moja ya sukari yaweza kukoleza bahari ikawa na utamu? Baba yako mpendwa angekuwepo angekueleza hili kwa umakini mkubwa. Kama Muasisi mwenyewe alisema hicho unachokinadi sio baba yake wala mama yake na je wewe Mpendwa unataka nani aje akueleza kuwa ulipo umepotoka kwani umeambiwa usikae barazani kwa wenye Mizaa nawe wakaa na kuchangamana nao wanao sababisha maafa kwa wapendwa wa BWANA, nape angalia ulipojikwaa ukatubu na kuongoka, Upendo wako unapoa Angalia siku zaja pale utakapo tazama juu na kukuta umebaki mwenyewe. Nape mpendwa katika BWANA nimeshindwa kukueleza hili kwa simu naomba kama ndugu na rafikio wa dhati nikuandikie humu ili uwe ukumbusho na uthibitisho wangu kwako.
Nape bwana anataka kukuinua lakini siko huko ulipo, Ujira wa kazi njema wa baba yako hautakufikia huko ulipo, Nape unawaziwa mabaya ondoka huko sio kwako. Na asikiae na afahamu.
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....
 
kaka angu asiyekujua atahamin uliyoyasema!ila ukweli nawe wachumia tumbo!baada ya minyukano yenu na wakina james milya,ni wazi upo kundi la nape!ni ukweli ulio wazi wewe si mpiganaji kama ulivyotaka ijulikane mwanzo!wewe unachumia tumbo na hilo lipo wazi!unadhani na kufikiri kwamba pengine kundi lenu laweza fanikisha ajenda yenu ya kupata rais!na pengne ukaukwaa ukuu wa wilaya au mkoa!!ndugu yangu mrisho,watanzania wamebadilika!!unafiki wenu wa wa wakina sitta utafika mwisho!sisemi haya nikitetea ufisadi(umonduli) ila ni ukweli ulio wazi kwamba ni bora ya chadema au ikibidi mafisadi kuliko ninyi wanafiki!!na kwa jinsi mafisadi walivyojipanga mtajuta!!jiulize kwa nini mmezuiwa kwenda igunga?ndio mmezuiwa ila amin bado hajategua mitego ya mafisadi!!ndo maana kila mbinu inatumika kuhakikisha igunga mnaichukua tena ccm kuwafunga midomo mafisadi ila bado na mtajuta!!kama una akili baki bila chama kama mimi,chagua chama makin!na tumia ujuz wako wowote kujitafutia riziki na sio tumbo wakla kufikiri kwa masaburi!!!
ndugu zangu,
jamii forum ni social platform yenye heshima sana. Ni sehemu ambayo watu tumezoea kupata mambo ya msingi sana ikiwa ni pamoja na mijadala yenye masilahi kwa taifa letu.

Lakini kwa mtiririko wa sasa kwa baadhi ya watu kutupia tu habari ili mradi wawe hewani siku hiyo si jambo jema na wala halina afya kwa forum hii. Tabia hii tusipo ikemea mapema itapelekea forum hii kupata taswira ya udaku kitu ambacho binafsi nisingependa kamwe.

Ushauri wangu ni kwamba watu watumie majina yao halisi humu maana naamini itawasaidia kutafakari kabla ya kuandika chochote. Vinginevyo itakuwa ni udaku form kitu ambacho forum kubwa kama hii haitafanana nayo.

Kama huu uongo wa mchana kweupe kabisa eti nnape kazomewa serengeti.

Nawasilisha.
 
CCM ukweli ambao pamoja na Nape hawautaki ni kuwa wamepoteza mvuto kwa wananchi, na wanatumia nguvu nyingi sana (DOLA) na watu individuals ili kushinda siyo sera wala nguvu ya chama inaonekana Igunga, bastola zinatumika, tindikali, kuchoma nyumba na kuwaangukia mafisadi waje wawasaidie na kuondoa viongozi wao kwenye kampeni
 
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....

Nape tumia akili kidogo mara moja moja .Unawezaje kuja foruma na kuandika message kwa capital letters zote ? Unaelewa maana yake ? Hebu jifunzeni kuandika humuj acheni mambo ya ajabu .Hii ni dharau kuandika kwa herufi kubwa zote .Rekebisha kwanza hili kabla hujaanza kujilinganisha na usiyo yaweza muongo mkubwa .Ulisema Zitto kashindwa kutinga Igunga sasa wewe na yeye nani kashindwa ? Wewe hutakiwi Igunga yeye alikuwa ana buy time .
 
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....

Kwa ufupi Ngd Mwenezi haujajibu hoja ya Igwa. Jee, ni kweli mkutano wako ulivunjika baada ya wewe kutukana CHADEMA?????????

Kama una lakusema juu ya Mbowe ingeleta maana kama ungelisema baada ya kujibu hoja ya Ige (umezomewa kwa kuitukana CHADEMA???).
 
Hii habari imepostiwa saa 6 usiku kwa saa za bongo. Ulikuwa wapi kupost tangu muda wa tukio? Au mkutano ulivunjika usiku? Hii source siiamini kabisa
Kwani mlielewana a-posti saa ngapi au ulimtuma kwamba mara tu mkutano wa Nape kwisha lazima a-post, mara nyingi magazeti hutoa habari ya jana yake hatujakusikia ukilalamika ni heri ya huyu kaacha usingizi wake kutuhabarisha inabidi tumpongeze.
 
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....
Kiongozi wa taifa badala ya kulinganisha sera unalinganisha ukubwa wa mikutano, halafu hujakana kuzomewa na mkutano wako kuvunjika inawezekana kuwa kweli pole sana.
 
Napee

Kama kawaida mtu anakuja na hoja nzito wewe unakuja na hoja nyepesi
hii inaonesha UTUPU ulionao kichwani jaribu kujifunza siasa na kupangua hoja
sio kuleta viloja na mikoja

Ushauri wa bure kwa Napee
Umepoteza mvuto kwa watanzania hasa vijana
1.jifunze kupangua hoja inapoletwa hoja nzito
2.Jifunze kujibu kwa ufasaha sio kwa matusi na kejeli
 
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....

Igunga utaenda lini mjomba? mbona unazunguka mbuyu?
 
Hivi huyu jamaa hajaweka kambi Igunga??? Nijuzeni maana sina taarifa yeyote kama alishatia mguu pale
 
Kama kweli umekwenda kutafuta ufalme Serengeti badala ya Igunga kwenye uwanja wa vita basi umekwisha kaka Napepesa......je ulikuwa na basitora yako au!! nenda igunga kaka,achana na akina MRAAAAAAAAAAAAAAA..watakutoa ngeu hao hawadanganyiki..Vipi magamba yamegeuka kuwa ngozi??
 
Igwa,
WATAKA WATU WAKUIGE KWA UONGO??? KUJIFARIJI HUMU NDIKO KUNAKOANGAMIZA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI. UKWELI HATA KAMA UNAUMA NI BORA KUUCHUKUA KAMA ULIVYO.... KUWA MKWELI, JANA KAFANYA MBOWE HAPA UWANJA HUUHUU WAAMBIE UKWELI WENZIO JINSI MKUTANO WANGU ULIVYOZIDI WA MBOWE KWA MBALI SANA NA JINSI WATU BAADA YA KUSIKIA UKWELI WALIVYO REACT KWA CDM....
Jibu swali ulizomewa hukuzomewa huwezi kwa namna yeyote ile ukazidi mkutano wa Chadema,propaganda zio zilizokushusha hadhi nakumbuka niliwahi kuandika post moja nikikuonea huruma jinsi ulivyomalizwa kisiasa umeingia kwenye kasri ya kusema uongo wewe ni muongo kama mwenyekiti wako Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu wako Mkuu MUkama na watendaji wa serikali yako akina LUhanjo,Jairo,Ngereja Pinda n.k Nape wewe sasa hivi umekuwa mmwagaji uharo wa maneno Pole Mzee
 
Back
Top Bottom