Paul Makonda: Katika uteuzi wa wagombea CCM itawasikiliza Wananchi wanasema nini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi ,uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri zaidi kusini mwa jangwa la Sahara Mheshimiwa Paul Makonda ameanza leo ziara zake rasmi katika mkoa wa Dar es salaam na kuendelea maeneo mbalimbali kwa kufanya vikao vya ndani na mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi mbalimbali ,kwa kuwasikiliza kero zao na kutoa majibu pamoja na kuelezea kazi na masuala mbalimbali yaliyofanywa na serikali ya CCM Katika utekelezaji wa ilani yake.

Ambapo pamoja na mambo mengi aliyoyazungumza na anayoendelea kuyazungumzia kadri anavyoendelea kupata nafasi amegusia kwa kina suala la uteuzi wa wagombea ndani ya CCM Katika nafasi za uenyekiti wa serikali za mitaa,udiwani na ubunge. Ambapo kwa ujasiri na dhamira ya dhati amesema kuwa CCM itawasikiliza wananchi wanasema nini juu ya watu wanaohitaji kupeperusha bendera ya chama.

Amesema kuwa kazi za mtu alizofanya ndio zitakazo mbeba na siyo habari za kujipendekeza kwa viongozi au kugawa kanga na chumvi au aina yoyote ile ya kutaka upendeleo. amesema kila mtu atabeba mzigo wake na chama hakita mbebea mtu mzigo pale wananchi watakaposema hapana.

Mimi Mwashambwa naunga kwa asilimia zote kauli hii ya Mheshimiwa Makonda kama ambavyo pia mwenyekiti wetu Taifa alisisitiza juu ya suala hilo la kuwa uchapakazi wa mtu na uadilifu wake na kukubalika kwake katika jamii ndio itakuwa kipimo cha kumpa mtu nafasi ya kugombea uongozi katika chaguzi zijazo, kusudi chama kisipate shida katika kuomba na kupata kura za ndio.

Niseme wazi kuwa mimi Mwashambwa niwe mkweli tu kuwa kuna majimbo mengi tulitapoteza mwaka 2010 na 2015 kwa uzembe wetu wenyewe wana CCM, ambao ulitokana na kuwasimamisha wagombea ambao walikuwa hawakubaliki kabisa na wananchi na kuwaacha wale wanakubalika na kuhitajika na. Wananchi.hii ilifanyika pale ambapo watu wanaosimamia uchaguzi ngazi za majimbo huko na huko mikoani kupofushwa na rushwa au kujuana au kubebana au kuleta dharau kuwa tutapita tu hata kama mgombea huyu wananchi hawamtaki katika jimbo hili.

Lakini pia makundi yalituathiri sana yaliyokuwa yanatokana na baadhi ya watu kugoma kuvunja makundi hasa pale mchahako wa uchaguzi unapoonekana haukuwa wa haki katika kumpata mgombea.ambapo wale wanaokuwa wanaona wamefanyiwa dhuluma walikuwa wanaamua kuunga mkono upinzani aidha wakiwa ndani ya chama au kuondoka kabisa na kuhamia upinzani.

Lakini pia ni lazima chama kihakikishe kuwa kinadhibiti Vitendo vyote vya rushwa ndani ya chama wakati wote wa mchakato wa kupata wagombea ,kusudi anayeshinda ashinde kihalali na kwa haki kwa nguvu ya hoja,uchapa kazi wake ,uadilifu wake,kukubalika kwake na uwezo wake kiuongozi na siyo kwa nguvu ya pesa .ambapo inaleta shida kubwa baadaye katika kumnadi mgombea ambaye anakuwa amepenya kwa nguvu ya pesa.

Lakini pia chama kiwe kinasikiliza kweli kweli sauti za watu maana unakuta wakati mwingine mtu amepata kura za ndio za wajumbe mia tatu(300) na alipata kihalali kabisa bila rushwa wala mizengwe ya aina yoyote ile .halafu anaachwa mtu huyu na kwenda kuchukuliwa mtu aliyepata kura 6 au saba ndio anapewa nafasi ya kugombea ubunge na kuachwa mshindi wa kwanza ,wa pili,wa tatu mpaka wa nne au tano huko anakwenda anachukuliwa mtu aliyeshika nafasi ya mwishoni huko bila maelezo ya msingi kwanini apewe yeye.

Jambo hilo limekuwa likikiumiza sana chama ambapo lilifanyika sana na kutokea kwa kiasi kikubwa sana sana mwaka 2020 kwa watu wengi kukatwa katwa ukilinganisha na miaka ya huko nyuma. jambo hilo linampa hata kiburi mgombea anayekuwa amepita na kuwa mbunge ambapo anaona kuwa ninyi wanachama ngazi ya jimbo hamna la kumueleza wala hawategemeeni kwa lolote na wala hawezi kuwasikiliza wala kuwa nanyi kwa kuwa ninyi mumpe kura au msimpe kura bado atapitishwa tu kwa kuwa ana watu wake ngazi za juu huko ambao anao uhakika kuwa jina lake litarudishwa tu kugombea.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom